Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hakika wewe ni mchochezi, na nisipoimaliza hii drama una kesi ya kujibu

Sent using Jamii Forums mobile app
ndio ukamtuma rafiki yako kipenzi aje anirushie kichambo kuliko cha instagram?
😛😛😛

endelea kuiangalia mpaka atakapoingia mwanadamu anayeitwa kim nam gil (bi dam)
1550307128585.png
 
hili neno akulaani lina maana gani huko upande wa pili?
kwetu sisi maana yake ni pesa au utajiri.
😛😛😛

kama maandishi yangu yalivuka mipaka nakuomba radhi ila na wewe unadhani huyu Khantwe anaweza kuangalia drama yenye episode 60 bila ya kuiba mchumba?
ngoja tumuulize amefika episode ya ngapi tokea aweke nia ya kutaka kuifuatilia queen seondeok.

umemuonaje mfalme gwanggaeto?
ahsante Mungu kwa kumuondoa go damdeok duniani akiwa bado na umri wa miaka 38, kwa balaa alilokuwa nalo kama angelifikisha miaka 60 huenda angelitembeza kipigo mpaka huku kwetu kwa waarabu koko.
pengine leo hii damushin angelikuwa ni uzao wa general komu wa goguryeo.
😀😀😀

Cursed

Nilichukua likizo kidogo ya wiki mbili/tatu hivi maana niliangalia drama nyingi mfululizo mpaka kichwa kikawa kinauma.
Niliishia episode ya 54... jamaa nimemkubali sana vile mwanaume wa ukweli.
Huyu ndio mfalme sasa, mfalme jasiri anayeamini ktk kile anachokifanya na uzuri zaidi anawasikiliza wasaidizi wake.

Ajabu hajanivutia kivingine kama Song Ill Gook hahaaaaa
Labda vimasikio vyake tu viko kama vyangu, lol

Leo narudi upya kuiangalia, nina list kibao za kuangalia na zote nitazimaliza kwani nimeziba masikio sitaki kusikia makelele yenu ya drama zenu mpya.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
ndio ukamtuma rafiki yako kipenzi aje anirushie kichambo kuliko cha instagram?
😛😛😛

endelea kuiangalia mpaka atakapoingia mwanadamu anayeitwa kim nam gil (bi dam)
View attachment 1023906

Jamani jamani Khantwe achana na Bidam
Wewe chagua kati ya Archeon au Kim Yushin
Japo Bidam alinikera sana kwa kukosa imani juu ya Deokman iliyopelekea adanganywe kirahisi ila bado ni my favorite ktk hii series pendwa.

Ila Mishil kiboko jamani, halafu kazuriiiiii na ana akiliiii dah. Sio kwa kuichanganya kule mibaba, alijua kuutumia uzuri wake haswaaa.
Mimi yule kaka yake mjingamjinga ananiachaga hoi [emoji23][emoji23][emoji23]

Hakuna drama ambayo nimewahi kuvunjika mbavu kama hii kwenye scene za comedy
Jukbang na Godo niliwapenda sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Siku ya ndoa yako na Roy kim tutawapigia huu wimbo...

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Hahahahaha!

Anajua Kweli Hili!!

roy kim Una Hizi Khabari!?

Nahisi Utakua Muongoza Shughuli.
hahahahaaaaaaa roy kim amenambia nimjibie kwa njia hii kwa sababu hana maneno mengi kama ilivyo juisi ya mgonjwa wa kisukari.

Da'Vinci bado utashikilia msimamo wako wa kuandaa mikakati ya ndoa na huyu ahjumma mtarajiwa baada ya miaka 20 wakati hajawahi kuwa wakwangu?
ndoa za kulazimishwa kama mbuzi anayetaka kunywa maji ya mto mimi siwezi

drama : familiar wife
starring : ji sung na han ji min
ost : no longer mine
muimbaji: roy kim

Hahahahahaha!

Anayekulazimisha Ni Nani!?

au Tu Vinci angependa Kumuona roy kim Akifanya Haya!

na Anapenda Kuona Si Kukulazimisha!
 
Hahahahahaha!

Anayekulazimisha Ni Nani!?

au Tu Vinci angependa Kumuona roy kim Akifanya Haya!

na Anapenda Kuona Si Kukulazimisha!
inawezekana nimemuelewa vibaya, ila kwa kuwa anapendelea basi si vibaya ila sijui kama muhusika mwenyewe roy kim / damushin na yeye anapendelea hilo wazo la da'vinci?

Roy Kim (로이킴) – Only Then

nimejaa bando la internet kama bakhressa na fedha zake za unga wa ngano
 
Kwani Lazima Uwe Vile ambavyo Binadam Anapenda Uwe au Ufanye kila Kimfurahishacho Mtu hata Kama We Kinakuumiza!!

We Upendi na Wala Huwazi Ila Yeye Anapenda Kuona Ikitokea Ivyo Labda!

Lakini Yote ya Yote We Kwangu Ni Chinguya tena Lovely Chinguya! Hayo Mengine tumuachie Vinci Kwa Sasa

Nauku Tukifurahia Ushindi Wetu Wa Leo.
 
umemaliza bakuli zima la chakula cha maneno sielewi mimi nitapata wapi maneno ya kuondolea njaa yangu.
hongera kwa ushindi wa jana dhidi ya mtani wako lakini muwe munawasaidia fedha ya matumizi kwa sababu hali yao hairidhishi kwa kipindi hiki cha mpito.
 
Jamani, mimi mwenzenu nimekuja huku kwasababu nimenuniwa. Leo ni siku ya tatu tangu niulizwe namna ya kupakua hizi series za kikorea. Sasa mimi kila siku naonekana nikipakua zile ninazoangalia mimi kupitia The Pyratebay, naonekana nimedharau.
Naomba mnisaidie site na namna a kupakua hizi series za Kikorea.
Natanguliza shukrani

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
umemaliza bakuli zima la chakula cha maneno sielewi mimi nitapata wapi maneno ya kuondolea njaa yangu.
hongera kwa ushindi wa jana dhidi ya mtani wako lakini muwe munawasaidia fedha ya matumizi kwa sababu hali yao hairidhishi kwa kipindi hiki cha mpito.
Ahsante Sana!
Jana Robo tatu ya Uwanja tulija Siye,Mchango tosha Uo.
 
Jamani, mimi mwenzenu nimekuja huku kwasababu nimenuniwa. Leo ni siku ya tatu tangu niulizwe namna ya kupakua hizi series za kikorea. Sasa mimi kila siku naonekana nikipakua zile ninazoangalia mimi kupitia The Pyratebay, naonekana nimedharau.
Naomba mnisaidie site na namna a kupakua hizi series za Kikorea.
Natanguliza shukrani

Sent from my iPhone using JamiiForums
  1. Watch Asian Movies And Asian Dramas Online Free With English Subtitles | QuickDrama
  2. Watch free Drama Online at Dramanice
  3. https://kissasian.es/
kama unatumia software ya IDM itapendeza zaidi.
 
Jamani jamani Khantwe achana na Bidam
Wewe chagua kati ya Archeon au Kim Yushin
Japo Bidam alinikera sana kwa kukosa imani juu ya Deokman iliyopelekea adanganywe kirahisi ila bado ni my favorite ktk hii series pendwa.

Ila Mishil kiboko jamani, halafu kazuriiiiii na ana akiliiii dah. Sio kwa kuichanganya kule mibaba, alijua kuutumia uzuri wake haswaaa.
Mimi yule kaka yake mjingamjinga ananiachaga hoi [emoji23][emoji23][emoji23]

Hakuna drama ambayo nimewahi kuvunjika mbavu kama hii kwenye scene za comedy
Jukbang na Godo niliwapenda sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapo ndipo tunapokosanaga ukinisimulia drama mimi mzuka unakata kabisa kuangalia yani daah hapa umeshanikata stimu inabidi nikusanye tena nguvu za kuanza kuangalia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Hwayugi” Writers Hong Sisters Cleared Of Plagiarism Charges + To Possibly Take Legal Action Against Accuser.

ukisikia dawa ya moto ni moto basi ndio hii
kwa ufupi kuna muandishi mmoja wa webtoon novel anayejulikana kwa jina la Ttangyeol aliwafungulia kesi waandishi wawili wanaofanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu Hong Jung Eun na Hong Mi Ran (the hong sisters) kwa madai ya kumuibia kazi yake inayokwenda kwa jina la AEYUGI.

jamaa anasema baada ya kumuibia kazi yake wakabadilisha baadhi ya mambo ikiwemo jina kutoka AEYUGI hadi HWAYUGI jambo ambalo ni kinyume na sheria ya haki miliki hivyo basi akaiomba mahakama itoe hukumu ya kulipwa fidia kwa hasara iliotokezea.

juzi mahakama imetoa hukumu yake ambapo kwa mujibu wa taarifa rasmi ya mahakama inadai ya kwamba hawajaona kithibisho chochote chenye kuonyesha ya kwamba kazi ya HWAYUGI ni ya wizi.

Hong sisters baada ya kutolewa hukumu na mahakama na wao wanasema ya kwamba taarifa za kuvumishiwa kuiba kazi ya AEYUGI zimewaumiza sana kwa muda mrefu hivyo basi na wao wanafikira kufungua kesi dhidi ya wale wote waliovumsiha taarifa zisizokuwa na ukweli wowote dhidi yao (defamation).
1550353181877.png

nimewakumbuka wafuatao kupitia habari hii:
raisi ng'ombe
mwana wa mfalme wa kiume kima
karani mbwa
mwanamfalme wa kike pweza
zombie boo ja
 
Yeo Jin Goo In Talks To Star Opposite IU In New tvN Fantasy Drama

kama wawili hao watakubali offer hiyo basi yeon jin goo ataigiza uhusika wa manager wa hoteli inayoitwa Hotel del Luna baada ya tukio la ajabu kutokezea.
IU ataigiza uhusika wa CEO wa hotel del luna na kwa mujibu wa stori ni msichana asiyekuwa na tabia nzuri kwa wenzake, huko nyuma aliwahi kufanya kosa lilopelekea apewe laana ambayo inategemewa kudumu kwa miaka 1000.

drama inaitwa Hotel del Luna na waandishi wa drama hiyo ni hong sisters.
1550353928715.png

tvN tvN tvN tvN tvN
 
Hapo ndipo tunapokosanaga ukinisimulia drama mimi mzuka unakata kabisa kuangalia yani daah hapa umeshanikata stimu inabidi nikusanye tena nguvu za kuanza kuangalia

Sent using Jamii Forums mobile app

Ama kweli watu tupo tofauti! Mimi ukinisimulia ndio unanipa hamasa ya kuangalia!

Hata hivyo sijasimulia sana mbona? Nimesimulia kijuujuu tuu. Niliwahi kusimulia deep wakati hii thread inaanza nadhani.

Enjoy bhana, ni drama nzuri sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cursed

Nilichukua likizo kidogo ya wiki mbili/tatu hivi maana niliangalia drama nyingi mfululizo mpaka kichwa kikawa kinauma.
Niliishia episode ya 54... jamaa nimemkubali sana vile mwanaume wa ukweli.
Huyu ndio mfalme sasa, mfalme jasiri anayeamini ktk kile anachokifanya na uzuri zaidi anawasikiliza wasaidizi wake.

Ajabu hajanivutia kivingine kama Song Ill Gook hahaaaaa
Labda vimasikio vyake tu viko kama vyangu, lol

Leo narudi upya kuiangalia, nina list kibao za kuangalia na zote nitazimaliza kwani nimeziba masikio sitaki kusikia makelele yenu ya drama zenu mpya.

Sent from my iPhone using JamiiForums
yes upo sahihi, mwili wa lee tae gon ulikuwa ni zawadi tosha ya kumfanya aweze kuutendea haki uhusika wa mfalme gwanggaeto.

ukiniuliza ni muigizaji gani aliyenivutia mule ndani basi jibu langu ni kim jung hwa.

drama ilikuwa na episode takribani 90 lakini cha kushangaza tumeonyeshwa upande mmoja tu wa maisha ya damdeok akiwa kama ni mtawala wa goguryeo nao ni upande wa harakati zake za kuitanua kingdom yake mpaka kuwa empereror.

je raia wa goguryeo walifaidika vipi na kampeni zake za vita zisizokwisha?
kama tunavyofahamu unaweza ukawa na himaya kubwa kama ilivyo Tanzania lakini raia wako wakakosa huduma muhimu za kila siku, cha ajabu sijawahi kukutana na historia ya gwanggaeto inayoangazia hali halisi ya maisha kwa raia wake, vita inataka
maandalizi ya ya chakula na mtoaji chakula cha jeshi ni raia wa kawaida kwa sababu ndiye mlimaji mkuu kwa msaada wa land owner.

utawala wake wa ndani ulikuwaje kwa wale ambao walikuwa na mawazo tofauti na yakwake?

ndio maana kiupande wangu SEJONG anabaki kuwa mfalme bora kwa sababu utawala wake ulielemea pande zote.
1550585849701.png
 
Back
Top Bottom