MR SUSHINE DRAMA
wakati huu tunangojea subtitle ya episode ya 19 na next episode ya 20 hapo kesho ngoja tuondoe stress zinazotukabili kwenye maisha yetu ya kila siku, kuna wengine huondoa stress kwa kunywa pombe na akina sisi wengineo tunaondoa stress zetu za maisha kwa mapira na korean drama.
Na bahati mbaya wiki hii ulevi wangu mkuu wa manchester united haujaingia sokoni.
binadamu kumbe akili zetu zenye mihemuko ya kimwendo kasi tunazijuwa wenyewe, ngoja nijicheke mwenyewe kwanza kabla sijaandika sentensi niliyokusudia kuiandika.
hahahahaahhahahahaaaaaaaa
kuna mashabiki wameanza kumlalamikia muandishi wa drama hii ambaye ni mwanamama
kim eun sook pamoja na director
Lee eung bok.
uvumilivu umeanza kuwashinda wafuatiliaji wa hii drama kwa sababu imeshafika episode ya 18 lakini hawajaona hata dalili ya
kiss scene.
- kuna wale wanaongojea kwa hamu kiss scene kati ya captain eugene choi (lee byung hun) na lady go ae sin (kim te ri), kundi hili la mashabiki ndio wapo wengi zaidi duniani na povu lao hata nguo za wafungwa wa gereza la keko au kiinua miguu lililopo zanzibar unaweza kufulia, bahati nzuri Kwenye kundi hili mimi sihusiki
- kuna wale wanaongojea kwa hamu kiss scene kati ya mtemi aliyezaliwa na wazee wawili waliokuwa wakiuza butcher goo dong mae (yoo yeon seok) na mwanadada kudo hina (kim min jung) ambaye ameachika na mume wa kijapani na pia ndiye mtoto wa lee wan ik msaliti wa joseon, pia kwenye kundi hili mimi simo.wafuasi wa kundi hili wana hasira kali kuliko upanga wa Dong mae, unapaswa ukae nao mita 600.
- kundi la tatu nipo peke yangu na sitaki mfuasi kwenye kundi hili,bado nasuburia kwa hamu kiss scene kati ya ahjumma Haman-daek na yule ahjussi ambaye pia ni mtumishi wa lady aesin na mzee go sa hong. Nitafurahi sana kama hawa wazee wawili watafunga ndoa na kuishi kwa amani na upendo na kuondokana na minyororo mizito ya utumwa,nasisitiza tena kwenye kundi hili sihitaji mfuasi.
aminas ,
talnam hivi nyinyi mupo team gani kwenye kiss scene?
hahahahahahhaaaaaaaa bangi za usiku ni mbaya sana zinaweza kukufanya ukayanunue makontena ya makonda.
huku kwetu serikali imebana, kule kwenye mpira manchester united wamebana na huku kwenye drama mwanamama
kim eun sook ameendelea kubana.
huu mwaka kwa hali inavyokwenda sisi wengine tutakufa na tai shingoni.