Nipo episode ya 25 ila bado roho haitaki kabisa kuona Gwanghae akiwa dethroned.
nimetoka kuangalia bossam: steal the fate drama ambayo ilikuwa na hadithi ya mfalme gwanghae.
naangalia hwajung drama ambayo imebeba simulizi ya mfalme gwanghae.
bado najaribu kuitafuta sababu ya msingi inayopelekea baba na mwana kuchukiana katika maisha ya kawaida hususani ya kiutawala.
ukiangalia jing bi rok, admiral yi soon shin na hwajung drama kwa nyakati tofauti zote zimetuonyesha uhusiano mbovu uliopo kati ya mfalme seonjo na gwanghae ambaye ni mwanawe aliyezaa na concubine.
hata ukiangalia medical historical drama zote mbili zinazoitwa hur jun nazo pia waandishi walituonyesha ill fated kati ya mfalme seonjo na gwanghae, ilifika hatua mfalme seonjo ni kama alikuwa na wivu wa kipuuzi dhidi ya gwanghae eti kwa sababu daktari bingwa (hur jun) alijiweka karibu sana na gwanghae kuliko mtoto wake aliyezaa na malkia (yeongchang).
stupid
why always gwanghaegun na seonjo?
kwanini waandishi hawatubadilishii mdundo.
natamani kanuni ya time travelling ifanye kazi kiupande wangu, ili nipate nafasi ya kuyashuhudia kiundani maisha ya baba na mwanawe, Je ni kweli baba alimchukia mwana kwa sababu za kisiasa au maandishi yanatudanganya?
pengine nikirudi nitaweza kuwabadilishia mdundo wa hadithi
unamchukiaje mwanao aliyekuwa mstari wa mbele kuilinda familia ya kifalme nyakati za uvamizi wa japan (imjin war), muda ambao baba amekimbia nchi yeye bwana mdogo amebaki ikulu (as the defacto ruler) kana kwamba haiogopi bunduki ya katoo kiyomasa na konishi.
hata huyo Injo waliyemuweka madarakani alikuwa kama panya mpunga tu mbele ya wanasiasa wenye uchu waliomuweka madarakani
huwezi kuwaongoza watu wanaokuchukia, kibaya zaidi ni watu unaowategemea wakupe msaada wa kiutawala.
chini ya utawala wa gwanghaegun ndio kiliandikwa kitabu cha tiba ya mashariki (dongui bogam), ukiangalia hur jun dramas (zote mbili utamfahamu kiundani huyo legendary hur jun na mikono iliojaa baraka ya utabibu)
Gwanghae aliangushwa na utabaka wa kisiasa (factions), hayo mengine ni viongezeyo tu.
==============
chawa wa ganghaegun amezungumza,
kutoka gereza la kiinua mgongo hapa jang'ombe uwanja wa punda