Korean celebrities ambao wanatarajia kutumikia shughuli za kijeshi
(military activities) 2017
Kwa yeyote Yule ambaye ni mpenzi wa
Korean entertainment naamini kitendo cha korean celebrities kwenda kutumikia shughuli za kijeshi (military activities) ni jambo ambalo humuacha na huzuni sana kwa sababu atashindwa kumuona celebrity anayempenda kwa takribani miaka miwili (2). Kama ni mwanamme na umezaliwa 1997 kwa sasa utakuwa unatimiza miaka 20 ambao ndio umri ambao unapaswa kujiandikisha kutumikia jeshi hadi miaka 38 kwa sheria za korea kusini.
Celebrities wanapaswa kutumikia military activities kabla hajavuka miaka 30 ya kuzaliwa na baada ya kujiandikisha unapaswa kutumikia mazoezi kwa takribani wiki 4 katika kambi ya kijeshi na pia kutumikia miezi 21 katika kambi ya jeshi iliyopo eneo lolote,kama ni marine service utatumikia miezi 23 na kama ni air force ni miezi 24.
Hata hivyo wapo baadhi ya waigizaji ambao baada ya kurudi kutumikia military activities walirudi kwa mafanikio makubwa sana,kwa mfano
Song Joong Ki baada ya kumaliza miaka 2 ya kutumikia jeshi alirudi kwa mafanikio makubwa baada ya project yake ya
descendent of the sun kuwa ni drama bora kwa mwaka 2016.
Miongoni mwa celebrities ambao wametangaza kutumikia shughuli za kijeshi ni pamoja na :-
Big bang T.O.P:
Kama ulipata kuangalia IRIS 1 (2009) drama basi utakuwa unamkumbuka huyu jamaa,alicheza kama ni X killer (muuaji) anayetumikishwa na MR BLACK na BAEK SAN (iris) ,licha ya kuwa ni muigizaji ila kazi yake kubwa ni uimbaji ambapo ni miongoni mwa member wanaounda group la muziki linalojulikana kama ni BIG BANG, amezaliwa November/ 4/ 1987.
Siku ya tarehe
9/2/2017 ndio alijiandikisha kwa ajili ya kutumikia jeshi na anatarajiwa kutumikia wiki zake 4 za mazoezi katika kambi ya Nonsan Army Training Center.
Siku ya tarehe
8/2/2017 katika account yake ya instagram alipost picha ya chupa ya mvinyo (wine) ambayo alipokea kutoka kwa rafiki yake ambaye ni
LEE BYUNG HYUN ambapo aliandika
“kutoka kwa kaka yangu mpendwa ambaye pia ni rafiki yangu”
Chupa hiyo ya wine ilikuwa na ujumbe ambao umeandikwa na
Lee Byung Hyun
“
tafadhali naomba urudi ukiwa na afya njema na natumai muda ambao utautumia huko hautojisikia kama umeupoteza na natumai utakapo rudi tutapata muda wa kunywa pamoja”
Chupa hiyo ya wine ya kifaransa aina ya Chateau Petrus 1987 gharama yake ni won million 5 hadi 6 won million kwa chupa ($4370 hadi $ 5240) ambayo ni sawa na wastani wa Tzs 10 million hadi Tzs 12 million.
Wawili hao walikutana mwaka 2009 ambapo kwa pamoja walishiriki kwenye IRIS 1 drama ambapo LEE BYUNG HYUN ambaye pia ndiye mmiliki wa BH entertainment aliigiza kama ni KIM HYUN JUN (TK1) agent wa NSS.
JI CHANG WOOK
Amezaliwa july5 1987, ni actor na pia ni muimbaji ila mpaka sasa hajatangaza tarehe rasmi ya kujiunga na military activities, kazi yake ya mwisho itakuwa ni crime action movies inayoitwa
Fabricated City.baadhi ya nyimbo zake zimetumika kama ni original sound track (ost) katika drama alizoshiriki kama vile
EMPRESS KI, WARRIOR BAEK DONG SOO, K2. Amesema ya kwamba
“
kujiunga na jeshi nikiwa na miaka 30 itakuwa ni maisha tofauti, nina hamu ila nahofia”
SEO IN GUK
Amezaliwa Oct 23 1987, ni actor na pia ni muimbaji,mara yangu ya kwanza nilimuona kwenye historical drama ya
KING FACE ambayo aliigiza kama ni prince Gwanghae ambaye alikuwa ni mtoto wa mfalme
Seonjo,Gwanghae ni mmoja ya crown prince waliorithi ufalme kwa shida sana naamini kama umeangalia hii drama ,pamoja na JING BIROK: THE MEMORY OF IMJIN WAR, ADMIRAL YI SOO SHIN na nyenginezo utakubaliana na mimi kwa sababu kwanza alipewa cheo cha crown prince wakati wa vita kubwa sana dhidi ya japan ( imjin war vilivyodumu kwa miaka 7 ) Seo In Guk amesema ya kwamba
“
Nategemea kujiunga na jeshi pale ambapo nitapokea barua,nategemea kukutana na watu wapya na maisha mapya na anategemea atakua bado Na mwonekano mzuri atakapo maliza kutumikia military activities”
JOO WON
Amezaliwa Sep 20 1987, kazi yake ya mwisho ni historical inayojulikana kama ni
MY SASSY GIRL, alifaulu mtihani wa kutumikia
Seol Police Metropolitan Agency ila ameamua kujiunga na jeshi ambapo kwa sasa anasubiri tarehe ya kujiandikisha jeshini.miongoni mwa drama alizoigiza ni pamoja na
BRIDAL MASK, YONG PAL,GOOD DOCTOR, LEVEL 7.
LEE MIN HO
Amezaliwa jun 22 1987, ni actor na pia ni muimbaji, project yake ya mwisho inasemekana kuwa ni
LEGEND OF THE BLUE SEA, Minoz ambaye mwaka uliopita pia alicheza movie ya
THE BOUNTY HUNTERS alifaulu katika physical exam yake,na ameamua kutumikia katika huduma za kijamii kuliko kujiunga na jeshi.
JANG GEUN SUK
Amezaliwa aug4 1987 ni actor na pia ni muimbaji, mwenyewe anajiita Asia’s prince, mpaka sasa hajathibitisha kama atakwenda kutumikia shughuli za kijeshi ila amesema
“wala sijashitushwa na kujiunga na military activities kwani ni jukumu la kila mkorea mwanamme”
Miongoni mwa drama alizoigiza ni pamoja na
LOVE RAIN ambayo nyimbo yake ya love rain ilitimika kama ni ost
, HONG GIL DONG, JACKPOT (daebak),
YOU ARE BEAUTIFUL.
KIM SOO HYUN
Amezaliwa feb16 1988, ni actor ambaye ameigiza drama kama
THE PRODUCER,
MY LOVE FROM ANOTHER STAR,
THE MOON THAT EMBRACE THE SUN, GIANT (young seongmo), ila mpaka sasa hajaweka tarehe ambayo atajiandikisha kutumikia jeshi, amesema
“
atatumikia military activities baada ya kumalizia project ya movie yake mpya ya REAL premier”
YOO AH IN
Amezaliwa oct6 1986 ni miongoni mwa waigizaji wanaofanya vizuri nchini korea,ameshiriki drama kama vile
JANG OK JUNG,
FASHION KING, SIX FLYNG DRAGON, anategemea kutumikia na huduma za kijamii kuliko jeshi kwa sababu aliumia bega lake la kushoto.
Korean celebrities ambao wanatarajia kurudi uraiani baada ya kutumikia jeshi
KIM HYUN JOONG
ni actor na pia ni muimbaji ambaye alijiunga na jeshi tokea May12 2015 ambapo alikuwa ni border patrol na anatarajiwa kurudi mwezi huu wa February,ila kurudi kwake kunaweza kufufua upya kwenye vyombo vya habari lile sakata pamoja na aliyekuwa mpenzi wake ambalo bado lipo kwenye vyombo vya sheria.miongoni mwa drama alizoigiza ni pamoja na
BOYS OVER FLOWER,
PLAYFULL KISS.
PARK YOO CHUN
Ni actor na pia ni muimbaji na anatarajiwa kurudi August 2017 ambapo alikuwa akifanya kazi za kijamii katika maeneo ya Gangnam,mwaka uliopita alishutumiwa kwa kosa la sexual assault. miongoni mwa drama alizoigiza ni pamoja na
3 DAYS,
I MISS YOU,
THE GIRL WHO SEES SMELL.
CHOI SI WON
Ni actor na pia ni muimbaji ambaye ni member wa band inayoitwa Super Junior ambaye imekusanya vijana wenye vipaji vya kuimba kama vile
Super Junior Kyu Hyun, Super Junior Yesung anatarajiwa kurudi mwezi August ambapo alikuwa akitumikia jeshi la police,miongoni mwa drama alizoigiza ni pamoja na
ATHENA,
POSEIDON, SHE IS PRETTY.
Licha ya kuwa anatokea katika familia ya kitajiri Choi siwon na member wenziwe wa super junior ni miongoni mwa bendi zinazotengeneza pesa nyingi sana kupitia kazi zao za muziki.
LEE SEUNG GI
Miongoni mwa best actor nchini korea,
Miongoni mwa best ballad singer, kpop singer niliopata kuwashuhudia katika maisha yangu
Miongoni mwa best singer niliopata kuwashuhudia linapokuja suala la kuimba live
Je wajua lee seung gi ni mwanafunzi wa mwanamama
LEE SUN HEE gwiji wa muziki nchini korea.
Alijiunga na jeshi February mwaka 2016 na anatarajiwa kurudi October 2017.
Miongoni mwa drama alizoigiza ni pamoja
GU FAMILY BOOK.
MY GIRLFRIEND IS GUMIHO,
SHINING INHERITANCE,
YOU ARE ALL SURROUNDED.
NB:
Laiti kama sheria hii ingelikuwepo Tanzania basi ningelijirudisha umri kila siku,
hahahahahaaaaaa kishindo cha JKT na JKU sikiwezi na utawala wenyewe ndio huu mwaka wa pili mshahara haujapanda, mara unaamka asubuhi kambini hata mkate hamuna.na pembeni yako unamkuta celebrity DIAMOND PLATNUMZ amekata kipara munabaki kutazamana tu.
nongdam - ee - ehyo = (natania tu) = im just kidding
Dangyunhee jangnanigi = kweli natania = Of course I’m just kidding.