Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

hii elimu mbona imenipitia kushoto au nilikuwa nasinzia kipindi nafuatilia kiundani maisha ya Yi Ui Bang
 
Huku kwetu Pyongyang mambo ni shwari kabisa, ila ni marufuku kuangalia X, Kuvaa jinsi, modo, hereni, panki , kufuatilia movie za kimagharibi na kutumia misemo ya kimagharibi. Huku far east walikuwepo wanafalsafa wengi.
 

Nilikuwa nimemisss Drama toka three kingdom, Nasubiria hizo kazi.
 
Huku kwetu Pyongyang mambo ni shwari kabisa, ila ni marufuku kuangalia X, Kuvaa jinsi, modo, hereni, panki , kufuatilia movie za kimagharibi na kutumia misemo ya kimagharibi. Huku far east walikuwepo wanafalsafa wengi.
munaendelea kulinda mila na utamaduni usio wahusu kwa nguvu ya mshale, hata hayo masuruali mapana munayovaa mfano wa madeera hayakuwa sehemu ya utamaduni wenu.
mwambie bwana kim avae hanbok, tena zile zilizotengenezwa kwa vitambaa vya kimasikini
 
Nilikuwa nimemisss Drama toka three kingdom, Nasubiria hizo kazi.
na itakuwa series ndefu sana itakayobeba kwa mtiririko historia ya wafalme watano.
Nitafurahi sana kama watatuletea wanaume waliolelewa jeju, busan, pyeongyang ndio waziongoze hizo chronicles.
hawa waliozaliwa seoul watuache kwanza wenye jambo letu.
 
Hatmaye Nimeimaliza "The Age of warriors", yenye episode 158. Hii series haikuwaelezea tawala za kijeshi kama ingeelzea zote basi tungekuwa Episode 300 na kuendelea.
Unajua hili dude mwaka jana sikulifuatilia
nakumbuka niliishia episode za 90 baada ya archfield Yi Ui Mini kurudishwa mji mkuu na bwana mfalme
acha niangalie schedule itakavyokuwa nipate kushitua kiporo.
wale jamaa zake waliokuwa wanamtia ujinga alifufue taifa la shilla sijui waliishiaje.
wana mkakati wengine wanafurahisha sana,
unataka kuirudisha dola ya chagga ndani ya Tanzania inayochechemea
utapigwa mpaka uchakae
 
Operation Ji Jin hee yaelekea ukingoni
  1. undercover drama - (8.3/10)
  2. move to heaven drama - (8.3 /10)
  3. designated survivor: 60 days drama (8.3/10)
  4. misty drama - (8.5/10)
  5. second to last love drama (7.5/10)
  6. identical affairs drama / I have a lover drama - (9/10)
  7. blood drama - (6.8/10)
  8. dong yi drama - (9.6/10)
  9. jewel in the palace - (9.8/10)
  10. a word from warm heart drama - (6.8/10)
  11. the great seer drama :
Jambo kubwa lililonishangaza linalomuhusu ji jin hee na tasnia yake ya uigizaji ni hili:
asilimia 80 ya drama alizoshiriki na nilizoziangalia amekuwa nyuma ya kivuli cha muigizaji mwengine, namaanisha hata kama yeye atakuwa ndiye muigizaji mkuu wa kiume basi stori kwa kiasi kikubwa sana itahusu upande wa mwanamke hivyo hivyo kwa upande wa wahusika wa kiume(the great seer nayo nimeanza kunusa harufu hiyo)

Drama zote hizo nilizoziwekea wino mweusi uliokoza kama utakuwa umeziangalia basi utakubaliana na mawazo yangu

=========================

Hii drama (the great seer) ndio itakayofunga hii kampeni ya kuangalia project zote za ji jin hee zinazopatikana kwenye video streaming tofauti zinazohifadhi korean drama, Nimeshajifunza vya kutosha jinsi taifa la Goryeo lilivyosambaratika na baadae kuzaliwa kwa taifa la Joseon kupitia kwa watoto walewale waliolelewa na Goryeo ila si vibaya kujiongezea maarifa zaidi na zaidi kupitia pembe nyengineyo.

Waandishi wengineo niliobahatika kuangalia kazi zao (six flying dragons na jung do jeon) walijaribu kutuonyesha jinsi gani wanasiasa walishiriki kwa kiasi kikubwa sana katika kampeni ya kuanzishwa kwa taifa la Joseon, ila mwandishi wa the great seer yeye ameamua kunionyesha upande mwengine ambao sikuweza kuufahamu hapo kabla unaowahusu wataalamu wa elimu ya nyota jinsi walivyoshiriki kwa kiasi kikubwa sana kwa kumuunga mkono Yi seong gye katika mpango wake wa kuiangusha Goryeo.

Kinachonifurahisha ni kuona waandishi wote kwa kiasi kikubwa sana hawakwenda kinyume na maudhui ya historia kwa baadhi ya matukio walioyatengeneza kupitia kazi zao, kwa mfano hii episode 1 ninayoiangalia imeanza kwenye tukio lile la yi seong gye kuamua kusitisha vita dhidi ya Ming na hatimaye kurudi mji mkuu wa Gaegyeong.
muandishi wa the great seer kwa hii episode 1 niliyoiangalia amemchora bwana ji sung kuwa ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kumshauri Yi seong gye kurudi mji mkuu wa Gaegyeong na hatimaye akapambane na majaliwa yake (akishinda ni mapinduzi, akishindwa ni uhaini)

ukija kwenye Jung do jeon drama nayo imelielezea vizuri sana hili tukio na sababu zilizopelekea yi seong gye akatae amri ya mfalme ya kupambana kwa lengo la kurudisha ardhi ya liaodong iliokuwa chini ya Goguryeo ya zamani na hatimaye kurudi ikulu kupambana na general choi yeong (niliwahi kuandika huko nyuma mkasa huu), drama zote mbili (jung do jeon na six flying dragon) zilituaminisha ya kwamba sambong (jina lake halisi ni jung do jeon) ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kumshauri Yi seong gye arudi mji mkuu na hatimaye akapambane na majaliwa yake (akishinda ni mapinduzi, akishindwa ni uhaini).

kumbe siku za mbeleni anaweza kujitokeza bwana tukinao akatutengenezea historia ya yi seong gye na kwenye upande wa wana mkakati akamchora mtaalamu wa mapishi wa yi seong ye kuwa ndiye mshauri mkuu wake na isiwe dhambi wala kosa kisheria.
 
Inshaallah kitakachofuata baada ya hapo
  1. operation so ji sub
  2. operation ji sung
wote hao sikuwahi kuwapa heshima inayostahili kupitia kazi zao, nitailazimisha nafsi yangu izipende project za hao wanadamu bila ya kujali mwaka husika wa projects zao.
waswahili wana msemo wao "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo"
 
Kwenye ubora wako daah hayo yote unayafatilia utadhani hauishi kwenye ulimwengu wetu wa kuisoma namba.

Nipo busy na utengenezaji wa noodles sijui ndo tambi zetu hizi ndani ya a hundred year's inheritance kwama kawaida family drama ya ep 50

Huyu mbaba hapa jin hee nilikua nikimwangalia namuona kama Mwendazake ila tatizo huyu hana ubabe nilitamani niingie kwa tv kumuambia aache uboya anamuaibisha pacha wake wa kikoromije aongeze kaubabe kwenye uigizaji wake kazidi mno upole.
 
Me too(ila mie nipo disappointed hakuna romance😂😂😂) Ni kweli ni ya kawaida maana wamerahisisha mno mauaji mpaka mtu unaona ni hali ya kawaida na wanaoua hawakamatwi wala kufanya jitihada kubwa kuficha. Story nzima inaendeshwa na watu watatu.

Nilichopendea ni Comedy za hapa na pale ila author ni kama alikua anasikilizia reactions za watazamaji ili arefushe au akatize aweke season two
Nimemaliza Vincenzo..sijajua ni kusifiwa sana ndio kukafanya niangalie nikiwa na high expectations au ni vipi..nimeona ya kawaida tu.

Nipo na Mr. Queen muda huu..ngoja tuone
 
Hee mimi hainifai....hata hivyo sikuwa na mpango wa kuitazama
Itafute drama inaitwa mask utafurahi kwa roho yako na utanishukuru binafsi najua taste za drama za Wanawake wanazopenda kama uliipenda Penthouse basi hiyo "mask" utaipenda pia.
Nimemaliza Vincenzo..sijajua ni kusifiwa sana ndio kukafanya niangalie nikiwa na high expectations au ni vipi..nimeona ya kawaida tu.

Nipo na Mr. Queen muda huu..ngoja tuone
Kabisa hiyo Vincenzo ni ya hovyo sana nimeangalia episode 1 tu haikunivutia nikaamua niachane nayo angalia hiyo "Mask" ni Kali Sana utanishukuru sana
 
Nimemaliza Vincenzo..sijajua ni kusifiwa sana ndio kukafanya niangalie nikiwa na high expectations au ni vipi..nimeona ya kawaida tu.

Nipo na Mr. Queen muda huu..ngoja tuone
Kuhusu vincenzo sijui ila Mr Queen niliinjoi sana aisee sikujutia kabisa bando langu. Na ili uinjoi zaidi inatakiwa uwe
mtazamaji wa historical drama......uusiache kuleta mrejesho
 
Sema tu hukuipenda huna haja ya kuweka hiyo ' hovyo sana' wakati umetazama episode moja tu
 
na itakuwa series ndefu sana itakayobeba kwa mtiririko historia ya wafalme watano.
Nitafurahi sana kama watatuletea wanaume waliolelewa jeju, busan, pyeongyang ndio waziongoze hizo chronicles.
hawa waliozaliwa seoul watuache kwanza wenye jambo letu.
Umenifurahisha sana sunbae
 
Ina vi comedy sana nayo..nilichoona japo kwa kuchelewa ni kuwa wakorea wana great sense of humor..hata kwa series ya kawaida hutokosa kucheka hapa na pale [emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…