Utakutana na 'mazombi' ya hapa na pale!
Kama wewe ni mpenzi wa filamu za namna hiyo (horror), basi na hiyo utapata kuipenda.
KINGDOM inamuelezea Mwana Mfalme wa Joseon aitwae Lee Chang ambaye katika harakati za kiuchunguzi kufahamu undani wa ugonjwa uliomkumba Mfalme wa kipindi kile (baba yake) anasafiri kuelekea mbali kidogo na mji ili kutafuta ufumbuzi juu ya suala hilo.
Lee Chang anafika katika eneo moja la kitabibu akiwa na mlinzi wake binafsi ama bodyguard na kubaini kuzuka kwa janga kubwa na la kushangaza la wafu kurejea katika maisha na kuwaua wale walio hai, janga ambalo tayari limekwisha leta athari kubwa katika eneo hilo. Huko anakutana na mfanyakazi mmoja wa kitabibu, mtu pekee aliyenusurika katika kituo hicho cha kitabibu, mwanadada unaweza muita Seo-Bi.
Ni jukumu la Lee Chang pamoja na ushirika wa watu wake wa karibu kupambana dhidi ya kuenea kwa janga hilo kubwa na la kutisha katika eneo hilo na taifa la Joseon kwa ujumla.
Nakutakia utazamaji mwema!