Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Jamani hii Marry Me Now karibu itanifanya kichaa na my colleague, kuna wakati mpaka tunajisahau tunacheka kwa sauti SMH 🤦‍♀️
hahaha Unapitia kipindi kama ambacho nilichopotia na mwenzangu tunaitazama WAIKIKI 1, Tulikuwa tunacheka kwa sauti mpaka najiuliza hizi ni miye ndio nacheka hivi!! au nimefungiwa spika, maana hiyo Drama kwa vituko ni bora sana.
nina mpango wa kuirudia tena, Ingawa WAIKIKI 2 Imetoka ila sidhani kama ni mzuri kama WAIKIKI 1.
 
"The Temperature of language: Our Nineteen" kwa mnaoangalia ongoing imesihia episode 7 au kuna muendelezo? Sijaivuta maana google inaonyesha ina episode 16 ila kissiassian na wenzie ipo episode 7 tu
 
Hapo nimeangalia my golden life tu ipo poa. Hizo nyingine zimewekwa kando kidogo, hizi za episode 16 tamu sana na historical fupi fupi zilinibana kwa muda.
 
PATA 500 KWA KUDOWNLOAD APP YA TIGOPESA
Wadau fursa imejitokeza sio ya kukosa kabisa...
kama una tumia laini ya Tigo zama play store download app ya Tigopesa na uifungue weka namba yako watakutumia verification code weka baada ya hapo watakuomba promo code weka 👉 ROBL5582 ili upewe hiyo jero ni lazima uweke hiyo promo code
 
Nenda Chrome Tafta VIDMATE APK download+install afu bonyeza hiyo link ulopewa itakupeleka mpaka YOUTUBE ukianza kuangalia italwta ki mshare cha Share unakibonyeza utaletewa machaguo itafte download video ibonyeze itakupereka moja kwa moja Vidmate ita analys data afu italeta FORMAT TOFAUTI (QUALITY) Ko utachagua kama 360,720 au 1080 Itaanza ku DOWNLOAD yenyewe tu.
Shukrani sana, ila nilihitaji ni- download


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh 500 tu nilidhani pata GB huu umaskini mbaya tumefikia huku aiseee
 
Umeongelea kwa kirefu na kwa upana zaidi. Huwa sipendi kuangalia drama za kikorea zenye waafrika ndani yake maana kama hawata mchezesha kama jambazi mfano descendants of the sun kule urk basi watamchezesha mbea balaa mfano top management(haka kajamaa kamemzidi hata lokole halafu ana mdomo kama mondi basi balaa tupu,japo ni kipande cha dakika tu)

Kijana aliyekata tamaa ya maisha au kutaka kujiweka mbali na dunia anaitaja afrika kama sehemu ya kwenda huku wenzie wakishtuka anaenda pabaya

Mtoto au kijana wa kitajiri akileta ujeuri anatishiwa kutupiwa afrika. Hawa watu tunawapenda ila ni wabaguzi balaa
 
huenda ni kwa sababu tulikuwa tunalingana nao sana kimaisha kabla ya vugu vugu la mapinduzi na uhuru kufanikiwa, kitendo cha wao kutuacha nyuma baada ya uhuru ndio kunawafanya waamini ya kwamba waafrika wote ni jamii isiyojielewa

mikakati mingi waliobuni kwa lengo la kujikwamua na umasikini iliwapa mafanikio tofauti na sisi (matokeo yake tumeishia kuwa omba omba).

kejeli zao zina ukweli ndani yake lakini njia wanayoitumia kuwasilisha kejeli hizo si sahihi baadhi ya nyakati
 
Ujinga WA fikra za kibaguz zimetokana na uwezo WA viongozi wetu.
Tunaitwa wajinga na ukweli ni hivyo, tazama drama zao na zetu au linganisha maudhui ya miswaada yao au bajeti hata pia uhusika na wahusika.

Mifumo ya kiafrika ni ajabu na ya dunia ya 3 nyuma.
Hata wao walibaguliwa sana na wazungu mpaka walipoamua kuwa na akili ya kizungu ili kupambana na wazungu

Elimu, siasa uchumi bado ni kituko kwao acheni watubague tuwe na akili, wakati tunapata Uhuru tulikuwa sawa na China je Leo tuko wapi?
 
Hata wao walibaguliwa sana na wazungu mpaka walipoamua kuwa na akili ya kizungu ili kupambana na wazungu

Elimu, siasa uchumi bado ni kituko kwao acheni watubague tuwe na akili, wakati tunapata Uhuru tulikuwa sawa na China je Leo tuko wapi?
Acheni Maskhara, Umesema eti China?!!!.....!!!.
kwa taarifa yako Qing Dynasty iliwahi kutawala kiuchumi Duniani, kuanzia GDP na fact zingine nyingi za kiuchumi. na walishuka kiuchumi baada ya madhara ya vita dhidi ya Wajapan na baadaye waingereza.
Halafu hao wachina ambao unasema kuwa wazungu waliwabagua si kwa sababu hawakuwa na akili, laah!! Siku zote Unapaswa kuwa na akili uweze kumtambua mwenye akili. ni wazi kuwa Wazungu walitumia Ubaguzi na matusi as right tool to mask their incompetence.
China ni moja ya sehemu chache za Dunia iliyozalisha majitu yaliyokuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, mfano;-
Master Kong Fu zi ( Confucius), Meng zi ( Mencius), Laozi, Zhuangzi, Xunzi, zhu xi, zhuge liang( Greatest military Advisor katika history ya Dunia) , zhuang zhou n.k maana ni wengi mno. na walikuwa wanaishi vizazi mpaka vizazi. Ni wazi kuwa hawakuwa wanyonge.
Kwahiyo kama sisi tunataka tusonge ni lazima tuanze kubadilika sisi wenyewe ( Wananchi), People are the limbs of the Government, na Serikali inajengwa na watu, Serikali yenyewe ni kama msimamizi.
kwahiyo kabla haujailaumu Serikali itazame kwanza Familia na Jamii yako inazalisha watu wa aina gani? maana hizo tabia walizonazo ndizo zitakazo wajenga hata mpaka wakipata nafasi ya utumishi wa umma ndizo watakazofanya, kama ni njema basi tutakuwa na Serikali endelevu na Nchi yenye matumaini, kama wamejawa na uovu basi tegemea serikali masikini na Nchi isiyokuwa na matumaini na Dira.
Ubora wa Taifa lolote unategemea Ubora wa watu wake, kuanzia ngazi familia mpaka...
 
Mifumo ya inayoongoza familia inatoka kwenye Sera ya nchi pamoja na kazi za serikali.

Qing dynasty haikuwahi kutawala dunia kiuchumi labda unisaidie wakati UPI? Tunaposema dunia onyesha ulinganifu pamoja na Nguvu za kisiasa kwan uchumi unaendana na utawala

Ni kweli tamaduni zao Confucius na Mencius ziliwajengea hamu ya kusoma tangu kale. Tujiulize sisi waafrika kusoma tumeanza lini?

Huwezi kuwa na taifa bora nawakati elimu si utamaduni wenu. Fuatilia nchi za afrika zenye mifumo angalau mizur ya elimu hata siasa na uchumi angalau ni safi.
Lkn afrka wajinga ni wengi kuliko walioelimika hivyo tubadike kwanza na ndipo hatutabaguliwa
 
Zinasifiwa sana ngoja nizitafute maana waikiki niliwahi ivuta episode moja tu ikanishinda pale story ilipoanzia mtoto aliyetelekezwa maana hii story nshaiona kwa wahindi mwanzo mwisho kisha bongo movie wakaua kabisa kwa kuiiiga vibaya
View attachment 1419440

hahaha Naam, baada ya Burudani niliyoipata kwenye WAIKIKI, sasa nimeamua kuitafuta WAIKIKI 2.
Karibuni sana tucheke wenyewe kama vile hatujielewi.
 
Hahaha hiyo kitu iliwahi kunitokea wakati ambao nimemaliza kuitazama VAGABOND ambayo ilikuwa Hot Drama. nilipoitazama Episode ya kwanza ya WAIKIKI siku ielewa, almanusra niifute lakini baada ya kuitazama kama episode mbili tu za mwanzo,ohoo! nikaanza kuwa mrahibu wa hiyo WAIKIKI maana ni tamu kweli kweli full vituko ziandae mbavu zako. utakutana na chewbacca ( Bacca) na marafiki zake wa Waikiki Guest house.
miye nipo kwenye WAIKIKI 2.

Zinasifiwa sana ngoja nizitafute maana waikiki niliwahi ivuta episode moja tu ikanishinda pale story ilipoanzia mtoto aliyetelekezwa maana hii story nshaiona kwa wahindi mwanzo mwisho kisha bongo movie wakaua kabisa kwa kuiiiga vibaya
 
Kaka Nimechoka kutype.
kwa kifupi tu.
l Familia ndio ilianza kisha Zikawa Jamii na Jamii nazo zikaunda Taifa, na watu ambao walienda kuhudumu kwenye Serikali hizi ni watu watokao kwenye Familia na Jamii zetu.
mifumo ya malezi na Elimu walizopewa huko kwenye Familia na Jamii zao ndizo watakazoziishi hata mpaka wakihudumu serikalini, na watajenga mifumo hiyo Serikalini kulingana na aina ya malezi na Elimu walizopewa huko kwao, kama wamelelewa kwa ubinafsi, Chuki, utengano, wizi,uvivu n.k tegemea Serikali itakayoundwa haitotofautiana na, vitu nilivyovitaja, kwahiyo Taifa la namna hiyo haliwezi kuendelea na HalitokuA na kwakukosa Dira litapoteza mwelekeo.
kama watu hao wametoka kwenye Familia na Jamii ambazo zimewajenga watu wake katika Umoja, ushirikiano, upendo na katika misingi ya kupenda kujifunza, kuwa na bidii na uvumilivu n.k Jamii yenye watu wa namna hii endapo watapata nafasi ya kuhudumu serikalini lazima watajenga mifumo ya namna hiyo kwenye Serikali na Taifa hilo lazima litaendelea na litakuwa na Dira.

kwa kifupi sana.
unaposema Elimu sio utamaduni wetu unanishangaza sana, kwahiyo Waafrika Waumbwa kuwa masikini ama wajinga?( naomba majibu)

kwa kifupi sana Ming Dynasty ilikuwa inaingoza kwa uchumi Duniani kuanzia miaka ya 1490 mpaka baadaye ilipounda Qing Dynasty mwaka 1644, na Qing Dynasty iliendelea kuongoza mpaka 1900. na katika miaka yote hiyo ya kutawala China bado India ilikuwa namba 2.
kisha baadaye miaka ya 1900s zikaja nchi kama British,Japan, German, France , US, Russia n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…