Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

20180704_103800_4127.jpg
pale mafundi wawili wanapounganishwa na muandishi mahiri anayeitwa lee soo yeon
hivi ni mimi peke yangu ndiye ninayeiangalia hii medical drama inayoitwa Life.
unaikumbuka drama inayoitwa secret forest (stranger) ambayo tulishuhudia vita kubwa sana ya kupambana na mfumo wa rushwa kwenye sekta kuu ya sheria nchini korea.

humu ndani kwenye drama ya life utashuhudia vita kubwa sana kati ya madaktari na rais wa song koo hospital university juu ya suala zima la uendeshaji wa hospital.ambapo rais anataka kuiendesha hospitali kama kampuni yenye kutengeneza faida kubwa.
unadhani kinatokezea kitu gani pale jopo la madaktari bingwa wenye akili wanapochezewa akili zao na rais mwenye akili nyingi kama mimi.
narejea tena hii ni best drama na kwa anayehitaji kuiangalia hatojutia.
doctor lee dong wook vs president choi seung woo

muandishi wa drama hii ya life ndiye aliyeandika drama ya secret forest ambayo lead actor alikuwa ni choi seung woo.
 
dah mzuka wako wa simba day umekufanya utuwekee poster lenye maandishi ya kijapani.
au ndio team madeepa?
mungu azidi kumponyesha ugonjwa wa nasopharyngeal cancer na pia awape afya wagonjwa wote wanaohangaika kurudisha afya zao.
Kim-Woo-Bin.jpg
Mwezangu Hmmm!! Mahaba Yanatuzidi Na Iyo Poster Ni Wakati Hiyo Drama Inaonyeshwa Japan Nahisi.

Karibu Na Zakupotea Pia?
 
hahahahahaaaaa uyo bwege madeepa ( madeera) vurugu lake lote akifika kwa beautiful lady Ae shin anatulia kama bata anapoongozana na mama yake..
ananikumbusha yeom jang kwenye emperor of the sea dhidi ya mwanadada jung hwa.
mhhhhhhhh mapenzi ni zaidi ya ugonjwa wa cancer ndio maana naogopa kuyakaribia.
fighting my brother ambaye hatuna uhusiano wowote mr yoo yeon seok
yoo-yeon-seok.jpg
Nguvu Ya BinAdamu Wa Jinsia Ya Kike, Hiyo Ndo Nguvu Yao Kwenu Hata Uweje Ukifika Kwa Mtoto Wakike Unakuwa Kama Mkate Tuuh.

Mi Alinikera Pale Alipomvuta Yule Binti Mdogo, Then Akakubari Kupigwa Kibao Na Binti Mkubwa. Huyu Jina La Bwee Linamfaa
 
ilikuwa ni 17/10./2017.ndipo uliniomba nikuweke link ya historical movie inayoitwa the fortress.
bahati nzuri leo nimetembelea tovuti ya dramanice ndio nimeona wameshaiweka subtitle ya kiingereza.
THE-FORTRESS_Main-Poster-e1521502729925.jpg

kwa ufupi
mnamo mwaka 1636, Qing dynasty ambayo ndio china ya kipindi hiki kama sijakosea waliivamia nchi ya joseon ambayo kwa sasa ni korea japokuwa imegawanyika nchi mbili. mfalme Injo na watumishi wake waliikimbia ikulu na kwenda kujificha kwenye ngome iliopatikana maeneo ya milimani inayoitwa Namhansanseong.

mtumishi mmoja aliyekuwa anaitwa Choi Myung-Kil aliamini njia pekee ya kurudisha hali kama ilivyokuwa mwanzoni ni kuingia makubaliano na QING, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba joseon pia wakubali matakwa ya utawala wa Qing.
Pia kulikuwa na mtumishi mwengine aliyeitwa Kim Sang-Hun ambaye aliamini njia pekee ya kurudisha heshima ya serikali ya joseon ni kuendelea kupambana hadi mwisho wa nguvu zao.
je mfalme atachukua maamuzi ya nani?
starring
lee byung hun = choi myung kil
kim yun seok = kim sang hun
park hae il = mfalme Injo​
Awards
  1. 2018 (54th) BaekSang Arts Awards - May 3, 2018 ,"Best Film"
  2. 2017 (38th) Blue Dragon Film Awards - November 25, 2017 ,"Best Screenplay" (Hwang Dong-Hyuk)
nakuomba radhi kutoka ndani ya kiwililiwili changu kilicho hai muda huu, hivyo basi usije ukadhani nilikupotezea kwa kipindi cha miezi 10.
aigoooo lakini mimi sijaiangalia mpaka muda huu.

nashukuru ntafanya kuipitia wala hakuna mbaya iliyofanya.asante
 
Nguvu Ya BinAdamu Wa Jinsia Ya Kike, Hiyo Ndo Nguvu Yao Kwenu Hata Uweje Ukifika Kwa Mtoto Wakike Unakuwa Kama Mkate Tuuh.

Mi Alinikera Pale Alipomvuta Yule Binti Mdogo, Then Akakubari Kupigwa Kibao Na Binti Mkubwa. Huyu Jina La Bwee Linamfaa
upande mmoja wa sarafu unaweza kumchukulia Dong mae kama ni mwanadamu asiye na chembe ya huruma anapokuwa kwenye mawindo yake ila mwisho wa siku utagundua ya kwamba kumbe hata yeye ameumbwa na hisia tofauti na robot Namshin na ndio maana anapokutana na mwanadamu anayemfanya hisia zake za kikatili zitulie anakuwa mnyonge sana.

mfano wa pili muangalie anapokutana na manadada Hina ambaye ni mmiliki wa hotel anakuwa mkimya sana, hii inaonyesha kwa kiasi kikubwa sana ameathirika na maisha aliyoyapitia udogoni kwake.
dongmae hakuzaliwa kuwa shetani ila maisha mabovu aliyoyapitia pamoja na wazazi wake yamemfanya ajione kuwa ni shetani aliyetakasika ambaye ana uhuru wa kutoa adhabu yoyote na kwa mtu yoyote na kwa muda wowote.

aigooooo maandishi ulioanza nayo sijayapatia majibu.
 
Hahahahah Pole.
 
ATa mi nampenda,sijui kwa nn li bang ji wasifu wake humu sijaupenda
anakusalimia jang hyuk sunbaenim
nafikiri miongoni mwa watu wanaochukia kuzaliwa kwenye noble family ni kim hee sung.
inaonekana amechukizwa sana na maisha wanayoishi familia yake hususani kuanzia babu yake ambaye alikuwa ni mkatili sana kwa watumishi wake.
ukiachana na hisia za kimapenzi anaonekana kama ni mtu ambaye hapendi kuweka wazi ndoto zake na hatimaye kujifanya kama ni mwanadamu asiye na malengo yoyote.
"I’m afraid of the blood running through my veins. If given the power it might be wielded inappropriately
kama ni wewe unafikiri ungeliishi maisha gani?
ikiwa dhambi ya babu yako ya kuwatesa watumwa unabebeshwa wewe na choi eugene.
ikiwa dhambi ya noble family kuishi kama wapo peponi unabebebeshwa wewe na dongmae.
acha tu aendelee kuishi hotelini ili ajiweke mbali na uchafu wa noble family.
tumblr_nigvpeCqP51rcoad1o1_1280.jpg
je ni kweli hajali yanayoendelea ndani ya nchi yake?
hata teja aliyeathirika na madawa ya kulevya anajali yale yote yanayoendelea ndani ya nchi yake na ndio maana hata ukimuuliza mlevi rais wa tanzania ni nani?
atakujibu ni magufuli.

sijui huko mbele kitatokezea kitu gani ila ninamuona kim hee sung naye akivutwa na sumaku ya mwanadada Ae sin.
  • pindi japan watakapoivamia joseon huenda akawa ni pro japan pamoja na familia yake, kivyovyote kwa akili za baba yake na mama yake zilivyo hawawezi kuiunga mkono joseon pindi wajapani watakapoikalia kimabavu.
  • au huenda akawa mfanya biashara ambaye atakuwa anawaunga mkono anti japan.nyuma ya pazia. kwa kuwa amesoma japani basi wajapani watamuona ni mtumwa wao kumbe ni kinyume chake.
kwa jinsi hii drama inavyoendelea nahisi muigizaji mkuu ni mwanadada Ae shin.
eugene + dongmae + kim hee sung = lady go aesin

ila wanawake muna tabia moja ya ajabu sana, munakumbuka episode ya 3 walipokuwa kwenye boti eugene na ae sin walipokuwa wanatoka kwa mzee anayetengeneza vyombo.
ae sin akampa siri choi eugene ya kwamba yeye ndiye aliyemshambulia kiongozi wa marekani kwenye hoteli.
하하하 하하하하하 하하하하하 하하
mapenzi yenu yanavuka kiwango cha phd mpaka munatoa siri za ndani.
,mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

Kufatilia ongoing mateso sana. Halafu sijui kwann sijaipenda hii movie kama nilivyozipenda wok of love na whats wrong with secretary kim
  1. mapenzi ya kweli hayaangalii hali ya mtu aliyokuwa nayo na hili nimezidi kujifunza kupitia drama hii
  2. mama ndiye kiumbe pekee ambaye yupo tayari adhurike yeye lakini mtoto wake awe na amani, nachukizwa sana na wale wasio waheshimu wazazi wao.
  3. mwandamu unaposaidia unapaswa uwe na shukurani hata kama aliyekupa msaada hana heshima kubwa sana kwenye jamii zaidi yako.
  4. kwenye maisha yetu tamaa zinaepukika, ji young hoon amenipa funzo kubwa sana kupitia drama hii. Alikuwa na uwezo wa kuendelea kurithi nafasi ya mwenyekiti wa makampuni ya PK lakini aliona hii si sehemu yake anayostahili kuwepo. wanadamu tunapswa tuwe na tabia ya kuridhika.
  5. wanawake wanapaswa kuheshimiwa kwenye jamii, jaribu kumuangalia mwanadada so bong alijitolea kwa uwezo wake wote kumlinda nam shin robot huku akijua fika hatapata ujira wowote kwa kazi anayoifanya.
  6. nitakereka sana kwenye KBS awards za mara hii kama seo kang joon atashindwa kupata tunzo ya top exellence actor.
 
Namjibia mengine atajibu mwenyewe. Ni mtanzania anayezipenda kama wewe,ndo maana anaandika lugha fasaha ya kiswahili ila yeye anazipenda sana movie za kakikorea kuliko kihindi,telenovela etc.
Sorry mkuu wewe ni mkorea?
 
  • hapana nimezaliwa Tanzania.
  • wazazi wangu wote ni watanzania kutoka Zanzibar japokuwa kihistoria wametokea sehemu tofauti za East African
  • sijawahi kufika nchini korea na pia sijui kuzungumza lugha ya korea.
  • wala sijawahi kulala nikaota nimepanda mnara wa Namsan Tower.
  • pia sijawahi kulala nikaota ninakula jjajangmyeon na chupa ya soju.
  • uhuru wa kufanya ninachokitaka nikiwa Tanzania pasina kuvunja sheria ndiko kulikonipelekea kuwa ni mfuatiliaji wa korean entertainment.(korean hallyu). wale watu weupe wanaita demokrasia.
  • je majibu yangu yangu yamejitosheleza?
Yanajitosheleza ila naona unafahamu mengi kuhusu Korea. Labda uongezee tena nyama kidogo...
 
  1. dah! nimeshangaa sana kuona kumbe mfalme ndiye kiongozi mkuu wa kikundi cha righteous army.
  2. naona kim hee sung naye ameshaanza kunasa kwenye sumaku ya mwanadada go aesin, hapo anamwambia kama umeamua maisha yako kuwa mpigania haki wa joseon basi nipo tayari kuwa kivuli chako.
  3. kuna nukuu moja ameizungumza kim hee sung imenichekesha sana kwenye icho kipande hahahahahahahaaaaa
amemwambia dongmae unashangaa mimi kulipia tiketi zote za treni?
inawezekana mfalme wa joseon ndiye mmiliki wa milima na wanachi wote lakini familia yangu ndiyo wamiliki wakuu wa ardhi ya joseon
 
Na Dong Mae Akamjibu kuwa, Uo Ukubwa Wa Iyo Ardhi Ndipo Atakapoenda Kumzika Sababu Hatapata Shida ya Kutafuta Pakuzikia.
 
Back
Top Bottom