Park min young
nilikuwa nikijawa na furaha kila sekunde nilipokuwa nikiigiza uhusika wa kim mi so, nilishikw ana woga baadhi ya wakati lkini furaha niliokuwa nayo sitaweza kuisahau kwenye maisha yangu.
pia nilikuwa nikijiuliza maswali
je kuna nyakati ambazo niliwahi kujisikia nikiwa na furaha kama hivi sasa?
sifahamu kama watizamaji wametambua ya kwamba drama hii imenifanya niwe na furaha wakati huu, baadhi ya watu wameniambia kiukweli nimefanana na kim miso.
kitu muhimu zaidi kwangu mimi ni kinachokuja mbele yangu na si kilichopita hivyo basi nawaahidi mashabiki nitazidi kujituma kwenye kazi zangu na kuwahakikishia nitarudi na project nzuri.
natumai mutamuaga kim miso kwa tabasamu lililojaa nafsini mwenu.
Pyo Ye Jin
namshukuru sana director Park Joon Hwa, writer, actors na staff wote waliokuwa pamoja na mimi kwa muda wote. nilijawa na furaha kwa muda wote na kwa kweli siamini kama ndio tumeimaliza project hii. Nahisi kama miezi miwili imekimbia kwa spidi kubwa sana zaidi ya muangaza. Mwisho niwashukuru mashabiki kwa ushirikiano mkubw amuliouonyesha kwa muda wote.,
nawapenda sana.
2PM Chansung
nilijitahidi kadri ya uwezo wangu nisiwavunje moyo mashabiki wangu, film set ilikuwa ni furaha muda wote wa kazi.
aigoooo sijui hizi episode mbili za mwisho alibadilisha suti?
hwang bora
mchumba wangu wa 40 ambaye ndiye nyota wa tatu wa drama hii kiupande wangu.
amesema
"niwashukuru wale wote waliovutiwa na uhusika wa Sera na Yang bok couple,pia niwashukuru staff wote waliofanikisha drama hii.nitaendelea kuwa muigizaji ambaye kila ninapopata nafasi nitaonyesha kitu kipya.
kwa sasa ninajiandaa kushiriki kwenye drama ya
VAGABOND ambayo waigizaji wakuu watakuwa ni Lee seung gi na Bae Suzy.
kila la kheri mchumba endelea kufanya kazi kwa bidii tupate hela ya kula na pesa ya kodi, mimi mwenzio nitendelea kuwa mume na baba mtarajiwa wa nyumbani.
Kang Ki Young
niwe mkweli huyu kijana namuheshimu sana kwa sababu kwenye kazi zake hajawahi kuniangusha licha ya kwamba sijawahi kumuona akiigiza uhusika mkuu.
amesema
"napenda niwashukuru watazamaji wote waliovutiwa na drama hii, pia niwashukuru team nzima ya whats wrong with secretary kim kwa kipindi chote tulichokuwa pamoja tulifanya kazi kama familia.napenda kumshukuru director kwa kunipa nafasi ya kushiriki kwenye hii drama, hivyo basi nawaahidi mashabiki nitaendelea kujitahidi kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kushiriki kwenye project nyenginezo pindi nitakapopewa nafasi.
Kang Ki Young atashiriki kwenye drama ya
Boyfriend ambayo waigizaji wakuu ni park bo gum na song hye kyo.
vile vile atashiriki kwenye drama ya
terius behind me ambayo muigizaji mkuu ni SO JI SUB.
ngoja niendelee kuziweka kiporo episode mbili za mwisho mpaka nitakapopata majibu ya ubuyu wangu wa leo. sitaki kushuhudia tukio la uongo la ndoa.
whats wrong with secretary kim ndio best romantic comedy kwa mwaka huu kwa maoni
yangu.