Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

My watchlist kama ifuatavyo, Doom at your service, hospital playlist, imitation, nevertheless, train...

Nashusha penthouse s3 Ila Sina nguvu ya kuitanzama Kwa Sasa, Chicago typewriter kila niikitazama nastopisha kama chief Kim.

Loool nimepata uraibu mpyaaa king of mask singer wakorea wanaimba jaman...Basi nikiimaliza hizo dozi za mara Moja Kwa wiki nakaa hapo


Park Bo young kwenye doom anajua sanaaa
 
Nilishajaribu mara mbili nikala za uso. Mara ya kwanza kuiona hio menu nilijiona bonge la mjanja nikaisaka laini yangu part two kung'uta vumbi nikaijaza bando saa tano na dakika 59 usiku huo fasta nikajitumia night bundle bwana weee sms ikaja nimelamba kifurushi cha bila kikomo wacha nifurahie,kuvuta episode 6 napokea ujumbe wa kifurushi kukaribia kuisha sijakaa sawa naambiwa kifurushi kimeisha kumbe wajinga wale walinipa gb 5 tu kwa 1500 na sio unlimited.

Mara ya pili nikajipa moyo labda walinishtukia ngoja nitumiwe na mtu wa mbali yaan mikoa miwili toka nilipo. nikatumiwa bando la usiku. sms ikaja nina unlimited ila sababu nshakua mwenyeji(kwa maumivu ya kudanganywa unlimited kumbe sio)nikaangalia salio kwanza nikakuta gb 5 tu na sio unlimited.

#wavutadramatunateseka
#boraamshapopo

Kwa style ya halotel tunaibiwa sana ndugu zanguni
 
Chicago ni majanga mengine nami nilikua naiangalia hivyo hivyo haina amsha amsha story imepoa mno bahati mbaya nilikua nimeivuta yote na kuifuta bila kuiangalia hasara kubwa
 
Chicago ni majanga mengine nami nilikua naiangalia hivyo hivyo haina amsha amsha story imepoa mno bahati mbaya nilikua nimeivuta yote na kuifuta bila kuiangalia hasara kubwa
Hahaha yaan nimevuta tano Ila haziamshi
Watu wengi walirecomend wakat natizama Mr. Sunshine Ila imekuwa tofaut na expectation zangu.
 
Ohoo bora nimeiona hii repyl..hivi nilikuwa nataka ninunue vocha ya buku mbili nijiunge maana nnazo line mbili ingekula kwangu
 
Mwezi huu nimeshuka miaka ya huko

nipo ndani ya

1.Take care of us captain

2. Youth of May(nimeimaliza) 2021

3. Navillera 2021

4. The sweet blood(naona ya kitoto kufikirika ila nimeipenda) 2021

5.Second to last love

6. Gye baek

7. cantabile tommorow

Stock ya kutosha kufaidi usingizi kwa wiki kadhaa
 
Navillera nzuri sana
So inspiring yaani
 
Wadau naomba mnipe site ninayoweza ku download ancient Korean Dramas (zile kama Jumong n.k) for free.

Atakae niwezesha kupata pa kudownload nitamtupia voucher.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…