Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Mapema tu tunasonga na kitonga nishapakua episodes kama 7 za mb chache
Screenshot_20220304-093250.jpg
 
Bad thief,good thief kwa aliyeiangalia je ni nzuri?
Mimi sikuimaliza, sio kwamba iliniboa ila aliyenipa alinipa nusu na mimi wakati huo ujanja wa kupakua sikuwa nao. Sijarudi tena kuangalia kwa sababu nikisema nianze mwanzo naona uvivu, nikisema nianzie nilipoishia kule nyuma nimesahau mambo mengi. Hiki kizungumkuti niko nacho pia kwenye missing you
 
Hakuna drama ambayo haipo Kissiassian.



site ipi? kissasian na nkiri hazipo
 
Hakuna drama ambayo haipo Kissiassian.



[emoji23][emoji23]. majina niliandika kama alivyoyaweka chief pale juu
 
Currently watching.

1. Through the darkness drama:

kumbu kumbu zangu ikiwa zipo sahihi kuanzia episode 6 muandishi ameamua kuturudisha kwenye mkasa wa ukweli wa kihalifu uliotokezea nchini korea mnamo mwaka 2003/04, kuna muhuni anaitwa yoo young chul(nafikiri bado yupo gerezani),

huyu fala alihusika na mauaji ya wanawake takribani 20. Alikuwa akiwalenga zaidi wanawake wanaotokea kwenye familia za kitajiri na alitumia nyundo kama ni silaha yake kubwa ya kutekeleza ushenzi wake.

huyo bwana alipoulizwa kwa nini anafanya mauaji hayo alijibu

Women shouldn't be sluts, and the rich should know what they've done."

mwishoni mwa mwaka 2021, mtandao wa netflix walirelease special documentary inayozungumzia mkasa mzima wa mauaji ya huyu bwana na wameipa jina la The Raincoat Killer: Chasing a Predator in Korea.


2. King of tears, taejo Lee bang won

hii drama ilisimama kwa takribani wiki tatu, hawa mabwana wanaozalisha hii drama walifanya dhambi isiosameheka ya kusababisha kupotea kwa uhai wa farasi waliomtumia kushoot tukio la yi seong gye kuanguka na farasi akiwa mawindoni. Ili kutengeneza uhalisia wa tukio waliamua kutumia farasi wa ukweli, wakaamua kumfunga kamba za miguu, katika kumuangusha farasi akaanguka vibaya na hatimaye baada ya siku chache farasi akafariki.

Hapo ndipo mgogoro wenye kuambatana na matamko ulipozuka ndani ya korea.
Mwanamke ni kama majani ya chai huwezi kuona nguvu yake mpaka uyachanganye na maji ya moto.

utakapoiangalia hii drama ndipo utakapofahamu nilichomaanisha.

  1. Yi seong gye alizungukwa na mwanamke mwenye ushawishi
  2. Yi bang won naye akaongozwa na mwanamke jasiri.
What next: ni vita ya kutoana roho Kati ya baba na mwana.



 
nilizopanga kuziangalia panapo uhai na uzima:
  1. our blues drama: mandhari yalee ya hometown cha cha cha. Humu ndani utakutana na waigizaji wenye Cv nzito ndani ya korea. Kuanzia lee byung hun, shin min ah, han ji min, cha seung won, kim woo bin. Sijui hii drama bajeti yake ni kiasi gani maana si kwa A list actors hawa. itaonekanwa netflix ifikapo April
  2. Again my life: lee jong gi na action project ni sawa na mpemba anavyopenda mihogo. Hii itakuwepo April.
 
Back
Top Bottom