Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Huwaga Najiuliza Namimi Ntakuja Potea Jf Kiasi Hiki! Wakati Hata Siku Aitapita Mpka Nione @Damushin Kapost Nini?

Lol!
hahahahahahaaaa nilifikiri huu ugonjwa unanisumbua peke yangu kumbe nina mwenzangu?
ila mimi sijaathiriwa sana na waandishi mahiri wa JF hivyo basi ugonjwa wangu unaweza kutibika.
unaonaje tukajaribu kuishi mwezi mmoja bila ya thread hii?
aigoooo tumekuwa kama eugene choi na Ae sin humu ndani.
hmmmm! tuwaachie legendary wa thread hii waiendeleze wanapopata nafasi japo kwa mwezi mmoja.
ila itawezekana kwangu mimi haliyakuwa siwezi kukaa bila ya kumjibu mtu pindi anapohitaji msaada?
goblin-quote-kimgoeun3.jpg
 
“Maze Runner” Star Ki Hong Lee To Make Korean Drama Debut Opposite Ha Ji Won And Jin Goo
Ki Hong Lee ambaye anafanya kazi zake hollywood amethibitisha kushiriki kwenye upcoming spy drama inayokwenda kwa jina la “Prometheus”
muigizaji huyo atabeba uhusika wa CIA agent anayeitwa Frank lee.
muigizaji huyo alipewa offer ya kushiriki kwenye drama hiyo miezi nane iliopita lakini alichelewa kuthibitisha ushiriki wake kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kuigiza drama za korea.
mwishoni mwa mwezi september inatarajiwa drama hiyo kuanza kutengenezwa na mwanzoni mwa mwaka 2019 itaanza kuonyeshwa.
bajeti ya drama hiyo inakadiriwa kufikia won billion 30 ambazo ni wastani wa billioni 60 za kitanzania.
0c4e9c8d4fa041a5be3d59acef8b8ce2.jpeg
 
hahahahahahaaaa nilifikiri huu ugonjwa unanisumbua peke yangu kumbe nina mwenzangu?
ila mimi sijaathiriwa sana na waandishi mahiri wa JF hivyo basi ugonjwa wangu unaweza kutibika.
unaonaje tukajaribu kuishi mwezi mmoja bila ya thread hii?
aigoooo tumekuwa kama eugene choi na Ae sin humu ndani.
hmmmm! tuwaachie legendary wa thread hii waiendeleze wanapopata nafasi japo kwa mwezi mmoja.
ila itawezekana kwangu mimi haliyakuwa siwezi kukaa bila ya kumjibu mtu pindi anapohitaji msaada?
goblin-quote-kimgoeun3.jpg
Inabidi Tujaribu Kweli!

Mi Naona Tuanze Mwenzi Huu Wa Sept.

Tunalog off Kabisaa Tutakuwa Tunasoma Bila Kulog,

Mi Mwenyewe Sidhani Pale Ambapo Umekaa Unasubiri Upate Alert Ya Damushin Lol!
 
Inabidi Tujaribu Kweli!

Mi Naona Tuanze Mwenzi Huu Wa Sept.

Tunalog off Kabisaa Tutakuwa Tunasoma Bila Kulog,

Mi Mwenyewe Sidhani Pale Ambapo Umekaa Unasubiri Upate Alert Ya Damushin Lol!
chincha?
really?
basi tufanye hivyo mwezi ujao inshaallah.
sidhani kama mwezi ujao kuna drama ya muigizaji anayenivutia sana.
kwa waigizaji mashuhuri labda project ya so ji sub na project ya jang hyuk kama sikosei.
project ya hyun bin na park shin hye mpaka itakapomaliza MR SUNSHINE mwezi November.
huwezi amini hii ni comment yangu ya 1135 kuiandika ndani ya thread hii
duh hawa JF ndio nini kuniwekea takwimu kila thread niliyowahi kuitembelea.
HBS-SJS-BOSS-2017-4-1200x800.jpg
 
Damushin Ahsante kwa elimu mulya hii aisee..
Mkuu kama utapata wasaa naomba unipe historia ya jumong na utawala wake
  1. mfalme yuri ndiye aliyerithi madaraka ya baba yake na kuiongoza goguryeo iliokuwa tayari imeshagawanyika na aliongoza vita nyingi sana dhidi ya nchi ndogo ndogo na kuweza kuiongezea goguryeo mipaka yake.
  2. alikuwa na watoto sita ambao ni dojeol, haemyoung, muhyul, go jaesa, hae seryu, yeojin na hae sae kju
  3. dojeol alifariki dunia ndipo akampa cheo cha urithi wa mfalme haemyeong lakini baadae akampa heshima hiyo mtoto wake mwengine wa kiume ambaye ni muhyul
  4. baada ya kufariki mtoto wake muhyol alirithi madaraka na kuzidi kuongeza mipaka ya eneo la goguryeo kwa njia ya mapambano ya vita.
  5. muhyool ndiye aliyemaliza vita ya muda mrefu kati ya mababu zake wawili ambao ni jumong na daeso kwa sababu yeye ndiye aliyefanikiwa kumuuwa daeso na kuimiliki nchi ya buyeo.
  6. mwaka 37 alifanikiwa kuitawala nchi ya Nakrang na kabla ya hapo alimtumia mtoto wake ambaye ni ho dong kwa ajili ya kuivamia nchi hiyo ya Nakrang. Wakati huo hodong alikuwa na miaka 16.
  7. ubabe wake kwenye uwanja wa vita ulipelekea kupewa heshima ya daemusin ("Great Holy Warrior King")
  8. baada ya kufariki daemusin alitawala mdogo wake ambae ni Hae Saek-ju ambaye alikuwa mfalme wa 4 na kupewa jina la Mobon ambaye alifariki miaka 4 baadae kwa ugonjwa.
  9. baadae alitawala Mobon ambaye alikuwa ni mtoto wa kwanza wa Damushin muhyool, mobon aliuliwa na kiongozi aliyejulikana kwa jina la Duro.Ukoo wa Yuri upande mmoja walikuwa wakitumia jina Hae na inasemekana Mobon ndiye mfalme wa mwisho kutumia jina la Hae.
  10. baadae akatawala Taejodae na kihistoria ndiye mtawala wa pili duniani kukaa madarakani kwa miaka mengi, Taejo wa goguryeo alikaa madarakani miaka 93.alikuwa ni mtoto wa go jaesa ambaye naye alikuwa mtoto wa Yuri kupitia ukoo wa Go, Inamaana ukoo wa go ambao chimbuko lake ni jumong ulirudi tena madarakani.
kwenye drama ya kingdom of the wind muigizaji jung ji young aliigiza nafasi ya mfalme yuri na song il kook aliigiza nafasi ya muhyool daemusin ambaye ni mjukuu wa jumong
kotw_fi_09.jpg

kotw_fi_03.jpg

kotw_fi_14.jpg

picha hizi zimepigwa siku ya interview ya cast member wote wa hii drama mwaka 2008.
 
chincha?
really?
basi tufanye hivyo mwezi ujao inshaallah.
sidhani kama mwezi ujao kuna drama ya muigizaji anayenivutia sana.
kwa waigizaji mashuhuri labda project ya so ji sub na project ya jang hyuk kama sikosei.
project ya hyun bin na park shin hye mpaka itakapomaliza MR SUNSHINE mwezi November.
huwezi amini hii ni comment yangu ya 1135 kuiandika ndani ya thread hii
duh hawa JF ndio nini kuniwekea takwimu kila thread niliyowahi kuitembelea.
HBS-SJS-BOSS-2017-4-1200x800.jpg
Yah Chincha! Sijajua Kama Nimejibu Sawa!

Inabidi Tukae Pembeni Kidogo, Tuone Kama Tutaweza Bila Maisha Ya Hiki Chama!! Maana Tumebaki Siye Tuuh.

Ila Tupo Vizuri Wawili Tuuh Katika Nchi Ya Joseon Na Tukipata Ramyeon Pembeni na Sojuu Tukisindikiza Na Kimchi.

Usije Nikimbia Tuuh Nawewe Maana Huwaga Uchelewi.
 
mhhhhhhh niwe mkweli sijabahatika kuiangalia heartless city.
ila kama unahitaji drama zenye kuzungumzia ishu za criminal, action,thriller, investigation basi jaribu zifuatazo.
  1. life on mars
  2. voice season 1
  3. voice season 2
  4. black
  5. tunnel
  6. secret forest
  7. criminal mind
  8. signal
  9. partners for justice
  10. bad guys 1
  11. bad guys 2
  12. phantom
  13. duel
  14. incarnation of money
  15. pied piper
  16. sign
  17. mad dog
  18. innocent defendant
  19. Healer
  20. Come and Hug Me
Barikiwa sana mkuu
 
dah mkuu si nitaandika mpaka kesho na bado sijamaliza ila labda tuanzie hapa kwa ufupi
  1. jina lake la kuzaliwa aliitwa jumong (chumong) ila baadae alipewa heshima ya dongmyeong seongwang (holy king of the east) baada ya kufanikiwa kuanzisha taifa la Goguryeo kwa msaada mkubwa wa mwanamama soseono mnamo mwaka 37 B.C
  2. alikuwa ni mtoto wa Hae mosu na lady yuhwa lakini maisha yake yote alilelewa na mfalme geumwa wa Buyeo ya Mashariki ambapo taifa hilo mwanzoni lilikuwa ni koloni la Han china
  3. baadae aliondoka buyeo kwa lengo la kutimiza ndoto za aliyekuwa baba yake mzazi za kuwakomboa watu wa Gojoseon ambao walikuwa chini ya mabavu ya wachina.
  4. Ndipo alipokutana na mwanadada soseono kwenye harakati zake na kuhamia Jolbon na kuanzisha taifa la Goguryeo mnamo mwaka 37 B.C
  5. mnamo mwaka wa 19 BC mke wake wa kwanza alifanikiwa kukimbia nchini buyeo na kumfuata jumong akiwa na mtoto wao wa kwanza ambaye ni Yuri na wakati huo mwanamama soseono alishakuwa na watoto wawili ambao ni biryu na onjo.
  6. ujio wa lady ye ulipelekea soseono avuliwe nyadhifa ya kuwa malikia kwa sababu sheria zao walizozitunga ilikuwa zinamtaka mke wa mwanzo awe ndiye malikia.
  7. baadhi ya hadithi zinadai ya kwamba soseono aliamua kuondoka goguryeo baada ya kugundua ya kwamba jumong anataka kumpa madaraka ya urithi mtoto wake wa kwanza ambaye ni Yuri licha ya kwamba hakuwepo kwenye harakati za ukombozi kwa muda mrefu.
  8. ndipo soseono akaelekea maeneo ya kusini na watu wake kusini ambayo kwa sasa ndiyo korea kusini na kuanzisha taifa la Baekje, aliamua kuchagua ardhi ya kusini kwa sababu ardhi ya kusini ilikuwa ni bora sana kwa shughuli za uzalishaji na pia vyanzo vya maji vilikuwepo kwa urahisi sana ukilinganisha na Goguryeo.
  9. hivyo basi kukawa na mataifa mawili ambayo ni goguryeo ambayo eneo lake kubwa ilikuwa ni kaskazini ya korea na baekje ambalo eneo lake kubwa ilikuwa ni kusini mwa korea na msingi wa mataifa hayo ni jumong na soseono.
  10. jumong alimrithisha madaraka mtoto wake Yuri na alifariki akiwa na miaka 40 mnamo mwaka 19 BC.
  11. taifa la goguryeo lilidumu kwa miaka 705 hadi utawala wake ulipoangushwa kutokana na muungano wa mataifa mawili ya Tang china na Shilla mnamo mwaka 668.
  12. Nadhani kuhusiana na hadithi ya jumong tuishie hapo baadae tutamuangalia bwana yuri ambaye ndiye mfalme wa pili.
song il kook aliigiza nafasi ya jumong kwenye drama ya the book of the three hans na mwanadada han hye jin aliigiza nafasi ya soseono hii ilikuwa ni miaka 12 iliopita.
kwa miaka hii hakuna drama iliofikia kiwango cha kuangaliwa na 50% ya wakorea ispokuwa jumong.
unajua huyu jamaa kwa aibu aliyokuwa nayo ilimfanya amchumbie mke wake kwenye gari na haliyakuwa alishakodi sehemu nzuri ya kumchumbia mwanamama msomi mwenye PHD ya sheria anayeitwa jung seong yeon. eti aliwaogopa mashabiki si unajua alikuwa ni national actor kipindi hicho cha jumong.
😛😛😛
2007090309050092501_103814_0_1248423107.jpg
Baada Ya Kuwa Na Taifa la Jumong Na Seseono Buryeo Lilienda Wapi!???
 
Yah Chincha! Sijajua Kama Nimejibu Sawa!

Inabidi Tukae Pembeni Kidogo, Tuone Kama Tutaweza Bila Maisha Ya Hiki Chama!! Maana Tumebaki Siye Tuuh.

Ila Tupo Vizuri Wawili Tuuh Katika Nchi Ya Joseon Na Tukipata Ramyeon Pembeni na Sojuu Tukisindikiza Na Kimchi.

Usije Nikimbia Tuuh Nawewe Maana Huwaga Uchelewi.
hahahahahaaaaa umenichekesha sana mpaka watu wanadhani tumezaliwa joseon kumbe tupo Tz.
tarehe 31/08/2018 itakuwa siku ya Ijumaa tunasitisha mkataba kwa muda wa kuitembelea hii thread pendwa.
si kwamba tunafanya hivyo kwa ajili ya kutafuta kiki kwa mashabiki wa thread hii ila umefika muda wa kuishi kimya kimya kama mwanzo tulipokuwa hatujaifahamu hii thread tuone na sisi kiupande wetu kama itawezekana.
kwa hivyo tutaiangalia MR SUNSHINE bila ya mrejesho na uchambuzi wetu humu ndani.
no update
no news za celebrities
hahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaa
ni sawa sawa na kumwambia demiss asiingie chit chat na MMU.
say-bye-in-korean-12.jpg
 
Baada Ya Kuwa Na Taifa la Jumong Na Seseono Buryeo Lilienda Wapi!???
pande zote mbili walijitambulisha kama ni warithi wa buyeo.
buyeo mashariki utawala wao uliishia kwa daeso baada ya kuuliwa na mfalme muhyool daemusin wa goguryeo.
lakini pia kulikuwa na buyeo nyengine ambayo utawala wake uliishia mwaka 410 baada ya kushindwa vita na mfalme gwanggaeto wa goguryeo.
 
hahahahahaaaaa umenichekesha sana mpaka watu wanadhani tumezaliwa joseon kumbe tupo Tz.
tarehe 31/08/2018 itakuwa siku ya Ijumaa tunasitisha mkataba kwa muda wa kuitembelea hii thread pendwa.
si kwamba tunafanya hivyo kwa ajili ya kutafuta kiki kwa mashabiki wa thread hii ila umefika muda wa kuishi kimya kimya kama mwanzo tulipokuwa hatujaifahamu hii thread tuone na sisi kiupande wetu kama itawezekana.
kwa hivyo tutaiangalia MR SUNSHINE bila ya mrejesho na uchambuzi wetu humu ndani.
no update
no news za celebrities
hahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaa
ni sawa sawa na kumwambia demiss asiingie chit chat na MMU.
say-bye-in-korean-12.jpg
Hahahahhahahah Eti kutafuta Kiki!!!!

Yah Inabidi Tuchukue Likizoo Ila Unaonaje Tukisubili Mpka Sunshine Iishe, Hmmm!!! Lakini ngoja Acha tuanze Hiyo likizo, Tuone tutaweza Je!!!?

Uku Tukienda Zetuuu Busan Tukale Sushi na Jjgae.

Weleee
 
pande zote mbili walijitambulisha kama ni warithi wa buyeo.
buyeo mashariki utawala wao uliishia kwa daeso baada ya kuuliwa na mfalme muhyool daemusin wa goguryeo.
lakini pia kulikuwa na buyeo nyengine ambayo utawala wake uliishia mwaka 410 baada ya kushindwa vita na mfalme gwanggaeto wa goguryeo.
Nipe Drama Ya Zamni Niicheki, Maana Now Nina Life na Sunshine Tuuh.

Vagabond Lini!???

Nimejaribu Kuicheki Jewel in the Palace Lakini Naona Picha Yake Kwa Maana Ya Video Aiko Sawa.
 
huu mtandao wa soompi upo more update kuliko mtandao wowote unaoandika habari za korean celebrities.
masaa yaliopita waliweka habari hii
BTS Breaks Record As “IDOL” MV Hits 10 Million Views
leo hii BTS wamerelease video ya wimbo wao mpya unaojulikana kwa jina la Idol saa 6pm kwa saa za korea na ilipofika saa 10:16 pm kwa saa za korea video ya wimbo huo imeangaliwa duniani na mara millioni 10.
ina maana ndani ya masaaa 4:16 wimbo huo umeangaliwa mara millioni 10
ndani ya muda huo wimbo huo umepokea likes zinazofikia millioni 2.
bts-10-million.png
unaambiwa BTS wamevunja rekodi ya wimbo wao wenyewe unaoitwa fake love ambao uliangaliwa na mara millioni 10 ndani ya masaa 4 na dakika 56.
BTS ni more fire
update ya habari hii dakika 45 zilizopita kupitia mtandao wa soompi

BTS’s “IDOL” MV Smashes Another Record As It Reaches 20 Million Views
ilipofika saa 12;35 a.m kwa saa za korea wimbo huo umefikia rekodi ya kuangaliwa mara millioni 20.
inamaana ndani ya masaa sita na dakika 35 wimbo huu ushaangaliwa mara millioni 20 duniani wakati huo mimi wala sijaiangalia hata mara moja
hahahahahaaaa hatari sana hawa jamaa halafu mtu ananishangaa mimi kuwafuatilia wakorea na muziki wao wakati nicki minaj anataka kushirikishwa kwenye wimbo wa BTS.
bts-idol-20.png
tufahamu ya kwamba muda huu nchini korea ni usiku wa saa 7:45 AM na tayari ni tarehe 25 August.
kwa sasa mpaka wanaweka taarifa hii mtandao wa soompi video hii imepata likes million 3.2
BTS-920x584.jpg

huku kwetu mtu akifikisha view millioni moja ana kelele kama panya.

Hahahahahahhahaah Dah!! Panyaaa

Nakufananishaa Na Rafiki Yangu Wa Huko Huko Kuvuka Bahari, Ni Ana Maneno Akianza Tuuh Kuongee Mbavu Sina, Anayoyaongeaa Yaani Ni Vichekesho Tuuh

Mara Nyingi Nakufananisha Nae Sana.
 
Hahahahhahahah Eti kutafuta Kiki!!!!

Yah Inabidi Tuchukue Likizoo Ila Unaonaje Tukisubili Mpka Sunshine Iishe, Hmmm!!! Lakini ngoja Acha tuanze Hiyo likizo, Tuone tutaweza Je!!!?

Uku Tukienda Zetuuu Busan Tukale Sushi na Jjgae.

Weleee
mimi mwenzio hata kuogelea sijui sasa kwenda busan kutaleta faida gani kwangu mimi?
bora twenda kwenye mji mpya na wa kisasa unaoitwa Songdo nipate kunywa chai nyumbani kwa Song il Kook na baadae niombe ajira ya kuwatembeza mapacha watatu bila ya malipo.
najua nitakapotembea na song triplets kila sehemu nitajitengenezea fedha kwa mgongo wao.

wazo lako ni zuri lakini Mr Sunshine inamaliza mwezi November na baadae inafuata memories of alhambra drama ya hyun bin na mwanadada park shin hye na usisahau kuna drama ya boyfriend inayowakutanisha song hye kyo na park bo gum.
Na drama hii ya memories of alhambra location zao si za nchi hii, tayari wameshamaliza kurekodi nchini hispania kwenye mji wa granada, hivi karibuni walikuwepo hungary kwenye mji wa budapest na kwa sasa sijui wameenda nchi gani inayopakana na urusi.

pia usisahau fundi jang hyuk anarudi tena akiwa kama mpiganaji wa ulingoni kwenye drama inayoitwa bad papa (baba mbaya)
usisahau mwishoni mwa mwaka kuna korean drama awards za mashirika ya KBS, MBC, SBS
hahahahaaaaaa tunaweza kujikuta tumeganda humu ndani kama tumewekea vizizi na mshana junior.
mara paap 2019 inaanza na Drama ya Asadal inayowakutanisha song joong ki, jung dong gun inaanza
mara paap 2019 drama ya kijasusi ya prosmetheus inaanza inayowakutanisha Ha ji won na jin goo
mara paap 2019 season 2 ya waikiki drama
bila ya kusahau mwenye kutoa uhai ni Mungu mweza wa yote.
57525ec35b5aa0b2128b47ce-2-full-ideas.jpg
 
Hahahahahahhahaah Dah!! Panyaaa

Nakufananishaa Na Rafiki Yangu Wa Huko Huko Kuvuka Bahari, Ni Ana Maneno Akianza Tuuh Kuongee Mbavu Sina, Anayoyaongeaa Yaani Ni Vichekesho Tuuh

Mara Nyingi Nakufananisha Nae Sana.
nilimpa password ya computer mdogo wangu cha ajabu sasa anajifanya kama ndio nimempa haki miliki ya kutumia pc yangu.muda wowote anaojisikia.
nimebadilisha password na kuweka neno panya
 
Back
Top Bottom