Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!



Yi Bag Won( Taejong)

(SIX FLYING DRAGON POSTERS)

Kaka zote hapo tayari,
Hapo kwenye Six flying dragon inaingia kwenye 20 bora yangu, Mwaka 2015 Channel ya SBS walijitahidi sana kwenye hii kazi nadhani humu ndani kuna Martial arts za hali ya juu mno. Ila kabla yake ilikuwepo kazi inaitwa Jeong Do Jeon hii iliandaliwa na KBS, drama hii ilikuwa ikielezea zaidi maisha ya Sambong( Jeong do Jeon) na jinsi ambavyo aliiangusha Goryeo iliyokuwa imeoza na Kuianzisha Joseon. Ukiniuliza kati ya Six flying dragon ambayo ilifokasi na maisha ya Taejong( Lee Bang won) na hii Jeong do Jeon ya Sambong, nakwenda na Jeong do Jeon. Ingawa kazi zote ni nzuri mno.



Hapo ilikuwa battle of Legend Generals; General Choi Young( wa kulia) ambaye anahesabika kama Shujaa wa Goryeo, akipambana na Kijana wake General Yi Songgye( Taejo of Joseon)ambaye ni shujaa wa Joseon na msaliti wa Goryeo.
Hawa wote mpaka Leo wanahesabika Mashujaa wa Korea.
Lee min Ho aliwahi kucheza uhusika wa General Choi kwenye Drama ya Faith.


Sambong kwenye Jeong do Jeon drama. 2014 KBS1
 

[emoji91][emoji91]

Adamas ina season 2!???
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]unakosa uhondo
Kati ya hizo nimeangalia prison playbook na Weightlifting Fairy tu. Ni vile hazijafocus sana kwenye hiyo michezo na mimi sikufocus kabisa huko [emoji1787][emoji1787] hapo yenye unafuu ni ipi
 
Zote zimefocus kwenye michezo,kuna michezo mingine kuiona mpaka kwenye olimpic ila wakorea wanaicheza ndo nimeionea kwao pia. Zipotezee tu karibu kwenye realities 😂😂😂
Kati ya hizo nimeangalia prison playbook na Weightlifting Fairy tu. Ni vile hazijafocus sana kwenye hiyo michezo na mimi sikufocus kabisa huko [emoji1787][emoji1787] hapo yenye unafuu ni ipi
 
Zote zimefocus kwenye michezo,kuna michezo mingine kuiona mpaka kwenye olimpic ila wakorea wanaicheza ndo nimeionea kwao pia. Zipotezee tu karibu kwenye realities [emoji23][emoji23][emoji23]
Kwenye realities nako hamnipati [emoji1787][emoji1787][emoji1787] labda drama zinichoshe
 
Zote zimefocus kwenye michezo,kuna michezo mingine kuiona mpaka kwenye olimpic ila wakorea wanaicheza ndo nimeionea kwao pia. Zipotezee tu karibu kwenye realities [emoji23][emoji23][emoji23]

Tuendelee kumuhamasisha na realities jaman ataelewa tu


Nimeshusha jinny’s kwa nkiri, ina rangi nzuri japo dakika moja tu nimetizama

Nimependa hata intro ya masikhara, najikaza nimalize kuishusha ndo niitazame nshahisi itanikosesha usingizi[emoji23]
 
Ukiachana na hiyo ya bonus, hizo zote ulizotaja hapo juu nimebahatika kuziangalia, zote ni nzuri na sikujutua bando lango livha ya kuwa zina episode 50-60. Nyingine iliyostahili kukaa hapo ni HWAJUNG.

Ngoja niifuatilie hiyo bonus drama.
 
Soon atakuja tu😂😂😂

Nilijaribu kuangalia episode moja kutest kama nzuri nikajikuta mzima mzima naangalia zote na kusubiria zinazofatia,uzuri ijumaa tunamaliza ila nimenasa kwenye ongoing drama the secret romance guesthouse nzuri hii
 
Basi mtizame hata sugar dady wang nam goo min kwenye stove league akiwa na park eun bin (attorney woo).
Nilihisi unamzungumzia Namkoong min nikasema ngoja nijiridhishe gugo. Ila wewe kumbe katoto sana yaani huyu kwako ni sugar daddy [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Nitajaribu nikipata muda ambao hauna kazi [emoji16]
 
Hiyo Jinny's kitchen ina episode ngapi? Naweza kuangalia kwa sababu ya Tae
 
Nimeangalia K-drama nyingi za historical zikihusisha
himaya za (Goguryeo,Silla,Baekje,Goryeo,Joseon-hapa ndo za kumwaga-early Joseon, middle Joseon and late Joseon during Japan invansion, pia za Joseon-during independence fighting).



Kitu ambacho kinashangaza hawa wakorea jinsi wanavyo-depict historia yao kwenye maigizo zinaonesha himaya zao zilikua na nguvu sana na wababe sana. Drama nyingi za kihistoria toka Korea zikiachiwa mara nyingi wachina wanalalama wakisema historical kdramas baadhi zinakengeuka na ku-edit baadhi ya matukio halisi ya kihistoria tofauti na jinsi yalivyotokea hapo zamani.

Miongoni mwa himaya za mashariki ya kati na mashariki ya mbali basi;himaya zilizokuwepo ndani ya Korea wakati huo ( Goguryeo, Silla, Baekje, Balhae,Goryeo na Joseon) kwenye historia inaonekana zilikua himaya dhaifu kwa sababu :

1. Mgawanyiko ulikua mkubwa katika utawala. Wakorea ni watu wanaopenda kuwa katika makundi makundi ya ukabila, koo na kikanda hali iliyopelekea kukosekana kwa umoja miongoni mwao hivyo kuwa dhaifu na kupelekea kupigwa kirahisi na maadui zao.

✓Mfano China alitumia mbinu ya kuungana na Silla akampiga Goguryeo
na Baekje na kwa mfuatano na kuzi-conquer hapo ikaundwa Goryeo (Unification of the three kingdoms).

✓Joseon kulikua na mpasuko mkubwa ilikua kila baada ya muda wanapindua wafalme wao na kuweka wengine madarakani mvutano ukihusisha factions zenye mrengo tofauti kama (Sarim,Seo-in,Dong-in,So-ron,No-ron).



✓Hali hii imeendelea hadi karne ya 20 na 21 baada ya uhuru nchi imejigawa kuwa Korea ya kaskazini na kusini. Tangu zamani wenyewe ni wazee kuungana, kusalitiana, kupigana kisha kutengana.

2. Himaya za zamani za Korea zilipigwa na zikatawaliwa na karibia kila himaya mbabe wa enzi hizo.

✓Kwanza walisumbuliwa na himaya za China ya Wakati huo zikiwemo (Han, Ming,Liao/Khitan,Yuan,Tang na Qing,Jin).

Hizi himaya zilipigana vita kwa vipindi tofauti tofauti na himaya za Korea na baadhi zikafanikiwa kuwatawala wakorea na kupelekea wafalme wa korea kuongoza nchi kama vibaraka/viongozi kivuli hivyo kukosa maamuzi ya mwisho kama watawala.

✓Katika nyakati hizi watawaliwa walitumia lugha ya kichina katika kuandika, wakaletewa dini ya buddhism, na mfumo wa kuongoza falme zao ulifanania sana na mfumo uliokuwepo China.

✓Hapa drama nyingi zimeonesha hili zikiwemo Emperor of the sea na Chuno/Slave hunters.



✓Korea ilitawaliwa na Japan 1910-1945. Hili lilitokea juzi tu hapo dunia ikiwa imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja za teknolojia na viwanda.
✓Japan alikua ameendelea sana kipindi hicho. Kulinganisha Japan na korea ilikua kama mbingu na ardhi.
✓Kilichowaokoa kutoka katika huu utawala ni pale Japan aliposhindwa katika vita kuu ya pili dunia hivyo Korea wakapata uhuru wao 1945.

Drama zilizoonesha kwa uzuri maisha halisi yalivyokua Joseon chini ya utawala dhalimu wa Wajapan ni pamoja na The Land (Toji), Mr Sunshine na Pachinko.
zikionesha (mateso, manyanyaso, umaskini,mauaji ya wazalendo, mapambano ya kudai uhuru, wanawake wakisafirishwa kama watumwa)



✓Wakorea pia walipigwa na Wamongolia (himaya ya Yuan) . Mongol (Yuan) chini ya mtaalamu Genghis Khan mnamo karne ya 13-14 ilikua himaya yenye nguvu sana Asia na ilipenda vita. Yaani huyu mpuuzi Genghis Khan alikua mbabe sana kila akiamka asubuhi yeye anawaza kutanua tu mipaka ya falme yake na alifanikiwa kuitanua Mongol kwa kiasi kikubwa wakati wa utawala wake kwa kuzipiga himaya nyingi na kuzitawala.



✓Mongolia wakati huo ilikua ya moto iliitawala China, ikaitawala Korea, ilipigana vita na kuzi-conquer himaya kama Ottoman,India,Serbia,Poland, Bulgaria, Croatia, Hungary na Japan na ilishinda katika vita walizopigana na kutanua mipaka yake kuifanya Mongolia kuwa himaya yenye nguvu sana mshariki ya kati na mashariki ya mbali kwa wakati huo.



✓Nikiwaangalia Wamongolia sasa hivi walivyo masikini nikalinganisha na ubabe waliokua nao zamani nashindwa kuelewa imekuaje wamepooza hivi!!!!



✓Yuan dynasty (Mongol) chini ya mtoto wa 3 wa Genghis Khan aitwae Ögedei Khan iliingia vitani na himaya ya Goryeo na kujaribu kuitawala kwa vipindi tofauti katika karne ya 13 ikifanya uvamizi mara kwa mara takribani mara tisa (9) na baadae ilishinda vita na hivyo Goryeo ikatawaliwa na Mongolia (Yuan dynasty).



✓Utawala na Vita ya Mongol (Yuan) dhidi ya Goryeo imeoneshwa kwenye drama ya Empress Ki.



✓Himaya za Korea kwa vipindi tofauti zimeingia vitani dhidi ya Han,Qing, Tang, Ming,Japan, Mongol,Jurchens ,Khitans nk kwa vipindi tofauti tofauti.

✓Kitu kinachoshangaza kwenye Drama za wakorea tunazoangalia zinaonesha Korea lilikua dude kubwa ikiwa na watu-watu kweli wababe wa vita na wajuzi wa elimu ya siasa na sayansi ya ulimwengu waliopikwa kutokea Sungkyunkwan.



✓Historical figures walioshiba wamepambwa wakiwemo miamba kama Queen Seondeok,Lady/Empress Ki,mwanasayansi Jang Yeong-sil, Daemusin Muhyul, Jumong, General Yi Seong-Gye (King Taejo), Warrior Yi Bang-Ji, Yi-San (King Jeongjo), King Gwanggaeto, King Geunchogo,Yi Do (Sejong the great), General Choi young, General Kim Yushin, General Gye-Baek, Kim Suro, Bidam,Great scholar Jeong Do-Jeon (Sambong). Jang Bogo, King Yeongjo, Shin Sa im dang nk




✓Drama zinaonesha himaya za korea zilikua zimeendelea kimapigano na hivyo kupelekea kushinda vita nyingi, Pia zinaonesha korea ilikua imestaaribika na ni jamii bora kimavazi na vyakula, pia inaonesha kielimu ilipiga hatua kiasi ya Sungkyunkwan kutoa scholars wengi waliochonga mfumo wa uongozi wa vizazi na vizazi katika Joseon na baadae Korea ya Sasa.



∆Je, hawa wataalamu hawatufungi kamba kweli? na kuikuza historia ya nchi yao tofauti na uhalisia ulivyo? Sababu historia inaonesha yeye(Korea) ndiye aliekua kibonde wa wote akisumbuliwa na majirani wa karibu na wa mbali.


Hii imekaaje?
Gwanggaeto the Great
 
Nilihisi unamzungumzia Namkoong min nikasema ngoja nijiridhishe gugo. Ila wewe kumbe katoto sana yaani huyu kwako ni sugar daddy [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Nitajaribu nikipata muda ambao hauna kazi [emoji16]

Katoto wapi ni shangazi hapa[emoji1787]
Sema vile napenda hivo vi marioo vya korea inabid huyo awe sugardady tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…