Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

siku hizi wanatuletea mabishoo hata kuendesha farasi hawawezi mpaka watumie waigizaji feki na technology juu.
mdogo wangu mwaka huu KBS wanaadhimisha miaka 50 ya utoaji wa huduma ya habari, wahuni wameamua kutuzawadia hiki chuma ifikapo katikati ya mwaka.

chuma kinaitwa Goryeo-Khitan War.

A story of King Hyeonjong of Goryeo and Commander-in-Chief Gang Gam-Chan (Choi Soo-Jong). They unite the people of Goryeo to one and lead a war against Khitan.

baada ya miaka 10 hatimaye choi anarudi tena katika maisha ya periodic historical drama, huyu bwana yeye haogopi changamoto na miaka yake 60 ya kuzaliwa.
 
Huyu Rais wasasa( Yoon Suk Yul) huko S. Korea anakiherehere sasa dawa yake ipo jikoni, moon jae in alikuwa mstaharabu. Huyu wa sasa anatafuta mpk ushirika na Japan ili tu kumfurahisha Marekani. Amakweli Siasa na unafiki ni chanda na pete. Bora wangempa yule aliyekuwa gavana wa Gyonggi do Bw. Lee Jae Myung.

Mbali na hayo,
Namshukuru Mungu niko salama, na pia nimefurahi bado mzima kabisa. Naam nami sasa ni Gwanggaeto the Great na si Great Conqueror.
 
Nilikuwa nimemiss drama za kibabe kama hizo, huyo mwamba naomba asizeeke maana hawa watoto wetu mabishoo sana.
Imagine eti kwenye historical drama unamkuta Prince ni shoga?!!!! Anyway wazee kama hawa wakiingilia kazi hakuna kinachoharibika.
Kituo cha habari cha KBS nawakubali maana kwenye historical wako vizuri mno wakifuatiwa na MBC. Kazi hiyo itoke mapema tu.
 

huyo bwana pichani ndiye alipaswa kuigiza uhusika wa yeom mun kwenye emperor of the sea drama.
kama umeangalia lobbyist drama huyo bwana alimpenda sana yule dada aliyeigiza uhusika wa maria (Jang Jin-Young).

maisha hayana formular, kwenye lobbyist alikuwa mpinzani wa song il kook ambaye huku alimpokonya tonge mdomoni

pumzika kwa amani wewe dada (cancer ilimsambaratisha mnamo mwaka 2009, miaka miwili baada ya kuigiza lobbyist).

Numbisa nikiandika magazeti ya song il kook hufurahi sana na baadhi ya wakati hunichomoa makusudi.
wiki 6 nyuma alinichomoa akishirikiana na al hadid ila nikaamua niepushe vayolence

==============
behind every successful man there is a woman
katika project ambayo song triplets father naamini hawezi kuisahau ni emperor of the sea,
kabla hajapata offer ya kushiriki emperor of the sea alikuwa ni muigizaji wa kawaida nchini korea lakini baada ya kuigiza uhusika wa yeom mun ambaye alikuwa anateswa na mambo mawili makubwa nayo ni mapenzi na ambition alipata umaarufu mkubwa sana kwa mashabiki hususani wasichana.

najiuliza kwa nini wanawake wengi walioangalia emperor of the sea walimpenda yeom mun ambaye alikuwa ni muuaji aliyebobea kuliko jang bogo ambaye alikuwa ni mtu mwema?
wanasema kwenye maisha yako unayoishi basi kuna nafasi tatu
hayo ndio maneno aliyoyazungumza song il kook baada ya kumaliza sherehe za kufanikiwa kumaliza kwa salama kurekodi drama ya emperor of the sea.

wakati alipopata offer ya emperor of the sea Song il kook alipata kwanza offer ya kuigiza kwenye drama ya ADMIRAL YI SOO SHIN, lakini kutokana na ishu za kisiasa wakati huo mama yake alikuwa anagombania uongozi wa serikali basi kulipelekea mpango wa kushiriki kutokufanikiwa.

nilimchukia sana mama yangu kwa sababu nilikwisha jiandaa vizuri kimazoezi, kuendesha farasi na mapigano lakini kwa sasa naamini sikustahili kuigiza kwenye drama ile, kama ningelishiriki kwenye ile drama naamini nisingelipata nafasi ya kuigiza kwenye jumong (MBC 2006). alisema song il kook.


kuondoka ghafla kwa muigizaji ji sung kwenye drama ya terms of endearment mke wa director aliamua kumshauri mume wake ampe nafasi song il kook wakati ambao director alikuwa anahangaika kutafuta muigizaji mwengine.

mke wa director alivutiwa sana na uwezo wa song il kook kupitia morning drama ya album of life.
kwenye terms of endearment kuanzia episode ya 25 song alicheza uhusika wa mwanamme ambaye alitokezea kumchukia mke wake baada ya kugundua maisha ya zamani ya mke wake,umaarufu wake ulizidi kuongezeka hususan kwa mama wa nyumbani baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye drama hiyo na kupelekea kushinda tunzo ya best couple pamoja na mwanadada han ga in.

tukirudi kwenye emperor of the sea timu nzima ya waongozaji wa drama hiyo walikuwa kwenye mtihani mkubwa wa kutafuta muigizaji wa kucheza nafasi ya yeom mun, muigizaji Han Jae Suk ndiye wa kwanza aliyepewa nafasi ya kuigiza na alikuwa tayari alishamaliza photo shooting ya drama hiyo lakini baadae kukatokezea matatizo kwani muda wake wa kwenda kutumikia jeshi ulikwisha fika.

mwanamama chae sira (madam jami) ambaye alishiriki kwenye drama ya terms of endearment pamoja na song il kook akatumia ushawishi wake kumtafutia nafasi song il kook ili aigize uhusika wa yeom jang.
wakati director kang il soo akielekea nchini china kwa ajili ya film location alimuona song il kook ni muigizaji wa kawaida tu ndipo akataka ushauri kwa mke wake lakini kwa mara nyengine nguvu ya mwanamke ilimbeba tena song il kook.

mke wake alisema;
unasemaje ?
kwa sasa ndani ya korea kusini amekuwa maarufu sana baada ya kuigiza terms of endearment na ni bora uharakishe kumpa nafasi kabla hujachelewa. hivyo basi ndani ya drama mbili alipata msaada mkubwa kutoka kwa wanawake. hii ni chance of a life time.

wanaume tunapaswa tuwaheshimu wanawake lakini si kila mwanamke anapaswa kuheshimiwa na kusikilizwa (sentensi tata).

wengine wanapenda vayolence akiwemo numbisa
 
Nilikuwa nimemiss hivi vitu, yaan umenikaribisha.
 
Awesomeeeee. Gazeti la kufungulia Mei Mosi
 
Ni nzuri.Huko insta wamempenda V wa bts ila mie anayenifurahisha ni woo shik kajamaa kajanja ila kamekutana na Boss mjanja zaidi yake. Halafu sehemu waliyoenda kushoot hawafahamu kuhusu korean drama ila wanaifahamu parasite movie
V na woo shik ni best friends nadhani wamependwa wote. Kuna kipande cha interview niliangalia V anamdai woo shik kimchi containers eti mama yake alimpea kimchi hadi leo hajarudisha [emoji23][emoji23]
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚jamani. Wana reality nilipost picha asubuh wapo marafiki sita V,woo shik,seo jun,hyung sik. etc Naona Kila alipo actor mmoja kati ya hao watatu na V anakuwepo.

Na kwenye hii reality woo shik alisema Tae anapenda sana tambi kila akienda kumtembelea kazi yake kula tambi,saiv katoka kwenye janjamieon kwenda malkagusu sijui nimepatia spelling (sijaenda google)πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
V na woo shik ni best friends nadhani wamependwa wote. Kuna kipande cha interview niliangalia V anamdai woo shik kimchi containers eti mama yake alimpea kimchi hadi leo hajarudisha [emoji23][emoji23]
 
Kilichomfanya Seonjo amchukie Gwanghae ni ile kuhisi dogo kamshusha sana vyeo na pengine anamchukulia kama coward na muoga asiyesitahili throne, baada ya Ghwanghae kushinda ile vita (Imjin War). Kwa urahisi zaidi niseme kwamba, ule ushindi wa Ghwanghae ulikuwa ni humiliation kubwa sana kwake hasa baada ya kuficha mkia wake kwa uoga. kibaya zaidi Ghwanghae alikuwa akiutumia huo ushindi kama reference ya kuonyesha kwamba hawezi kushindwa kuongoza, pale ambapo mzee wake alionyesha kum-undermine.

Kwa urahisi zaidi tuseme kulikuwa na kiwango kikubwa cha insecurities kwa Seonjo dhidi ya Ghwanghe.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hicho chakula ulichoandika mbona sijawahi kukisikia. Halafu inaonekana ilikuwa sio mara ya kwanza kuongea kuhusu hizo containers kwenye interview maana mtangazaji aliuliza 'hajarudisha mpaka leo? [emoji1787][emoji1787][emoji1787] V akasema hajarudisha.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ni tambiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Kucheka kotee huku bado hutaki kuangaliaa varayatiii[emoji1787][emoji1787] mbona mgumu hivo

Mnaadisiana mapigo ya moyo yananienda mbio kama niishushe saiv ila jeuri sina[emoji1787][emoji1787]

Niko na out blooming youth kama utan leo nimetizama ep 9 dah
 

Iyo jinny’s inanihusu tuu

Sio kwa haya masimulizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…