ukiyapitia maeneno ya kujidai ya professor lipumba kuna kanuni fulani inaitwa utility (the total satisfaction received from consuming a good or service) .
hii theory nimekuwa nikiitumia hadi kwenye ulimwengu wa korean drama, nakumbuka hii drama ya the best chicken niliihifadhi
episode 4 za mwanzo kipindi kile ndio kwanza inaanza kuonyeshwa.
niliangalia takribani dakika 10 za mwanzo bahati mbaya haikunifanya niwe na uchu, hamu (satisfaction) kuiendeleza hivyo basi niliamua kuzifuta episode zote 4.
haijalishi dunia nzima waisifie drama fulani kuwa ni bora kama kiupande wangu hainipi mzuka wa kuifuatilia basi ni sawa sawa na ushindi wa Tanzania endapo lesotho atakapopata ushindi.
mfano mwengine kuna drama inaitwa let me introduce her ambayo kuna binti fulani aliniomba nimtafutie, hii ni wiki ya tatu nimeihifadhi kwenye PC lakini mzuka wa kuiangalia sina, naisubiria siku tutakayokutana tena maeneo ya uchawini nimkabidhi mzigo wake then niuhamishe kwenye macho yangu.