Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samahani Sana mkuu sikuwa huku, ningekupa mwongozo. Vp Ulifanikisha?Jamani nisaidien kila nikiingia dramafire inagoma nahc kuumwa jamn nisaidien link au App nzuri
mkuu ni rahisi sana kusamehe chakula kuliko kuacha huu uleviAta mm nafanya mazoezi ya kuachana na hiv vitu. Huu mwaka niko busy sana nikisema nizipe nafasi kwakwel sito ambulia chochote. Mda wowote nitawakimbia
kiukweli najihisi nimechoka sana, naamini ndani ya mwezi huu baadhi ya viporo vyangu nitavimaliza na pia money flower itakuwa inakaribia kumaliza hivyo basi mwezi wa february rasmi inshaallah nitachukua likizo.
Sunbae,kiukweli najihisi nimechoka sana, naamini ndani ya mwezi huu baadhi ya viporo vyangu nitavimaliza na pia money flower itakuwa inakaribia kumaliza hivyo basi mwezi wa february rasmi inshaallah nitachukua likizo.
kiukweli sina sageuk hata moja kwenye hard driveSunbae,
Naomba uchungulie kwenye disk kisha nitajie sageuk ulizonazo.
Mkuu labda nikupe mbinu nayo tumia mm maana mi pia hiki kitu niliwaza toka mwaka jana kwasababu nilijua mwaka huu nitakuwa busy zaidi yake. Mm nimeanza mazoezi madogo madogo ya kujipa breki ama kuacha kabisa kufuatilia hizi Korea Drama japo si rahisi kama navyo andika.ni takribani miaka 5 tokea nianze kuwa mnywaji wa pombe kali ya korean drama na kadri ninavyoendelea kunywa cha kushangaza satisfaction inaongezeka tofauti na jinsi wachumi wanavyotuaminisha kama kadri unapo consume na satisfaction inapungua.
nahisi umefika wakati wa Damushin kupunguza au kuacha kabisa kunywa ulevi huu mkali ili kuendelea kudumisha afya yake, hivyo basi
- kuanzia wiki ijayo akipenda Mungu nitakuwa nakunywa pombe chupa moja tu yenye ujazo kama wa chupa ya kahawa, naamini hii ni njia ya kwanza itakayonifanya nipunguze ulevi.
- nitapunguza kutembelea baadhi ya bar zinazotoa huduma ya ulevi pendwa bila ya malipo yoyote, miongoni mwa bar ninazopenda kuzitembelea ni pamoja na dramanice, kissassian,dramacool, kshow, ikshow na bar nyenginezo.
- nitapunguza kutembelea baadhi ya kuta zinazotoa matangazo na taarifa zinazohusu kuzalishwa kwa ulevi mpya ambao tokea nianze kunywa nimeshindwa kuachana nao,miongoni mwa kuta hizo ni pamoja na soompi, reddit,dramabeans,alkpop,soompi forum n.k
- bila ya kuathiri vifungu vya hapo juu nitalazimika kumalizia kreti zangu takribani 40 ambazo nimezihifadhi kwenye store yangu ndipo niache kabisa kunywa ulevi huu pendwa.
- nitalazimika kuwakimbia walevi wenzangu waliokubuhu kwenye ulevi huu kwani hii ndio njia nyengine itakayonisaidia nisipate taarifa zozote kuhusiana na kuzalishwa kwa ulevi mpya, aigoooo walevi wenzangu naomba munisamehe.
- kubadili mfumo mzima wa kimaisha ndani ya nyumba hii kama vile kutokutembelea kabisa chumba hichi cha hatari na vile vile nisipokee simu yoyote yenye lengo la kunishawishi kutembelea chumba hichi (notifications).
- je ! haya yote yatawezekana? wakati ambapo ulevi unaoitwa money flower,black knight, hwayugi ndio zinazidi kuninogea
- EMPTY dongsaeng, aminas, mjr95 na walevi wengineo kama mumegundua njia nyengine japo ya asili ya kuacha ulevi huu basi tupeane taarifa.
- hiii pombe ya leo imenifanya niwashwe washwe, niwe frustration na kuishia kutamani kukutana na rais wa korea ya kaskazini mwenye namba yake ya simu aiweke humu ndani.
- mwisho nawaambia walevi wenzangu tuendeleze kunywa ulevi huu wa korean drama hadi hapo wapishi wa ulevi wa bongo movies watakapoweza kutengeneza ulevi wao kwa kiwango cha juu.
- yote haya niliyoyaandika asilimia (x) nipo kwelini na asilimia (y) natania, hivyo basi wale wazee wa betting waje watabiri asilimia x ni ngapi na y ni ngapi, mshindi atapata nafasi ya kwenda joseon
Aigooooo hiyo Emperor wang guhn nitaitafuta aisee. Ata kama niko kwenye mpango wa kuzikimbia hizi kazi lakini mm kwenye historical Drama ndio umenishika panapo staili kabisa. Tena mzigo una episodes nyingi hivyo ndio naangalia mpaka nalewa kabisa.![]()
takribani wiki nzima iliopita nilikuwa naangalia drama ya emperor wang guhn (taejo wang guhn) ya mwaka 2000 yenye episode 200 ambayo ni kiporo changu cha muda mrefu sana,kihistoria wang guhn ndiye mfalme wa kwanza wa taifa la goryeo (koryeo) na aliingia madarakani baada ya kumpindua mfalme gongyae ambaye alikuwa ana tabia za kidikteta.
ndani ya wiki moja nilibahatika kuangalia kuanzia episode 90 hadi episode ya 122, kwa sasa nimeamua kuiweka tena kiporo kwa sababu upande wa kwanza wa maisha ya wang guhn nimesha ufahamu kwa sababu hadi episode ya 121 ndio anabeba madaraka. licha ya kuwa ni drama ya zamani lakini haikunichosha kuitazama kwa sababu hadithi yake ni ya kusisimua na cha kufurahisha zaidi nusu na robo ya stori yake ni ukweli mtupu yaani namaanisha matukio mengi yamerikodiwa kwenye vitabu vya kihistoria.
kuhusu kizidownload episode na kuziangalia baadae ilo suala nalifanya ila tatizo linakuja kwenye kuziangalia, kiukweli mzuka wa kuangalia ndio umepungua, napata tabu sana siku hizi.
- money flower ndio drama pekee ambayo episode zake nikizodownload naziangalia muda huo huo,nakumbuka mwezi uliopita niliwahi kuandika natamani siku za wiki zipungue ili jumamosi ifike haraka nipate kuiangalia money flower.
- hwayugi episode ya 3, 4 tayari nimezidownload tokea jumatatu lakini hakuna hata moja niliyoiangalia.
- father is strange drama episode 4 za mwanzo tayari nimezidownload tokea siku ya jumatatu ya mwaka mpya lakini hadi leo sijaiangalia hata moja.
- 2 cops drama hii imechangia kuwa mvivu wa kuangalia drama, baada ya kujilazimisha jana ndio nimefanikiwa kuendelea kuangalia episode ya 11,12,13,14. sitaiangalia tena.
- the producer drama, ni drama ya 2015 ambayo ameigiza kim soo hyun kidogo hii ndio naweza kuiangalia japo kwa nusu saa, nimeishia episode ya 8.
- defendant drama nimeidownload siku aliyotangazwa ji sung kuwa ni mshindi wa grand prize kupitia sbs drama awards, nakumbuka ilikuwa ni mwaka mpya lakini hadi leo sijaiangalia hata nusu episode.
- kill me heal me nayo hivyo hivyo nimeidownload lakini mzuka wa kuiangalia sina
- hadi leo goblin nimeishia episode ya 4 na kwenye pc ninayo mpaka mwisho.
- black knight episode ya 9,10 kwenye pc ninazo lakini sijaziangalia.
- temperature of love nilikuwa naipenda sana hii drama lakini nimeishia episode ya 16 na nahisi tabu kuiendeleza.
- nadhani ni muda muafaka wa kuipumzisha akili labda mzuka unaweza kunirudia tena.
ukiachana na korean drama unapenda jambo gani jengine?Mkuu labda nikupe mbinu nayo tumia mm maana mi pia hiki kitu niliwaza toka mwaka jana kwasababu nilijua mwaka huu nitakuwa busy zaidi yake. Mm nimeanza mazoezi madogo madogo ya kujipa breki ama kuacha kabisa kufuatilia hizi Korea Drama japo si rahisi kama navyo andika.
Njia nayo tumia mm huenda ikawa tofauti kwako maana mm mda mwingi niko busy na kazi napata breki mda wa kula na kuswali. Hiyo ratiba niliyo jiwekee imenifanya napitisha ata siku mbili sijaangalia drama yoyote ile japo ni ngumu kupitisha siku tatu. Jaribu kuwa busy na kile unafanya ama ukiona mda ule ukiwa busy zinakutawala penda kusoma vitabu mda huo hiyo nayo ni plan B yangu.
ni nzuri sana hutajutia kuitazama ndani wamo magwiji wa historical dramaAigooooo hiyo Emperor wang guhn nitaitafuta aisee. Ata kama niko kwenye mpango wa kuzikimbia hizi kazi lakini mm kwenye historical Drama ndio umenishika panapo staili kabisa. Tena mzigo una episodes nyingi hivyo ndio naangalia mpaka nalewa kabisa.
ukiachana na korean drama unapenda jambo gani jengine?
Mkuu utanifaninya ni download saizi. Ngoja nitaanza kuishusha wiki ijayo, nashusha kama episodes 30 alafu natulia nazicheki kwanza kisha ndio nashusha zingine. Ile Dae Jo Young bado naisaka kwa udi na uvumba.ni nzuri sana hutajutia kuitazama ndani wamo magwiji wa historical drama
choi soo jong : anashikilia rekodi ya kuwa mshindi wa kbs daesang award mara tatu kupitia emperor wang guhn, emperor of the sea na king dae jo young
kim young chul : mshindi wa kbs daesang award 2017 na mwaka 2000 kupitia emperor wang guhn
Mkuu ata ww unaweza anzisha sio mpaka mtu akuanzishie. We anzisha alafu ss tutakuwa wachangiaji ama wanao fuatilia hizo Chinese drama wakiona uzi huo hawato pita mbali. Pia ungetuwekea ni drama ipi nzuri upande huo ili tuitafute tuangalie na huko kukoje.ukianzishwa uzi wa Chinese dramas tushtuane, maana ndio nazielewa wakaroea wakasome
Category:South Korean historical television series - WikipediaNee! Nilikuwa nahitaji list ya sageuk nzuri .