Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

mimi mwenzio hata kuogelea sijui sasa kwenda busan kutaleta faida gani kwangu mimi?
bora twenda kwenye mji mpya na wa kisasa unaoitwa Songdo nipate kunywa chai nyumbani kwa Song il Kook na baadae niombe ajira ya kuwatembeza mapacha watatu bila ya malipo.
najua nitakapotembea na song triplets kila sehemu nitajitengenezea fedha kwa mgongo wao.

wazo lako ni zuri lakini Mr Sunshine inamaliza mwezi November na baadae inafuata memories of alhambra drama ya hyun bin na mwanadada park shin hye na usisahau kuna drama ya boyfriend inayowakutanisha song hye kyo na park bo gum.
Na drama hii ya memories of alhambra location zao si za nchi hii, tayari wameshamaliza kurekodi nchini hispania kwenye mji wa granada, hivi karibuni walikuwepo hungary kwenye mji wa budapest na kwa sasa sijui wameenda nchi gani inayopakana na urusi.

pia usisahau fundi jang hyuk anarudi tena akiwa kama mpiganaji wa ulingoni kwenye drama inayoitwa bad papa (baba mbaya)
usisahau mwishoni mwa mwaka kuna korean drama awards za mashirika ya KBS, MBC, SBS
hahahahaaaaaa tunaweza kujikuta tumeganda humu ndani kama tumewekea vizizi na mshana junior.
mara paap 2019 inaanza na Drama ya Asadal inayowakutanisha song joong ki, jung dong gun inaanza
mara paap 2019 drama ya kijasusi ya prosmetheus inaanza inayowakutanisha Ha ji won na jin goo
mara paap 2019 season 2 ya waikiki drama
bila ya kusahau mwenye kutoa uhai ni Mungu mweza wa yote.
57525ec35b5aa0b2128b47ce-2-full-ideas.jpg

000.jpg

TripletsBike.jpg
Inamaana Kukaa kotee Uko Na Bahari Hujui Kuogelea Mpemba Wewe!!!
Hahahhaahahhaha Dah!!! Kuwatembeza Mapacha Bila Kulipwa Duuh We Noma...

Tukifika Seoul Tutaachana Apo Kila Mtu Ataingia Mitaa Yake Na Tutakutana Tena Apo Kurudi Nchi Ya Mpenda Wanyongee...

Mwezangu Sasa Inabidi Tusisubili Mpka Sunshine Iishe Nahisi Sisi Tuanze Tuuh Likizo Yetu.
 
nilimpa password ya computer mdogo wangu cha ajabu sasa anajifanya kama ndio nimempa haki miliki ya kutumia pc yangu.muda wowote anaojisikia.
nimebadilisha password na kuweka neno panya
Anhaa!! Mwambie Asiimiliki ya Kazi Iyo.

Nawe Unamdogo Hmmmmm!!!!
 
Sasa hiyo likizo mnajipa kwa muda gani? Nipeni hata drama 5 wakat nawasubiri mrudi. Natizama Mr sunshine na come and hug me kwa sasaivi

Sent using Jamii Forums mobile app
  1. my ID is gangnam beauty inasemekana ipo vizuri sana na nimekusudia kuitafuta siku chache zijazo
  2. 30 but 17 nayo ipo vizuri jaribu kuifatilia
  3. familiar wife drama ameigiza ji sung nayo inaendelea
  4. lovely horribly ya mwanadada song ji hyo imeanza wiki chache zilizopita
  5. life drama kama ni mpenzi wa medical drama pia ipo vizuri sana.
bado tunajishauri tuchukue likizo ya bila malipo mwezi gani?
 
  1. my ID is gangnam beauty inasemekana ipo vizuri sana na nimekusudia kuitafuta siku chache zijazo
  2. 30 but 17 nayo ipo vizuri jaribu kuifatilia
  3. familiar wife drama ameigiza ji sung nayo inaendelea
  4. lovely horribly ya mwanadada song ji hyo imeanza wiki chache zilizopita
  5. life drama kama ni mpenzi wa medical drama pia ipo vizuri sana.
bado tunajishauri tuchukue likizo ya bila malipo mwezi gani?
Asante hizo zote sijazitazama nitazifatilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  1. my ID is gangnam beauty inasemekana ipo vizuri sana na nimekusudia kuitafuta siku chache zijazo
  2. 30 but 17 nayo ipo vizuri jaribu kuifatilia
  3. familiar wife drama ameigiza ji sung nayo inaendelea
  4. lovely horribly ya mwanadada song ji hyo imeanza wiki chache zilizopita
  5. life drama kama ni mpenzi wa medical drama pia ipo vizuri sana.
bado tunajishauri tuchukue likizo ya bila malipo mwezi gani?
Hahahahhahahaha!

Sept Tuchukue.
 
hahahahahaaaaa umenichekesha sana mpaka watu wanadhani tumezaliwa joseon kumbe tupo Tz.
tarehe 31/08/2018 itakuwa siku ya Ijumaa tunasitisha mkataba kwa muda wa kuitembelea hii thread pendwa.
si kwamba tunafanya hivyo kwa ajili ya kutafuta kiki kwa mashabiki wa thread hii ila umefika muda wa kuishi kimya kimya kama mwanzo tulipokuwa hatujaifahamu hii thread tuone na sisi kiupande wetu kama itawezekana.
kwa hivyo tutaiangalia MR SUNSHINE bila ya mrejesho na uchambuzi wetu humu ndani.
no update
no news za celebrities
hahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaa
ni sawa sawa na kumwambia demiss asiingie chit chat na MMU.
say-bye-in-korean-12.jpg
Nimekuja huku mmeniita jaman japo nampenda Le mi niho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa ndugu, nlikua nimezoea kuomba kwa watu lakini saiv mkishataja tu najishushia mzigo mwenyew hapo baada ya maelezo uliyonipa ya jinsi ya kudownload. Maisha yenyewe yalivyo yanaboa bila hichi kilevi naweza chizika

Sent using Jamii Forums mobile app
ok,unajua baadhi ya wakati hufikia wakati najiuliza
hivi humu ndani ni watu wawili tu ndio wanaofuatilia korean drama kipindi hiki?
ukija humu ndani unakuta wachangiaji ni watu wawili na wengineo wanapita na kuondoka. Ndio maana nataka nijaribu je inawezekana kuendelea kufuatilia korean drama kama wengineo munavyofanya lakini nikawa siandiki chochote kwenye thread hii?
binafsi sifanyi hivyo nionekane najisikia mbele ya wenzangu
hapana hapana hapana.musije mukawa na dhana kama hizo.
 
ambae anaucheki familiar wife naomba anipe mrejesho ,vp upo vzr au kupoteza mb t ?? niliucheki episodes 4 za mwnzo nikauacha kdg

Sent using Jamii Forums mobile app
binafsi niliishia episode ya 2.
inaonekana time travel ndio zinakuzingua unapoiangalia au stori yake hujaipenda?
voice season 2 ipo vizuri kama ni mpenzi wa criminal drama na wiki hii inaendelea episode ya 5, 6.
hivi huku kwetu tuna shirika linalofanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu kisayansi?
hivi huku kwetu idara yetu ya ulinzi inaweza kutatua matatizo ya kihalifu kwa kutumia special customer service za njia ya mawasiliano?
nakusudia kusema ya kwamba nchi yetu tuna uwezo wa kumtrack muhalifu taarifa zake zote zinazomuhusu, kwa mfano kufahamu DNA za muhalifu, kufahamu taarifa za kifedha za muhalifu na kuweza kuzizuia, kufahamu taarifa za usafiri za muhalifu, anapoishi n.k

pia jaribu kuiangalia drama inayoitwa life on mars.
nayo pia inahusu masuala ya utatuaji wa matatizo ya kihalifu, ni remake ya program ya kituo cha BBC.
  • jamaa anajikuta anarudi nyuma mwaka 1988 ambapo ni sawa na miaka 30 iliopita baada ya kupigwa risasi
  • jinsi hiki kikundi cha polisi wanavyotatua matatizo wewe muangaliaji wa hii drama utapenda ukitaka usitake, hamuna cctv camera, hamuna computer, hamuna database kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za watu mbali mbali,hamuna shirika lolote linalihusiana na kufanya chunguzi za kisayansi, ni mwendo wa kutumia akili mwanzo mwisho.
  • location, music, uvaaji wao,usafiri wao na vyenginevyo vinakushajihisha uamini ya kwamba hii drama matukio yake ni ya miaka 30 iliopita.
  • wakati huku kwetu unaangalia filamu yenye kuzungumzia matukio ya kizamani yaliotokea kipindi cha utawala wa machifu wakuu cha ajabu pembeni yake unakuta nyumba imejengwa kwa matofali na wanatumia vyombo vya plastic. Tuna safari ndefu sana.
Life_on_Mars-p01.jpg

 
Back
Top Bottom