Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;
- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net


======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread) ..

Kazi kwako.. Enjoy!
Sasa zile link za english series mmeweka wapi??
 
jang hyuk
upcoming drama BAD PAPA
Bad Papa' is the story of a middle-aged man who keeps fighting to protect his family in a harsh world
View attachment 832471
38680978_1111044519071209_7943885340752740352_n.jpg
NImekaa mkao wa kuitazama
 
anakusalimia jang hyuk sunbaenim
nafikiri mi. goni mwa watu wanaochukia kuza Dwa kwenye noble family ni kim hename sung.
inaonekana amechukizwa sana na maisha wanayoishi familia yake hususani kuanzia babu yake ambaye alikuwa ni mkatili sana kwa watumishi wake.
ukiachana na hisia za kimapenzi anaonekana kama ni mtu ambaye hapendi kuweka wazi ndoto zake na hatimaye kujifanya kama ni mwanadamu asiye na malengo yoyote.
"I’m afraid of the blood running through my veins. If given the power it might be wielded inappropriately
kama ni wewe unafikiri ungeliishi maisha gani?
ikiwa dhambi ya babu yako ya kuwatesa watumwa unabebeshwa wewe na choi eugene.
ikiwa dhambi ya noble family kuishi kama wapo peponi unabebebeshwa wewe na dongmae.
acha tu aendelee kuishi hotelini ili ajiweke mbali na uchafu wa noble family.
tumblr_nigvpeCqP51rcoad1o1_1280.jpg
je ni kweli hajali yanayoendelea ndani ya nchi yake?
hata teja aliyeathirika na madawa ya kulevya anajali yale yote yanayoendelea ndani ya nchi yake na ndio maana hata ukimuuliza mlevi rais wa tanzania ni nani?
atakujibu ni magufuli.

sijui huko mbele kitatokezea kitu gani ila ninamuona kim hee sung naye akivutwa na sumaku ya mwanadada Ae sin.
  • pindi japan watakapoivamia joseon huenda akawa ni pro japan pamoja na familia yake, kivyovyote kwa akili za baba yake na mama yake zilivyo hawawezi kuiunga mkono joseon pindi wajapani watakapoikalia kimabavu.
  • au huenda akawa mfanya biashara ambaye atakuwa anawaunga mkono anti japan.nyuma ya pazia. kwa kuwa amesoma japani basi wajapani watamuona ni mtumwa wao kumbe ni kinyume chake.
kwa jinsi hii drama inavyoendelea nahisi muigizaji mkuu ni mwanadada Ae shin.
eugene + dongmae + kim hee sung = lady go aesin

ila wanawake muna tabia moja ya ajabu sana, munakumbuka episode ya 3 walipokuwa kwenye boti eugene na ae sin walipokuwa wanatoka kwa mzee anayetengeneza vyombo.
ae sin akampa siri choi eugene ya kwamba yeye ndiye aliyemshambulia kiongozi wa marekani kwenye hoteli.
하하하 하하하하하 하하하하하 하하
mapenzi yenu yanavuka kiwango cha phd mpaka munatoa siri za ndani.
,mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

Sa Aigooooo salam zimenifikia. Chaaah na iwe hivyo unavyomtabiria ikiwa virse vesa nitamchukia,hhope atafata nyayo za lady ae sin ahahaaa hapana chezea kulove na atawasnitch wamarekani navyohis
 
Inawezekana Mr. Sunshine Inaelezea Hii Ya Kutawaliwa Na Wajapan Kisha Urusi Na Marekani Wakaja Kuwakomboa, Maana Naona Ndo stori Inayozungumzia Sana Mule.
anyeong haseyo noona
bingo, upo sahihi upande mmoja wa shilingi, labda tuanzie hapa kwa upade wa Marekani kwa uelewa wangu natumai kama kuna mwengine muelewa zaidi yangu atanisahihisha kwa haraka zaidi bila ya kutumia lugha kali
  1. kama unakumbuka vizuri matukio ya episode 1 utaona hadithi yake imeanza mwaka 1871 ndipo kwa mara ya kwanza Marekani ilipoamua kuivamia kijeshi korea (Joseon) kwa dhumuni la kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi mbili hizo, tukio hilo wakorea wanalitambua kwa jina la Shinmiyangyo (western disturbance), sababu kubwa kama nilivyoeleza ni kuwa marekani walihitaji wawe na ushawishi nchini korea na eneo kubwa la Asia kiulinzi na kibiashara kama ilivyo hivi sasa.
  2. ni tukio ambalo lilitokezea kwa kiasi kikubwa kwenye kisiwa cha gang hwa ambapo jeshi la majini liliweka kambi eneo hilo kwa dhumuni la kutoa mashirikiano kwa msafara wa marekani kwa ajili ya kuanzisha diplomatic relation na emperor wa joseon ambaye alikuwa ni Gojong ambaye ulikuwa ni mwaka wake wa nane. Korea walishambulia meli mbili za marekani mnamo June 1 ndipo na wao wakaitumia nafasi hiyo kuivamia joseon baada ya kushindwa kuombwa radhi na serikali ya joseon, inakadiriwa takribani wanajeshi 650 wa marekani walivamia kambi tofauti na kuwaua wakorea takribani 200 mnamo June 10.
  3. licha ya marekani kuonyesha nguvu yake ya kijeshi dhidi ya joseon lakini serikali ya joseon iliendelea kukataa kufikia makubaliano ya kidiplomasia na Marekani hadi mwaka 1882. wakati huo licha ya kuwa mfalme alikuwa ni gojong lakini mamlaka ya serikali yalikuwa chini ya daewagun kwa sababu Gojong bado alikuwa ni mdogo sana.
  4. April–May 1882 ndipo marekani wakiongozwa na mwakilishi wao ambaye ni Robert W Shufeldt waliingia makubaliano na joseon ya kuanzisha urafiki kati ya nchi mbili hizo likiwemo suala kubwa la Marekani kuilinda Joseon dhidi ya vitisho vyoyote vya nchi jirani ikiwemo japani ambao walikuwa tishio kubwa sana.
  5. kwenye tukio hilo tukirudi kwenye drama ya MR SUNSHINE utagundua vita hiyo ndio ilisababisha kifo cha baba yake Jang Seung-Goo ambaye ndiye mwalimu wa lady go aesin kwenye kutumia bunduki na pia ni miongoni mwa wapiganaji wakuu wa righteous army. Hapo ndipo kwa upande wa Marekani ndipo walipoanza kuikalia Joseon. Na wakati huo ndipo choi eugene ndipo alipopata nafasi ya kukimbilia Marekani na baadae kujiunga na jeshi la majini.
  6. kwa mujibu wa hii drama choi eugene alirudi tena korea mwaka 1902, inamaana alirudi korea miaka 31 baadae, hivyo basi kama aliondoka korea akiwa na miaka 9 kwa hesabu zangu za vijiti alirudi korea akiwa na miaka 40.

sunshine-01-00019.jpg

daewagun
sunshine-01-00020.jpg

young emperor gojong

sunshine-01-00099.jpg

sunshine-02-00128.jpg
 
Inawezekana Mr. Sunshine Inaelezea Hii Ya Kutawaliwa Na Wajapan Kisha Urusi Na Marekani Wakaja Kuwakomboa, Maana Naona Ndo stori Inayozungumzia Sana Mule.
mkataba kati ya Japan na korea 1876
balaa lilianzia hapa

  1. miaka minne baadae (1875) japani nao wakavamia kisiwa cha Ganghwa kwa dhumuni lile lile walilokuwa nalo wamarekani ila japani wao kama kawaida yao waliitaka joseon kwa dhumuni la kuweza kupata njia ya urahisi zaidi kuikalia china na pia waweze kujenga miundo mbinu itakayowawezesha kusafirisha dhana zao za kivita ili kuivamia URUSI hapo baadae na wakati huo aliyekuwa malikia ambaye ni empress myeongseong alishaweka mahusiano mazuri sana na urusi kabla hajauawa kinyama na wajapani hapo baadae.
  2. tukumbuke kuwa kabla ya marekani, japani kuivamia korea kupitia kisiwa cha Gang hwa mnamo mwaka 1866 nchi ya ufaransa nayo pia iliivamia joseon kupitia kisiwa cha gang hwa.
  3. kupitia tukio hilo la uvamizi wa vikosi vya japani inakadiriwa wanajeshi 35 wajoseon walipata athari na wanajeshi 3 wa japani nao walipata athari, ndipo serikali mpya ya japani ikaitaka korea iombe radhi kutokana na tukio hilo na ndio ukawa mwanzo wa nchi mbili hizo kuingia makubalino ya kidiplomasia mnamo February 27, 1876 (ganghwa treaty)
  4. ila mkataba wa pande mbili hizi uligeuka kuwa ni kituko kwa upande wa korea kwa sababu ulionekana mkataba huo kuwafaidisha zaidi wajapani kwenye sekta ya uwekezaji nchini korea kuliko wakorea wenyewe, mkataba huo ulichangia kwa kiasi kikubwa japani kuitawala korea hapo baadae.
baadhi ya vifungu walivyokubaliana kupitia mkataba huo kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ya kiswahili

  • korea ni nchi huru na yenye mamlaka kama ilivyo nchi ya japan
  • japan na korea wanapaswa kubadilishana wajumbe ndani ya miezi 15 kwa dhumuni la kukuza diplomasia kati ya pande hizo mbili.
  • japani watalazimika kutumia lugha ya kijapani na kichina kwa ajili ya mazungumzo ya pande mbili hizo na upande wa korea watalazimika kutumia lugha ya kichina tu.
  • japani watakuwa na haki ya kutumia bandari zilizopo korea ambazo zimeidhinishwa kupitia mkataba huo.
  • meli za japani zina haki ya kufanya uchunguzi wowote kwenye mwambao wa bahari ya korea.
  • wafanyabiashara wa japani wana haki ya kufanya shughuli zao nchini korea ikiwemo kununua ardhi
  • kuwepo kwa uhuru wa kufanya biashara kwa pande mbili hizo bila ya kubughudhiwa na upande wowote wa serikali
  • Extraterritorial rights kwa upande wa wananchi wa japani wakiwa korea.
Extraterritorial rights ni haki wanazokuwa nazo wageni wakiwa nje ya nchi yao, inamaana kama wajapani walikuwa wanafanya makosa ndani ya joseon serikali ya korea haikuwa na mamlaka ya kuwaadhibu kutokana na sheria za korea.
ndivyo nilivyoelewa kwa upande wangu, wajuzi zaidi watanisahihisha.
1200px-Japan_Korea_Treaty_of_Amity_26_February_1876.jpg

jaribu kurejea Treaty of Nanjing, (August 29, 1842) moja kati ya nakubaliano ya ovyo kuwahi kufanyika kati ya nchi ya china dhidi ya mabepari wa bara la ulaya.
kutoka mwaka 1910 hadi 1945 ndipo korea ilitawaliwa rasmi na japani
 
MR SUNSHINE DRAMA
  1. mzee go sa hong ambaye ni babu yake lady ae sin kiupande wake nimeanza kuona dalili za kutembelewa na malaika wa kifo asiye na chembe ya huruma kwenye shughuli zake za utekelezaji wa majukumu. Je atakufa kifo cha kawaida au ataishia kwenye mikono ya muheshimiwa lee wan ik?
  2. kupitia episode ya 13 tumeona barua zake za siri alizokuwa akiwapelekea wanafamilia wenzake wanaounda timu ya noble family kugundulikana na lee wan ik. sidhani kama lee wan ik atamuacha akiwa hai kwa sababu kama hatamshughulikia ataleta athari kwenye mipango yake ya kuikabidhi Korea kwa mfalme wa Japani. Ila ningependa huyu mzee aende kwenye safari yake ya milele kwa haraka zaidi na asipate kushuhudia tukio lenye kuumiza. na litakalomshushia heshima yake kwenye jamii kwa sababu ukoloni unapoingia kwenye nchi ni mbwa pekee ndiye kidooogo anaweza kusalimika.
  3. Na bahati mbaya mzee Go sa hong hahitaji kuwa mbwa koko ambaye atabweka ovyo kwa mmiliki wake ili apewe chakula.Anaipenda korea kuliko mimi ninavyozipenda korean drama na ndio maana amekubali kukataa kulindwa na marekani nyumbani kwake baada ya kuombwa na Eugene choi huku akifahamu fika kwa hali ya serikali ya korea ilivyo kama hawana uwezo wa kujilinda wenye wao je wataweza kulinda nyumbani kwake.Tanzania tunawahitaji wazalendo millioni 48 wenye tabia za mzee go sa hong ndipo tutasonga mbele.
  4. daebak, nimependa majibu ya kim huiseong alipoambiwa na mzee go ha sang amuoe mjukuu wake, aigooooo kwa huu mzuka nilionao na sikukuu hii ningeli mjibu ifuatavyo mzee go ha sang.

"ukweli mzee nampenda sana mjukuu wako na najaribu kila njia awe na furaha pindi anapokuwa nami lakini yeye hana furaha na mimi, ukweli binti yako hanioni kama ni mwanamme mwenye upendo wa dhati kwake, mjukuu wako hanipendi hata kuniona, ukweli ni kwamba ana mchumba mwengine na ndio maana ananikataa, halafu pia ana mapengo"😛😡😉
inamaana kwa bangi zangu za GPA ya 32 balaa lote ningelimsukumizia lady Aesin ya kwamba ndio tatizo kuu la mahusiano yetu.

lakini kim huiseong amejishusha chini mbele ya mzee na kuamua aonekane yeye ndiye tatizo kuu, dah ameonyesha nidhamu ya hali ya juu sana. Unakumbuka alimjibu nini mzee go ha sang?
"naomba unisamehe mzee wangu kwa haya nitakayo yazungumza, kiukweli sivutiwi na mjukuu wako. Anapo tabasamu, mwendo wake wa taratibu, macho yake yenye kung'ara na kuvutia na kila kitu kinachomuhusu yeye nakichukia.

dah nilifikiri mzee go ha sang naye atamjibu ovyo na dharau kim hui seong kumbe nilikuwa najidanganya.
"nayafahamu yote unayoyazungmza (japokuwa umeyazungumza kinyume chake), nafahamu ya kwamba mjukuu wangu ndiye aliyekataa mipango ya ndoa dhidi yako, najua hutumia lugha kali na yenye kuudhi pindi anapokutana na wewe ila nakuomba ukubali ombi langu na ukubali kila jambo linalomuhusu yeye. Kama kuna jambo lolote litanikumba mimi hapo mbeleni basi nakuomba umlinde mjukuu wangu, nina hisia ya kwamba sina muda mrefu wa kuendelea kuishi."
je utafanya hivyo?


nidhamu nidhamu nidhamu
sunshine-13-00147.jpg

eid mubarak
 
0003846147_001_20180818223528436.jpg

This Scene..
dear eugene
miaka mingi imepita mwanangu nikiwa maeneo ya hamgyeong province yenye baridi kali sana.
naomba uwe unaendelea kusafisha nywele zako, utibu majeraha yako,hayo yote ndio niliokuwa nikiyaomba kwa Mungu.

Tafadhali mjaalie nguvu na hekima mtoto huyu mgeni asiyekuwa na ndugu wala jamaa,tafadhali mpe mkate na maji safi kila siku kwenye harakati zake za maisha.
tafadhali mjaalie mtoto huyu asisumbuliwe na hali ya baridi kali.
siwezi kusema ya kwamba hayo yote nina uwezo wa kuyafanya mwenyewe, kwa muhubiri wa dini kama mimi ambaye ni masikini ni ngumu sana kuzimudu gharama za matumizi kwa ajili ya mtoto huyu wa kigeni.

kwa sasa huwezi kuamini ya kwamba ninaweza kuandaa kilevi (takju) na nina mpango wa kukuleta pombe niliyoitengeneza pindi nitakapokuja kukutembelea, kwa sasa nimeamua kuacha kutumia kilevi mpaka hapo nitakapokutembelea hanseong ili tunywe pamoja
mpendwa wangu eugene popote ulipo nitasali na kumuomba mungu kwa ajili yako hata nyakati za usiku ambapo nitakuwa nimelala naamini mungu atakuwa pamoja na wewe
kutoka kwa joseph

dah muda mrefu hawajaonana halafu ndio siku ya kuonana unamkuta mpendwa wako ameshafariki.
38741023_2203522029932847_2718610944274989056_n.jpg

huyu jamaa anaitwa jason na inavyoonekana makaazi yake ni korea, more
projects pleaseeeeeee
Jason ‍♂️제이슨 (actor) (@jasoninkorea87) • Instagram photos and videos
 
Yi Wan-yong
100228_p02_new1.jpg
  1. amezaliwa 17 July 1858 na kufariki 12 February 1926
  2. alikuwa ni pro japanese akiwa kama ni waziri kwenye nchi ya korea ambaye ndiye aliyesaini mkataba ambao ulipelekea korea kutaliwa na Japan mnamo mwaka 1910.
  3. wakati wa uhai wake aliwahi kuishi marekani kwa miaka 3 kuanzia mwaka 1887–1891 na pia alianzisha Inderpendence club mnamo mwaka 1896.
  4. alikuwa ni waziri mnamo mwaka 1905 wakati nchi hizo mbili zilipoingia mkataba unaojulikana kwa jina la eulsa treaty.
  5. mnamo mwaka 1906-1910 alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa korea na alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliochangia kuvuliwa madaraka kwa mfalme Gojong mnamo mwaka 1907.
  6. mnamo mwaka 1910 alifikia makubaliano ya kuwaruhusu wajapani kuitawala nchi ya korea wakati ambapo mfame sunjong alikataa kutia saini hati ya makubaliano ya japani kuitawala nchi ya joseon.
  7. historia inamtaja yi wan yong kama ni kiongozi mkuu wa wasaliti watano waliowahi kutokezea nchini joseon.
  8. baada ya korea kupata uhuru wake mnamo mwaka 1945 kaburi lake lilifukuliwa na mabaki yake kuharibiwa
  • tukirudi kwenye drama ya MR SUNSHINE kuna uwezekano huyu Lee (Yi) Wan Ik uhusika wake ndio wa huyu Yi wan Yong?
  • nikiangalia historia yake huyu msaliti wa joseon na uhusika wa lee wan ik kwenye hii drama naona wanafanana.
  • je ni ipi hatma ya lady Aesin, choi eugene, dong mae, kim hee seong,kudo hina?
  • kwa mujibu wa historia ndio hivyo japan wataitawala korea kwa miaka 35 je kuna uwezekano lady Aesin akamfuata choi eugene nchini marekani?
  • kwa sababu lee Wan Ik mwisho wa siku ndiye atakayeibuka shujaa kwa sababu korea tegemezi lao kuu ni Urusi ambao ndio wanawategemea kwa kiasi kikubwa wawape ulinzi na vurugu lote tunaloliona la kutafuta document yenye signature ya mfalme ni kwamba japani wanahitaji ile fedha ili iwasaidie kwenye mikakati ya kupambana na urusi kwa Urusi anashindwa kwenye vita na japan na kupelekea matumaini ya korea kuzidi kufifia.
sunshine-12-00009.jpg
 
Song Hye Kyo And Park Bo Gum’s New Drama Confirms Details Of 1st Script Reading
kwa mujibu wa taarifa kupitia vyanzo tofauti vya habari inasemekana kwa mara ya kwanza wawili hao watakutana siku ya leo kwa ajili ya script reading ila cha ajabu sehemu watakayokutana imebaki kuwa ni siri mpaka muda huu.
0347b3ec2edc4ebbaedc933ad97e7178.jpeg


STzIplQ.jpg

drama inaitwa boyfriend (namja chingu =남자 친구)
 
Wakuu habari ya humu. Nataka vyuma vingine vyenye maudhui kama ya Heartless city.

Cc aminas Damushin na wadau wote
mhhhhhhh niwe mkweli sijabahatika kuiangalia heartless city.
ila kama unahitaji drama zenye kuzungumzia ishu za criminal, action,thriller, investigation basi jaribu zifuatazo.
  1. life on mars
  2. voice season 1
  3. voice season 2
  4. black
  5. tunnel
  6. secret forest
  7. criminal mind
  8. signal
  9. partners for justice
  10. bad guys 1
  11. bad guys 2
  12. phantom
  13. duel
  14. incarnation of money
  15. pied piper
  16. sign
  17. mad dog
  18. innocent defendant
  19. Healer
  20. Come and Hug Me
 
mhhhhhhh niwe mkweli sijabahatika kuiangalia heartless city.
ila kama unahitaji drama zenye kuzungumzia ishu za criminal, action,thriller, investigation basi jaribu zifuatazo.
  1. life on mars
  2. voice season 1
  3. voice season 2
  4. black
  5. tunnel
  6. secret forest
  7. criminal mind
  8. signal
  9. partners for justice
  10. bad guys 1
  11. bad guys 2
  12. phantom
  13. duel
  14. incarnation of money
  15. pied piper
  16. sign
  17. mad dog
  18. innocent defendant
  19. Healer
  20. Come and Hug Me
poseidon
two weeks
iris 1 n 2
gap dong
athena
switch
......
 
Lee Se Young in Talks to Star in Korean Drama “Gwanghae: The Man Who Became King”
kama atakubali offer hiyo ataigiza nafasi ya malikia ambaye anajikuta akiwavutia wanaume wawili.
Gwanghae: The Man Who Became King ni remake ya movies yenye jina kama hilo ambapo inazungumzia hadithi ya mfalme gwanghae ambaye alikuwa akiishi maisha ya ujanja ujanja (mjinga mjinga) ili atimize malengo yake.
tvN ndio watakayoionyesha drama hiyo mwaka 2019 na msimamizi mkuu wa drama hiyo ni producer aliyeisimamia drama ya money flower.
yeon ji goo ndiye aliyepewa nafasi ya kuigiza nafasi ya mfalme na pia nafasi ya mburudishaji (clown)
photo996216.jpg

huyu dada kwenye drama ya hwayugi alikuwa anatumia jina la buja.(zombie)
dah nimewamisi sana
mwenyekiti ng'ombe
mwana wa mfalme kima
secretary mbwa
mwana wa mfalme pweza
sam jang.

kwenye hii movie ambayo pia inaitwa masquerade starring alikuwa ni lee byung hun (mr sunshine drama) na han hyo joo (w drama)
Gwanghae20.jpg

kwa anayetaka kuiangalia
Masquerade 2012 at Dramanice
 
Lee Se Young in Talks to Star in Korean Drama “Gwanghae: The Man Who Became King”
kama atakubali offer hiyo ataigiza nafasi ya malikia ambaye anajikuta akiwavutia wanaume wawili.
Gwanghae: The Man Who Became King ni remake ya movies yenye jina kama hilo ambapo inazungumzia hadithi ya mfalme gwanghae ambaye alikuwa akiishi maisha ya ujanja ujanja (mjinga mjinga) ili atimize malengo yake.
tvN ndio watakayoionyesha drama hiyo mwaka 2019 na msimamizi mkuu wa drama hiyo ni producer aliyeisimamia drama ya money flower.
yeon ji goo ndiye aliyepewa nafasi ya kuigiza nafasi ya mfalme na pia nafasi ya mburudishaji (clown)
photo996216.jpg

huyu dada kwenye drama ya hwayugi alikuwa anatumia jina la buja.(zombie)
dah nimewamisi sana
mwenyekiti ng'ombe
mwana wa mfalme kima
secretary mbwa
mwana wa mfalme pweza
sam jang.

kwenye hii movie ambayo pia inaitwa masquerade starring alikuwa ni lee byung hun (mr sunshine drama) na han hyo joo (w drama)
Gwanghae20.jpg

kwa anayetaka kuiangalia
Masquerade 2012 at Dramanice
Bogoshiposeyo
 
Lee Se Young in Talks to Star in Korean Drama “Gwanghae: The Man Who Became King”
kama atakubali offer hiyo ataigiza nafasi ya malikia ambaye anajikuta akiwavutia wanaume wawili.
Gwanghae: The Man Who Became King ni remake ya movies yenye jina kama hilo ambapo inazungumzia hadithi ya mfalme gwanghae ambaye alikuwa akiishi maisha ya ujanja ujanja (mjinga mjinga) ili atimize malengo yake.
tvN ndio watakayoionyesha drama hiyo mwaka 2019 na msimamizi mkuu wa drama hiyo ni producer aliyeisimamia drama ya money flower.
yeon ji goo ndiye aliyepewa nafasi ya kuigiza nafasi ya mfalme na pia nafasi ya mburudishaji (clown)
photo996216.jpg

huyu dada kwenye drama ya hwayugi alikuwa anatumia jina la buja.(zombie)
dah nimewamisi sana
mwenyekiti ng'ombe
mwana wa mfalme kima
secretary mbwa
mwana wa mfalme pweza
sam jang.

kwenye hii movie ambayo pia inaitwa masquerade starring alikuwa ni lee byung hun (mr sunshine drama) na han hyo joo (w drama)
Gwanghae20.jpg

kwa anayetaka kuiangalia
Masquerade 2012 at Dramanice
Uyu Eugene Amecheza Sana Movie Kuliko Drama?
 
Back
Top Bottom