President Moon Jae In Congratulates BTS And ARMY For Achieving No. 1 On Billboard 200
BTS wameendelea kuushangaza ulimwengu baada ya album yao inayoitwa Love Yourself: Tear kushika nafasi ya kwanza kwenye chart za billboard 200 jambo ambalo limemfanya rais wa korea kusini kuwapongeza vijana hao pamoja na mashabiki wa group hilo kwa mafanikio yao na kwa kuzidi kuitangaza korean kpop.
ni kwa mara ya kwanza album ambayo si ya kiingereza kushika nafasi ya kwanza baada ya miaka 12 na pia ni mara ya kwanza kwa album ya muziki wa korea kushika nafasi ya kwanza.
rais moon jae in ameandika maneno yafuatayo kwenye barua yake kwa ufupi;
"natoa shukrani zangu za dhati kwa vijana hawa saba wanaopenda muziki wanaoitwa BTS army, vijana wengi duniani wanajisikia furaha kutokana na muziki wa BTS pamoja na dance performance wanayoionyesha.
kiukweli BTS ni vijana wa ajabu sana kutokana na jinsi wanavyoweza kuigeuza huzuni na kuwa furaha kwa njia tofauti.
ni jambo lililowazi ya kwamba muziki wetu umezidi kusonga mbele na kutambulika zaidi duniani na hii yote imechangziwa na BTS.
Nitawaunga mkono vijana hawa ili washike nafasi ya kwanza kwenye billboard chart 100 na wapate kushinda tunzo ya grammy, kufanya show kwenye viwanja vikubwa duniani na pia kuwa wanamuziki wenye mafanikio duniani.
nitayakumbuka majina ya vijana hawa saba Jin, Suga, J-Hope, RM, Jimin, V, na Jungkook kwenye maisha yangu na naamini huu ni mwanzo tu wa mafanikio.
ahsanteni sana kwa kushare nasi furaha kwa taifa letu na watu wote duniani kwa ujumla.
May 28, 2018.
“President Moon Jae In.”
kweli nimemini hakuna lugha nyepesi duniani kama lugha ya muziki
hata kama mutaimba kwa lugha ya chato na kipemba kama muziki wenu ni mzuri basi ipo siku utapendwa na kupata mafanikio.
EXO, bigbang na wengineo wakae pembeni kwanza wawaache majeshi ya BTS wakinukishe.
ni mimi
Damushin mkorea mweusi aliyezaliwa nchi inayopitisha bajeti ya kilimo kwa 5%.
kweli nimeamini mkono wa mtu mpumbavu ndio huazimwa kwa ajili ya kupimia urefu wa shimo la nyoka aina ya koboko (black mamba).
fake love