Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

WAIKIKI SEASON 2
Kwa wale wapenzi wa comedy season 2 ya waikiki imeanza rasmi siku ya jana, haijalishi hukubahatika kuangalia season 1 hii inakuhusu kuifuatilia.
unapaswa mbavu zako uzipeleke kwanza kwa fundi seremala apate kuziweka sawa zisije zikavunjika (ni amri na si ombi) kabla hujaingia kwenye ulimwengu wa waikiki.

aminas japokuwa bado unaendelea kusherehekea ushindi wa simba, na Taifa stars pindi utakapomaliza kugonga chupa zako za soju ya makonda naomba urudi kijiweni kwetu kabla sijachukia tafadhali.

Lee Yi Kyung a.k.a mzee wa gwenchanah gwenchanah ndiye muigizaji pekee aliyeshiriki season 1 na 2.
namnukuu director Lee Chang Min:

lee yi kyung amekuwa akija mara kwa mara ofisini kwangu, sikufikiria mara mbili kufanya maamuzi ya kumchagua tena kushiriki season 2. Kuhusu kuwachagua waigizaji wengine aliendelea kusema takribani waigizaji wote wana viwango vikubwa, nilitaka kuonyesha upande mwengine wa vipaji vyao vya uigizaji (comedy) na kiukweli nilikuwa nikiwagombeza mara kwa mara pindi wanapofanya makosa
View attachment 1054148
View attachment 1054149

lets go (가자 = gaja)
nimemkumbuka my beautiful chewbacca na style yake ya muharmusi fashion style
View attachment 1054150
  1. Watch Eulachacha Waikiki 2 Episode 1 online at Dramanice
hii taarifa nimeiona wakati ambao bando langu limebakia mb 350, pumbavu nitaitafuta magharibi ya leo inshaallah ep 1 pamoja na 2 kama itakuwa imeshawekwa subtitle na viki.

update:
episode 1 ya season 1 iliangaliwa kwa asilimia 1.7.
episode 1 ya season 2 imeangaliwa kwa asilimia 2.118.

tusisahau JTBC ni cable tv hivyo basi ni tofauti na mashirika ya umma kama vile MBC, KBS, SBS kwa kufuatiliwa, unaweza kukuta hata huko korea kuna watu ni mwendo wa TBC mchana kutwa.
Bogoshipseyo Sana Sana!

Kutoingia Kwako Umu Sana Kumenifanya Nami Nikufate!...
Natumai Umzima!!
 
Ahadi haikutimizwa watu walizunguka mji mzima mara waambiwe huku kuna ofa wakienda patupu mara hotel nyota tano zimepunguza bei wakati linaloitwa punguzo ndo bei halisi ya bia za mtaani

Tupo pamoja kwenye soka la Afrika nipo mbali nalo kabisa,mpira hakuna zaidi ya siasa za kujuana
😛😛😛😛 duh!
kumbe ahadi yenyewe ilimuhusu zaidi pierre mzee wa liquids.?
na watu wa upande wa pili wanavyopenda kunywa nadhani matajiri wote wanaofanya biashara ya ulevi wangelifilisika.
  • zenji ukitembea mita 150 unakutana na msikiti usiokuwa na waumini lakini bara ukitembea wastani wa mita 150 unakutana na bar iliojaa wanywaji.
starehe ni gharama na kila mtu ana uhuru wa kuchagua akipendacho, hapo ndipo ninapovutiwa na mifumo ya utawala ilioasisiwa na mabeberu.​
 
Hizi zinapendwa sababu zina visa na mikasa ya kueleweka ndani ya familia za jamii husika
upo sahihi familia ni kama maji safi ambayo huwezi kuyaepuka kimatumizi, baadhi ya wakati unatamani uwe mbali na familia yako kwa kigezo cha kutaka uhuru at the end unajikuta unatamani tena kurudisha ukaribu na wanafamilia wenzako.

hii dhana ya familia inaonekana wakorea wameifahamu zaidi ndio maana wanapendelea kuangalia drama zenye maudhui hayo.
 
Hahaha kama kawaida, karibu kijiweni kwetu
kuna mwanadamu humu ndani atakuwa ameniroga, haiwezekani kila ninapofanya maamuzi ya kukimbia humu ndani nashindwa, naweza kuchukua siku 10 then shetani ananivuta kwa kasi ya 5G.

au inawezekana nimejiroga mwenyewe, hahahahahaaaa kuna tangazo fulani la mganga wa kienyeji nimelisoma nimecheka sana.
anatibu matatizo zaidi ya 30 ila kilichonivutia zaidi ni uwezo wake wa kumwezesha mvuvi avue samaki wengi kila siku.
shikamooo mganga yule kama kuvua ni rahisi si atafute dau ukavue.​
 
Hahaha umejiroga au aliyekuroga mganga wake fundi sana. Sasa mzee mganga yeye si anavua wengi kwa hiyo anataka akugawie na wewe uvue wengi
 
Hahaha umejiroga au aliyekuroga mganga wake fundi sana. Sasa mzee mganga yeye si anavua wengi kwa hiyo anataka akugawie na wewe uvue wengi
kwa mukhtadha huo unaamini ya kwamba waganga wote wana nguvu za kiume?
kama kuvua rahisi dada yangu si angelitafuta boti akavue kwa kutumia dawa zake?
nilichojifunza waganga wote hawana roho mbaya linapokuja suala la kusaidiana, yupo tayari apoteze yeye lakini mteja wake afanikiwe.
binadamu wote tungeliiga tabia za waganga basi matatizo ya kibindamu yangelipungua.
waganga oyeeeee
 
😁😁😁
 
[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom