wahudumu wa humu ndani naomba munitayarishie chupa 50 za soju tafadhali, nataka nilewe mpaka nitapike korosho za bwana amunike wa lesotho.
halafu pia naomba mara hii munichagulie nyinyi wadau drama za kuangalia hata kama ziwe zimeshapita na wakati, ni matumaini yangu sitakutana na balaa nililolishuhudia kwenye thread ya wapenzi wa series.
heheheheheeeeee niliomba websites ya kuangalia series mpaka leo ni mwezi wa pili sijapatiwa mpaka nikaingia mzigoni mwenyewe.
mhhhhhhhh kweli binadamu tunatofautiana.
wala musiogope jamani hakuna mtu aliyeangalia drama nzuri zote za wakorea.
acha leo nifunguke kabla ulevi haujatoka, niwe mkweli sijawahi kuziangalia drama zifuatazo japokuwa zinasifiwa na kila mdau
- dong yi : hahahahahahaaaa munajuwa kwa nini sikuchangia comment zilizokuwa zinaisifia hii drama zikiongozwa na huyu ahjumma mtarajiwa miaka 30 ijayo XYZ,ni kwa sababu sikumbuki hata kama nilifika episode ya 5 ndio maana nikaufyata kimya.
- jewel in the palace : hii hata siifahamu hata inavyoanza, kwani hizi drama tunajibia mtihani?
- drama zote za ji sung ukiondoa the innocent defendant.
- drama zote za ji chang wook ukiondoa K2.
kama mutashindwa ni bora niende kwa mchungaji au shekhe aniombee nipumzike kuangalia drama japo kwa wiki mbili (shetani wangu wa likizo amerudi tena).
namimi nahitaji kuona raha ya kujisikia kama anavyojisikia bibi yenu mtarajiwa.
- terius behind me drama = imeshamaliza
- the beauty inside drama = imeshamaliza
- room no 9 = itamaliza jumapili.
- where star land = huenda ikamaliza jumatatu
- bad papa = huenda ikamaliza jumanne.
kama mutashindwa kuniwekea japo drama 15 kwa kila mtu ili nichague nitahama mtaa wenu.
povu naruhusu siku ya leo.
ujumbe wa leo
Damushin hajawahi kuwa serious