Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

lee joon gi anarudi na drama mpya inaitwa FLOWER OF EVIL itaanza tarehe 29.7.2020 🔥....kwa wenzetu wakorea wataangalia kupitia tv chanel ya TVN sisi wabongo tutaangalia online kupitia kissasian .sh!
 
Nani ame check It’s okay not to be okay ep 9 jana?
Daamn hii drama ni [emoji91][emoji91]
Kim soohyun hii drama anaitendea haki kwa kweli

Yaaan Yuko vizuri,alililia kwa hisia utasema kweli kumbe igizo tu,hadi chozi lilinitoka.
yuko njema ndo maana anaongoza kwa kulipwa vizuri
episodes 12 imeendeleaje?
-------------------------------------------
autism spectrum disorder ni ugonjwa usiomzuia mwanadamu kupenda;
nimenusa harufu fulani ya wivu alionao kaka mkubwa (sang tae) dhidi ya mdogo wake(gang tae) na inaonyesha dhahiri ya kwamba gang tae si kwamba anampenda Ko Moon-Young akiwa kama muandishi wa vitabu bali anampenda kama mwanamke anayepaswa kuwa wake kiuhalisia na si ndotoni,
  • kuna scene fulani koo moon young alitaka kulala pamoja na gang tae (baadae walilala pamoja) , sijui kulitokea mjadala gani yule bwana gang tae akamwambia brother wake pipes ya maji imepasuka ndio naitengeneza hivyo basi usitoke nje (kwa lengo asije kumuona yule binti), asubuhi walipoamka aligundua ya kwamba amedanganywa na mdogo wake (alikereka kwa sababu hapendi kudanganywa), ila kilichomkera zaidi ni kitendo cha binti kuvaa nguo za mdogo wake usiku kucha (kivyovyote alitaka binti azivae nguo za kwake yeye)
  • kuna scene fulani gang tae alimyoa (kumkata) nywele binti koo moon young na alimsifia sana ya kwamba amependeza, lakini kaka mkubwa alipokuja na kumshuhudia binti na muonekano wake mpya alichukizwa (kwanini binti amekata nywele) na kilichomkera zaidi kwa nini mdogo wangu anadai ya kwamba binti amependeza
  • gang tae alipomletea saini feki ya binti tulishuhudia hali ya kukasirika kwa kaka mkubwa sang tae
gang tae naye alipokuwa mdogo alikuwa na wivu sana dhidi ya kaka yake na sababu kubwa ni ile hali ya kaka kupendwa zaidi na mama kwa sababu mama yao alitaka gang tae awe zaidi ya mboni ya jicho yenye kumuangaza kaka muda wote, pia awe mtumwa au mlinzi wa sang tae kwa muda wote.

sang tae naye alikuwa na wivu dhidi ya mdogo wake na sababu kubwa ilikuwa ni afya (kwa nini nimezaliwa mgonjwa na si mdogo wangu).

ndio maana kwenye tukio la kuzama kwenye ziwa baridi kila mmoja alitaka kulipiza kisasi dhidi ya mwenzake
  • gang tae alisita kumuokoa kaka yake ili ajifie akiamini kifo cha kaka yake kitampunguzia madhila, baadae akaamua kumuokoa kwa huruma
  • sang tae baada ya kuokolewa naye akaamua kumuacha mdogo wake kwenye ziwa baridi ajifie
finally kwenye hilo tukio lililotokea hospitali ambalo sang tae anamlalamikia au kumpigia kelele mdogo wake mbele ya hadhira/hadhara (amezoea kumzodoa mdogo wake mbele ya hadhira/ hadhara) ya kwamba alimuacha akipiganie kifo chake kiuhalisia kaka mkubwa alikuwa anajizungumzia yeye mwenyewe (sote tunafahamu kilichotokezea ni kwamba yeye ndiye aliyemuacha mdogo wake).

kitendo cha gang tae kuwa karibu na binti hakileti tafsiri nzuri kiupande wake kwa sababu inaonekana dhahiri lengo lake ni kuwa pamoja na binti(rejea ule mchoro wa basi)

afanyeje ili amjengee muonekano mbaya mdogo wake:
acha nimzodowe mbele ya hadhara ndipo watu watakapomfahamu sura yake halisi,
oooooohhhhhhh! kumbe mdogo mtu alitaka kumuua kaka yake...... ndivyo watakavyosema wambeya na mafisadi vijisu na si viwembe
huyo wa mwisho hawezi kuwa ni sang tae (kaka) bali ni gang tae (mdogo) na huyo wa pembeni ni binti koo moo young ndivyo ninavyojiaminisha

simulizi ya sang tae na binti koo moo young inafanana na ule wimbo wa I DONT LOVE YOU ulioimbwa na Urban Zakapa (utatu mtakatifu).
ni rahisi kumpenda mtu ila ni vigumu sana kuingia naye kwenye mapenzi

 
Leo nipo nakupekua mkuu
 
Umenikumbusha huyu mwanadada @demiss na ile kashifa yake JF bhana
 
Nipo nacheki Doctor Stranger nikaona kwanza nitafute maoni yako kuhusu hii drama nikayapata kwenye page 350+
Kilichonisikitisha ulifall in love kwa manzi sijui ni nesi ama ni doctor kwa hyo hukuichambua ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…