Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Korean drama ambazo nishaziangalia so far:
Jumong,
Wind of the sea
the great queen(damdeok),
A man called God
Slave hunter (Chunno)
Iris
Gu family book
Time slip Dr. Jin
Giant..,

Nw naangalia "Warrior don so" lkn CD inascratch imeniuzi balaa
 
DramaTube
Mwenye njia ya ku dawnload series kutoka kwenye hii site katika format ya mp4 maana inakubali katika format ya 3gp please tupeane maujuzi.
 
Me napenda series za korea ila kwenye torrent sijawai kuziona kuna mtu anaweza nijuza jinsi zakuzipata wakuu msaada
 
DramaTube
Mwenye njia ya ku dawnload series kutoka kwenye hii site katika format ya mp4 maana inakubali katika format ya 3gp please tupeane maujuzi.

tumia PC utapata kwa mp4
lakini kwa simu inakuja 3gp 7bu unaingia kwa mobile hata link yake ni ya mobile section
 
Korean drama ambazo nimeangalia mpaka sasa hivi ni
* A man Called God
*Personal Taste
*Full house
*Take two full house
*City Hunter
*Emergency couple
*Your Beautiful
*Boys over flowers
*Liked or not
*Ad genius Lee tae Baek
*My love from the star
*Mask
*Gentleman Dignity
*I hear your voice
*Faith
*Healer
*Iris
*Hotel King
*Protect the boss
*Miss Korea
*My girl
*Coffee prince
*Secret Garden
*Pinocchio
*Oh my lady
*Fate to love you
*She was pretty
*My name is Kim sam soon
 
WAIGIZAJI WASAIDIZI WANAONIVUTIA (SUPPORTING ACTORS) NCHINI KOREA

Mara nyingi tumezoea kuwasifu waigizaji wakuu kwenye movies na drama(main characters) kutokana na uwezo wao wa kuigiza ila kiukweli wapo waigizaji wengine wanaosababisha hizi tamthilia za korea kuwa za kuvutia na kuburudishaa kwa mtazamaji.Inawezekana sijaangalia tamthilia nyingi sana za korea kulinganisha na wengine ila kiukweli tamthilia zao zinanipa athari nyingi sana kichwani mwangu na kuniacha na mawazo mengi na maswali yasiokwisha juu ya ubunifu wa waigizaji wao na jinsi gani wanavyoheshimu kazi zao.

1) JEON KWANG- LEOL: Amezaliwa 1959 nchini korea,watazamaji wengi wa drama za korea tumezoa kumwita GEUMWA kutokana na nafasi yake aliyotumia katika tamthilia ya Jumong (Prince of the legend) tamthilia ya mwanzo kumuona ilikuwa ni SWALLOW THE SUN ila sikumshughulikia sana kwenye ile drama ila alinivutia kwenye jumong,kusema kweli jamaa aliifanya jumong iwe ni bora zaidi.kwa mtazamo wangu ukimoundoa Song Il Kook kwenye jumong basi ni yeye aliipamba sana ile drama.pia nilimuona kwenye WARRIOR BAEK DONG SOO akiigiza kama Gwang Taek (SWORD SAINTS) na alionesha uwezo mkubwa wa kuigiza kuliko muigizaji mkuu kwa mtazamo wangu ambaye alieigiza kama baek dong soo.Tamthilia nyingine nilizoziona alizoigiza ni kama vile THE ROYAL GAMBLER(Jackpot), Flower in Prison,king and I, I miss You, king of baking,the man in the mask.

View attachment 360052

2) LEE JAE YONG:Amezaliwa 1963, mara ya mwanzo nilimuona kwenye tamthilia ya Emperor of the sea ambayo aliigiza kama mfanya biashara na ndiye aliyemnunua Jang bogo(choi soo jang) na kumfanya kuwa gladiator(mpiganaji), baadae nilimuona kwenye jumong ambapo alicheza kama waziri mkuu wa nchi ya BUYEO. Kiukweli aliigiza vizuri sana kwenye jumong licha yakuwa alikuwa ni mpinzani mkubwa sana wa mabadiliko ambaye aliamini BUYEO itakuwa na Amani kama itaendelea kuwa chini ya HAN DYNASTY.baadae nilimuona kwenye lobbyist ila hakunivutia sana labda kutokana na nafasi yake,tamthilia nyengine nilizomuona akishiriki ni YISAN,DEEP ROOT TREE,DONG YI,empress ki, aman called a god, the royal gambler,good bye mr black,the night watchman n.k

View attachment 360065

3) AHN KIL KANG: Sifikirii kama kuna tamthilia yoyote aliyocheza kama muigizaji mkuu ila kiukweli jamaa ni talent,haijalishi nafasi gani anacheza ila hatoacha kukuonesha uwezo mkubwa alionao jambo ambalo waigizaji wengine wanashindwa,kama unataka comedy,martial arts vyote anavyo.kwenye ILJIMAE alinivutia sana hususan zile harakati zake pamoja na mwanawe wa kike,pia kwenye QUEEN SEONDEOK ambayo aliigiza kama chil sook ambayo alishinda grand awards,tamthilia nyengine alizoigiza ni 3days, chuno,gye baek,shine or go crazy

View attachment 360067

4) JUNG HO BIN: MOON NO,DEAR MOON NO,DON’T DIE MOON NO,GROUND BREAKING MOON NO,DON’T DIE WOOTAE,nilimuona kwa mara ya kwanza kwenye swallow the sun ila sikumshughulikia sana,baadae nilimuona kwenye jumong akiigiza kama wootae ambaye alikuwa ni mume wa mwanzo wa Soseono, jamaa ana kipaji sana cha uigizaji hata kwenye Queen Seon deok alicheza vizuri sana.tamthilia nyengine alizoigiza ni Athena,Iris,Inspiring generation,baek dong soo,Poseidon, boys over flower,jeon woo chi.

View attachment 360068

5) KIM BYEONG KI: Wengi wetu tumezoea kumwita yeon- tabal ambaye alikuwa ni baba wa soseono kwenye jumong na ni miongoni mwa waigizaji walioipamba sana jumong tamthilia nyengine alizoshiriki ni land of wind,gye baek,empress chunchu,triangle,jang young sil.
View attachment 360069

6) AHN SUK HWAN: Unataka comedy,na mambo mengine huyu jamaa ni noma naweza kusema ni majuto wa korea haijalishi nafasi gani anacheza iwe ni modern au sageuk drama ni lazima atauvaa uhusika wake vizuri .nahisi mungu amemnyima martial arts tu. Ameigiza drama nyingi sana kama vile six fly dragons,bridal mask,deep root tree,slave hunter,boys over flower,personal test painter of the wind n.k
Ahn+Suk+Hwan.jpg

7) KIM KYU- CHEOL:Akiigiza mtu mwema utampenda na utasema hakuna mtu mwema kama yeye na akiigiza katili utasema hakuna katili kama yeye,anakipaji sana na kila akizeeka ndio anazidi.nimemuona kwenye drama nyingi ila alinivutia kwenye Daejoyoung ambapo aliigiza kama tactician wa Li Kaigu akiitwa Shin hong,pia kwenye king gwaggaeto alijitahidi sana kupambana na mzimu wa kaskazini a.k.a damdeok the conquery ila mwisho alikubali kujisalimisha yeye na kabila lake lote la watu wa Mohe.drama nyengine nilizomuona akiigiza ni crime squad,immortal admiral yi soo shin,land of wind,the merchant,age of warriors,bridal mask n.k
Kyu-cheol_Kim.jpg

8) CHEON HO- JIN: Amezaliwa 1960 ,ameigiza drama kama bridal mask ambapo alikuwa ni baba wa kimura shunji,unaweza kumpenda au kumchukia ila ni miongoni mwa waigizaji wanaofanya vizuri sana.tamtilia nyengine ni city hunter,six fly dragons,doctor stranger,good doctor.
View attachment 360071

9) JUNG HO KEUN: Hahahahaaaaaa kama kuna drama yoyote ambayo huyu jamaa ameigiza mtu mwema basi naomba muniambie, kwenye king gwaggeato alikuwa anaitwa general fengba (mkurugenzi wa fitina) na kwenye daejoyoung alikuwa anaitwa general sa bugu,kwenye emperor of the sea alikuwa anaitwa daechi, jamaa ni roho mbaya sana ila maisha yote hafanikiwi.
View attachment 360073

10) LEE WON- JONG: Ningestahili adhabu ya bakora 100 kama nisingelimtaja huyu jamaa,what a talent, Unataka nini kwake? Comedy?martial arts? Ukorofi? Basi jamaa sifa zote anazo,tamthilia nilizoziangalia mpaka sasa ambazo yeye ameigiza ni emperor of the sea,baek dong soo,princess jamyung,good bye mr black,body guard,king sejong,Iljimae, kim so ro,hidden identity,vanpire prosecutor,dr jin,empress ki, babysitter.

View attachment 360075

11) PARK CHUL MIN: Hahahahaaaaaa huyu jamaa hata kama atakuwa jambazi basi akija nyumbani kwako kukuibia utabaki kucheka tu kwa sababu sura yake ni comedy,maisha yake ni comedy na kutembea kwake ni comedy.kwenye warrior baek dong soo alicheza kama ni gangster wa kikundi cha wauaji. Tamthilia nyengine niliyomuona ni hotel king.

View attachment 360076
12) KWON HAE HYO: Mara ya mwanzo nilimuona kwenye the nine,ni mcheshi sana na ni comedian mkubwa nchini korea,tamthilia nyengine nilizomuona ni CAEN AND ABEL,LIE TO ME,WINTER SONATA,BIG MAN, SECRET DOOR.
View attachment 360077

13) LEE MOON SHIK: popote unapomuona basi anatabasamu,jamaa ana kipaji sana katika uigizaji haijalishi ni comedy au serious.alinivutia kwenye ILJIMAE. Tamthilia nyengine ni ROOFTOP PRINCE, AMAN STORY na GIANT
View attachment 360078

14)LEE DEOK HWA:Best actor haijalishi nafasi gani anacheza awe mtu mzuri au mbaya hachoshi kumtazama.mpaka sasa tamthilia nilizoangalia yeye akiwemo ni GIANT,DAEJO YOUNG,AGE OIF WARRIORS,SHINE OR GOING CRAZY,THE MERCHANT,HOTEL KING,QUEEN OF AMBITION
View attachment 360079
15)LIM HYUK: Unamkumbuka yule mzee aliyecheza kama baba yake daejoyoung basi ni huyu jamaa licha ya umri kumtupa mkono jamaa hachoshi,angalia drama kama GIANT,JANG YOUNG SIL,DAEJOYOUNG,KINGS DREAM,IRON EMPRESS.
View attachment 360081
Duuuuuh heshima kwako
Na bila hao duuuh, ni sawa na chai bila sukari.
 
Thanks mkuu Damush' namba moja nilimkubali sana kwenye swallow the sun,no 4 huwa ni msaidizi mzuri mno hasa kwa maboss wake, no 5 yeye nae haachagi kunichekesha hasa kny flames of ambition, no 13 is just the best in every drama.
 
Huyu baba no 8 nampenda sana jamani...Pia namkubali sana Ji sung na wengine wengi. Tuletee wasaidizi wa kike pls
 
Hiyo mashine ya namba 3 ni noma Sanaa, kwenye great queen nilimkubali sana chilsook warang, ila amefunika zaidi ktk jackpot, anachapa hatari, yaani alishindikana mpaka mwisho wa movie, ila hebu nieleweshe ktk chuno alicheza uhusika gani?
 
Back
Top Bottom