Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

1625744721108.png

Leo Nimeikumbuka Hii Drama Hasa Baada Ya Kusikiliza Moja Ya Ost Yake- 걱정말요 (Don't Worry)

Mwandishi Apa Alifanya Kazi Yake Hasa.

Ending yake jaman nlitaman awe na Yule mwingine Ila kama alivyosema mwenyewe timing tu
Ila Kwa Maisha Halisi Ni Wanadate, Kamkosa Kwenye Kuigiza Kampata Kwenye Uhalisia.
Ni Moja kati ya Drama Ilonisafirisha Kihisia Sana, Nimekua Kwenye Mazingira Yanayofanana Na Yale Kwa Asilimia ya Kati.

Namna Vyakula Vilivyokua Vinatembea Nyumba Mpaka Nyumba Ilinikumbusha Mbali Sana,Mtaani Kipindi Iko Ikifika IDD Kunakua Na MKEKA MMOJA Kwa Wakubwa na Wadogo Wao then Nyumba Zote za Jirani familia Zake Zinakusanyika Apo Haijalishi ni Dini Gani Ila Kila Familia Inapika Vyakula Vinakutanishwa Kati Vivyo Ivyo Ikifika Kwa Christmas ama Pasaka.
 
Eeh afadhali jaman nliwapenda sana

Yap hayo maisha yanaenda yanapotea baadhi ya sehem, Mimi pia nimeishi hivyo sema kuna mwaka ikabid tubadilike

Tulikua tukipika Eid na Christmas Sasa ikiwa chrismass vyakula vinakua vingi mno mpaka vya kulala na tuko familia kubwa. Tukaachaga kupika ikiwa sikukuu zakikristo maana majiran hufanya yao.

Kuna mwaka majiran wote walipata dharura chrismass ilikua mpaka sa 10 kimyaaa hahahha hatujapika jaman. Ukisikia hodi unasema hicho Kumbe Wala[emoji23], ikabid tuwashe moto tupike. Kumbe kuna aloalikwa, kuna alofiwa na babamkwe wakasafir usiku na mmoja mmewe alikua anaumwa figo akazidiwa.

Basi ikawa hivo mpaka leo sisahau Ila Bila kujua kila mmoja alituletea package Kwa wakati wao wavomaliza matatizo. Such a loving neighborhood yani
 
Huyu mpemba anataka kunigombanisha na ukoo wa mzaa babu yangu, hajui kama mimi ni shombe la kivietnam, nimekulia bara bahati mbaya

Kesi gani ngumu hivyo
tokea lini wavietnam wakaikataa hela kwa kisingizio cha utaifa.

umesahau ya kwamba shangazi K anatokea familia takatifu ila ni wakili mashuhuri anayesimama dhidi ya serikali inayozilea familia takatifu.
punguza visingizio ahjumma
 
Jamani jamani jamani wakati wa foleni ya nida ukasema mzaa babu ana undungu na mzee bulito wa nyerere leo hii ushapeleka damu Vietnam!!!??
hizo shughuli zake za uwakili sijui anazifanyaje ikiwa historia ya chimbuko lake imejaa utata.
huenda ni wakili slay queen wa kibongo

leo akizungumza atakwambia anamiliki shopping mall, kesho akipatwa na homa anatembeza bakuli
 
Numbisa mpe taarifa huyo mdogo wako, mwambie simuhitaji tena na wala asinitafutie wakili msomi wa kusimamia kesi yangu.
nina uwezo wa kusimama kama wakili msomi kwenye chumba cha mahakama licha ya kwamba ndiye mfunguaji mashitaka, natumai muheshimiwa jaji atakubaliana na ombi langu. Nimejifunza shughuli za kisheria kupitia korean drama kwa wiki mbili mfululizo, najihisi nipo fiti kuliko peter kibatala.
======================
nimetoka kuangalia legal drama zifuatazo

memory drama (2016):
Inazungumzia maisha ya mwanasheria Park Tae Suk, alikuwa ni wakili aliyeajiriwa na kampuni fulani inayotoa huduma za kisheria kwa taasisi na hata watu wa kawaida, alikuwa na rekodi nzuri sana ya ushindi, mchapa kazi na aliamini zaidi kanuni kuliko hisia wakati wa kazi. Siku moja huyu bwana alipata ajali ndogo tu ya gari lakini kupitia ajali ile alijikuta akipitia hali fulani ambayo si ya kutegemewa (alijihisi kama amepoteza kumbukumbu). Ile hali ilimchanganya kwa namna fulani na hatimaye aliamua kwenda hospital kwa dhumuni la kufanya checkup ndipo daktari ambaye ni rafiki yake wa karibu akamwambia bwana park una tatizo la Alzheimer na bahati nzuri tumefanikiwa kuligundua tatizo hili likiwa bado ni stage ya kwanza.
park aliendelea na shughuli zake huku ajiwengea lengo la kufuatilia ukweli juu ya kifo cha mtoto wake aliyempata kupitia mke wa kwanza aliyefariki kwa kugongwa na gari.
atachukua hatua gani pindi atakapogundua ya kwamba familia iliomuajiri ndio inahusika na mauaji ya mtoto wake kwa ajali ya gari?
hii drama nimeiangalia kwa muda mfupi sana kwa sababu ya jinsi ilivyoweza kuniteka kihisia muda wote.
nimeipa 8/10
the good wife (2016)
ni remake ya series ya kimarekani, Lee Tae-Joon na Kim Hye-Kyung ni wanandoa walio kwenye mahusiano kwa takribani miaka 15 ya ndoa yao na wana watoto wawili. licha ya kwamba wote walisoma shule ya sheria ila ni lee tae joon pekee ndiye aliyeamua kufanya kazi ambapo aliajiriwa kuwa prosecutor huku kim hye kyung aliamua kubaki kuwa mama wa nyumbani.

baadae Lee Tae-Joon anafungwa jela kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi likiwemo shitaka la kupokea rushwa ya ngono japokuwa yeye mwenyewe aliamini mashitaka hayo ni ya kupangwa kwa sababu bwana lee kabla ya hapo alikuwa anachunguza kesi kubwa ya ufisadi inayowahusu kwa kiasi kikubwa sana majaji pamoja na viongozi wakuu wa vyombo vya sheria mfano chief justice n.k

hatimaye mwanamama kim hye kyung aliamua kufuta vumbi vyeti vyake na hatimaye kuirudia fani yake ya uwakili na aliajiriwa kwenye kampuni binafsi inayotoa huduma hizo za kisheria, aliyemuajiri kwenye kampuni hizo ni rafiki yake wa zamani wa kiume na huyo bwana tokea chuoni alikuwa akimpenda sana kim hye kyung.
kitatokezea kitu gani pindi watu wawili hao wakiwa karibu,
je mama atamshamehe mume wake mwenye skendo ya kuchepuka zaidi ya mara moja tena kwa kurikodiwa.
je atapambana vipi na ulimwengu wa kisheria aliokwisha utelekeza kwa takribani miaka 15.
jamii hususani vijana watamchukuliaje mwanasheria huyo ahjumma aliyeamua kuvikumbuka vyeti vyake.
nikimwita super woman nitakuwa nakosea?​
nimeipa 7/10
 
Ya law school hujaiangalia?Japo nimeivuta episode 3 bado najivuta vuta kuiangalia maana sijamalizana na hii list yangu
Mwezi huu nimeshuka miaka ya huko

nipo ndani ya

1.Take care of us captain

2. Youth of May(nimeimaliza) 2021

3. Navillera 2021

4. The sweet blood(naona ya kitoto kufikirika ila nimeipenda) 2021

5.Second to last love

6. Gye baek

7. cantabile tommorow

Stock ya kutosha kufaidi usingizi kwa wiki kadhaa
Numbisa mpe taarifa huyo mdogo wako, mwambie simuhitaji tena na wala asinitafutie wakili msomi wa kusimamia kesi yangu.
nina uwezo wa kusimama kama wakili msomi kwenye chumba cha mahakama licha ya kwamba ndiye mfunguaji mashitaka, natumai muheshimiwa jaji atakubaliana na ombi langu. Nimejifunza shughuli za kisheria kupitia korean drama kwa wiki mbili mfululizo, najihisi nipo fiti kuliko peter kibatala.
======================
nimetoka kuangalia legal drama zifuatazo

memory drama (2016):
Inazungumzia maisha ya mwanasheria Park Tae Suk, alikuwa ni wakili aliyeajiriwa na kampuni fulani inayotoa huduma za kisheria kwa taasisi na hata watu wa kawaida, alikuwa na rekodi nzuri sana ya ushindi, mchapa kazi na aliamini zaidi kanuni kuliko hisia wakati wa kazi. Siku moja huyu bwana alipata ajali ndogo tu ya gari lakini kupitia ajali ile alijikuta akipitia hali fulani ambayo si ya kutegemewa (alijihisi kama amepoteza kumbukumbu). Ile hali ilimchanganya kwa namna fulani na hatimaye aliamua kwenda hospital kwa dhumuni la kufanya checkup ndipo daktari ambaye ni rafiki yake wa karibu akamwambia bwana park una tatizo la Alzheimer na bahati nzuri tumefanikiwa kuligundua tatizo hili likiwa bado ni stage ya kwanza.
park aliendelea na shughuli zake huku ajiwengea lengo la kufuatilia ukweli juu ya kifo cha mtoto wake aliyempata kupitia mke wa kwanza aliyefariki kwa kugongwa na gari.
atachukua hatua gani pindi atakapogundua ya kwamba familia iliomuajiri ndio inahusika na mauaji ya mtoto wake kwa ajali ya gari?
hii drama nimeiangalia kwa muda mfupi sana kwa sababu ya jinsi ilivyoweza kuniteka kihisia muda wote.
nimeipa 8/10
the good wife (2016)
ni remake ya series ya kimarekani, Lee Tae-Joon na Kim Hye-Kyung ni wanandoa walio kwenye mahusiano kwa takribani miaka 15 ya ndoa yao na wana watoto wawili. licha ya kwamba wote walisoma shule ya sheria ila ni lee tae joon pekee ndiye aliyeamua kufanya kazi ambapo aliajiriwa kuwa prosecutor huku kim hye kyung aliamua kubaki kuwa mama wa nyumbani.

baadae Lee Tae-Joon anafungwa jela kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi likiwemo shitaka la kupokea rushwa ya ngono japokuwa yeye mwenyewe aliamini mashitaka hayo ni ya kupangwa kwa sababu bwana lee kabla ya hapo alikuwa anachunguza kesi kubwa ya ufisadi inayowahusu kwa kiasi kikubwa sana majaji pamoja na viongozi wakuu wa vyombo vya sheria mfano chief justice n.k

hatimaye mwanamama kim hye kyung aliamua kufuta vumbi vyeti vyake na hatimaye kuirudia fani yake ya uwakili na aliajiriwa kwenye kampuni binafsi inayotoa huduma hizo za kisheria, aliyemuajiri kwenye kampuni hizo ni rafiki yake wa zamani wa kiume na huyo bwana tokea chuoni alikuwa akimpenda sana kim hye kyung.
kitatokezea kitu gani pindi watu wawili hao wakiwa karibu,
je mama atamshamehe mume wake mwenye skendo ya kuchepuka zaidi ya mara moja tena kwa kurikodiwa.
je atapambana vipi na ulimwengu wa kisheria aliokwisha utelekeza kwa takribani miaka 15.
jamii hususani vijana watamchukuliaje mwanasheria huyo ahjumma aliyeamua kuvikumbuka vyeti vyake.
nikimwita super woman nitakuwa nakosea?​
nimeipa 7/10
The good wife niliiangalia ina kombolela nyingi
 
sihitaji tena kuwekewa lists ya drama, nitaendelea kuzitafuta mwenyewe kama ilivyo kawaida japokuwa ni shughuli pevu.
nimesubiria wiki nzima nikitegemea wakorea wa JF watajitutumua kutoka usingizini.
mmeniangusha​
Baba Bora Hua Hakimbii Majukumu ata Kama Mtoto Akimtukana.., Usikasirike Baba Ahjussi
 
Eeh afadhali jaman nliwapenda sana

Yap hayo maisha yanaenda yanapotea baadhi ya sehem, Mimi pia nimeishi hivyo sema kuna mwaka ikabid tubadilike

Tulikua tukipika Eid na Christmas Sasa ikiwa chrismass vyakula vinakua vingi mno mpaka vya kulala na tuko familia kubwa. Tukaachaga kupika ikiwa sikukuu zakikristo maana majiran hufanya yao.

Kuna mwaka majiran wote walipata dharura chrismass ilikua mpaka sa 10 kimyaaa hahahha hatujapika jaman. Ukisikia hodi unasema hicho Kumbe Wala[emoji23], ikabid tuwashe moto tupike. Kumbe kuna aloalikwa, kuna alofiwa na babamkwe wakasafir usiku na mmoja mmewe alikua anaumwa figo akazidiwa.

Basi ikawa hivo mpaka leo sisahau Ila Bila kujua kila mmoja alituletea package Kwa wakati wao wavomaliza matatizo. Such a loving neighborhood yani
Kabisaa Na Inawezekana Kwa Umri Ule Labda Usielewe au Kufurahia Maisha Yale Ila Ukishakua ndo Unajua Utamu wa yale Mazingira,Bond Ile Dah! Sisi Tuliama Japo Ule Mji Bado Upo (Namaanisha Nyumba Tulokulia) na Baadhi ya Majirani Kufariki Na Nina Miaka Sijarud Tena Pale.

Ndomana Wanasema Mazingira Ni Muhimu Sana Kwa Ukuaji Wa Mtoto, Kuna Kumbukumbu Nzuri na Mbaya Unamtengenezea Mtoto Na Kamwe Hatokuja Sahau, Kwa Wakati Ule Anaweza Asijue AU Kuelewa Ila Zile Memory Zinaendelea Kusalia Kwa Ubongo Wake. Mi Ni Shuhuda Wa Hili.
 
hizo shughuli zake za uwakili sijui anazifanyaje ikiwa historia ya chimbuko lake imejaa utata.
huenda ni wakili slay queen wa kibongo

leo akizungumza atakwambia anamiliki shopping mall, kesho akipatwa na homa anatembeza bakuli
Leo mbabu wa kipemba, umeamua kususia kila kitu, ngoja nijidai nakupa ofa ya urojo hapa forodhani ili ukatae nipate kisingizio😒😒
 
Back
Top Bottom