Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Drama yake nyingine niliyoona inaitwa Surgeon Bong Dal-hee ilikua inarushwa na Arirang tv miaka hio.

Drama zilizoruka Arirang tv miaka hio enzi ma-dish ya Arisat ni Lobyst, The King and I, Hello my teacher, Lovers, Brilliant Legacy, Super rookie ranger, Lets go to the beach, The land (Toji),

View attachment 2600493
Shukrani mkuu, vipi lakini hivi lobbyist iliweza kumaliziwa mpaka mwisho?. Maana mimi sijawahi kuipataga yote full.
 
Hii variety naona walienda kula na kucheka cheka tu😂😂😂😂
In-The-Soop-Friendcation-korean-drama.jpg
 
😂😂😂😂😂😂kweli ni ulevi mkubwa just imagine mie wa kufatilia ongoing variety kweli!!?hadi najishangaa tena ya kuchungulia watu wanakula😂😂😂😂
Wooga squad [emoji7]nawapenda ila variety siangalii...sitaki ulevi mpya
Hii ni ya kuongeza tu idadi ya varieties ulizoangalia haina mvuto. Nzuri ni jinny's kitchen inaisha ijumaa ijayo.
Wanavutia

Nzurii?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kweli ni ulevi mkubwa just imagine mie wa kufatilia ongoing variety kweli!!?hadi najishangaa tena ya kuchungulia watu wanakula[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hii ni ya kuongeza tu idadi ya varieties ulizoangalia haina mvuto. Nzuri ni jinny's kitchen inaisha ijumaa ijayo.
Jinny's kitchen naionaga insta inaonekana nzuri
 
Nipo episode ya 25 ila bado roho haitaki kabisa kuona Gwanghae akiwa dethroned.
nimetoka kuangalia bossam: steal the fate drama ambayo ilikuwa na hadithi ya mfalme gwanghae.
naangalia hwajung drama ambayo imebeba simulizi ya mfalme gwanghae.

bado najaribu kuitafuta sababu ya msingi inayopelekea baba na mwana kuchukiana katika maisha ya kawaida hususani ya kiutawala.

ukiangalia jing bi rok, admiral yi soon shin na hwajung drama kwa nyakati tofauti zote zimetuonyesha uhusiano mbovu uliopo kati ya mfalme seonjo na gwanghae ambaye ni mwanawe aliyezaa na concubine.

hata ukiangalia medical historical drama zote mbili zinazoitwa hur jun nazo pia waandishi walituonyesha ill fated kati ya mfalme seonjo na gwanghae, ilifika hatua mfalme seonjo ni kama alikuwa na wivu wa kipuuzi dhidi ya gwanghae eti kwa sababu daktari bingwa (hur jun) alijiweka karibu sana na gwanghae kuliko mtoto wake aliyezaa na malkia (yeongchang).
stupid

why always gwanghaegun na seonjo?
kwanini waandishi hawatubadilishii mdundo.

natamani kanuni ya time travelling ifanye kazi kiupande wangu, ili nipate nafasi ya kuyashuhudia kiundani maisha ya baba na mwanawe, Je ni kweli baba alimchukia mwana kwa sababu za kisiasa au maandishi yanatudanganya?
pengine nikirudi nitaweza kuwabadilishia mdundo wa hadithi

unamchukiaje mwanao aliyekuwa mstari wa mbele kuilinda familia ya kifalme nyakati za uvamizi wa japan (imjin war), muda ambao baba amekimbia nchi yeye bwana mdogo amebaki ikulu (as the defacto ruler) kana kwamba haiogopi bunduki ya katoo kiyomasa na konishi.

hata huyo Injo waliyemuweka madarakani alikuwa kama panya mpunga tu mbele ya wanasiasa wenye uchu waliomuweka madarakani
huwezi kuwaongoza watu wanaokuchukia, kibaya zaidi ni watu unaowategemea wakupe msaada wa kiutawala.

chini ya utawala wa gwanghaegun ndio kiliandikwa kitabu cha tiba ya mashariki (dongui bogam), ukiangalia hur jun dramas (zote mbili utamfahamu kiundani huyo legendary hur jun na mikono iliojaa baraka ya utabibu)

Gwanghae aliangushwa na utabaka wa kisiasa (factions), hayo mengine ni viongezeyo tu.
==============

chawa wa ganghaegun amezungumza,
kutoka gereza la kiinua mgongo hapa jang'ombe uwanja wa punda
 
Kwanza kabisa nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea( DPRK) .
Kwanza ukimya huu umejawa na mengi sana moja wapo ni majukumu lakini pili kwa takribani mwaka mzima nilikuwa sina access ya kureply au ku like chochote humu Jf.
ahsante Mungu kwa kuendelea kukuweka hai, hayo mengineo sijui internet ni mbwembwe tu za kiulimwengu.
nimekuwa mzanzibari badala ya daemushin/ daemusin ila khulka yangu haijabadilika hata kwa sekunde.

ndio madhara ya kujichimbia huko korea kaskazini, si useme tu muhuni kim alikupokonya mtandao ili ufocus na project ya kutengeneza makombora ya hwasong, nimesikia lile mulilolifanyia majaribio juzi lina uwezo wa kufika PEMBA ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom