Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kifo cha Ha muji kwangu ilikuwa pigo mno baada ya kumpoteza Sagalhyeon,na Yeol salta.
Wewe ulivyotazama kifo cha nani kiliugusa kwa undani zaidi moyo wa mfalme?!
Hay ndiyo maono yangu walipokufa mfalme aliumia sana.
1. Princess[ Dam Ju]
2. Damang [ Prince )
3. Queen( mama yake)
4. Ha muji[ Military Advisor ]
5. Sagal hyeon[ Emperor's Bodyguard ]
6. Yeon salta( General )
Hakuumia sana mfalme alipokufa
Mimi naona kifo kilichomgusa zaidi kuliko vyote ni Dammang kaka yake pamoja na Ha Muji. Kama nipo sahihi vifo hivi ndio nilimuona akitokwa na machozi...

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hii Drama Niliicheki Kitambo Kidogo Ila Bado Naikumbuka Vyema. Kuna Vifo Vingi Ambavyo Viligusa Mioyo. Kuna Kifo Kimoja Hapo Kimesahaulika Cha General Mzee, General Komu.

Kifo Cha Huyu Mzee Kilinisikitisha Sana Ukizingatia Ndiye Alikuwa Generali Mbobevu Wa Vita Na Ndiye Aliyewalea Akina Damdeok Wakiwa Wadogo Ikiwemo Kuwafundisha Mbinu Nyingi Tu Za Kijeshi Na Mapigano.

Mchango Wake Hauwezi Kusaulika Katika Maisha Ya Damdeok Kwa Ujumla Na Hata Alipokufa, Alikufa Kifo Cha kishujaa Sana Wakati Anaitetea Ngome Isiyoingilika (Impregnable Fortress) Yodongseong. Alikuwa Loyal Sana Kwa Taifa La Goguryeo Na Alipigana Vita Nyingi Sana Kiasi Cha Kuathiri Afya Yake.
 
Kweli kabisa tumemsahau Camander Komu mzalendo wa kweli katika Taifa lake mtu ambaye alikuwa anaijali Gogryeo kuliko hata familia yake, Nakumbuka alipokuwa anakwenda kupigana na Murong Choi huku akiwa na hali mbaya Kiafya,Nadhani Chanzo cha kifo Murong Choi ilikuwa ni kupigana na Camander Komu ama mmiliki wa Ngome ya Yodoseong.
 
ㅋㅋㅋㅋㅋ ㅋㅋㅋㅋㅋ
nimependa mwanzoni walipokuwa sokoni akiambatana na mfanyakazi wake alimuuliza unadhani fedha zinazaliwa wapi?
dogo akajibu benki kuu, kutoka kwa matajiri na sekta nyenginezo za kifedha.

kwa kutumia lafudhi ya Gongju akamjibu
wazalishaji wakubwa wa fedha ni hao walalahoi unaowazarau, kadri wanavyofanya kazi kwa amani na furaha inayotokana na mzunguko mkubwa wa kifedha ndipo matajiri nao wanapata fedha ya kuendeshea biashara zao.

ile hotuba siku aliyotambulisha kwenye mkutano wa shareholders nimeipenda, [emoji120][emoji120] amekichafua vibaya sana,
nchi yetu ni masikini utanunuaje ndege zaidi 4, hivi kuna atakayeamini kama sisi ni masikini?

nimenusa harufu ya vita kubwa sana ya kimaslahi kati ya upande wa rais wa benki bwana Kang Sam-Do dhidi ya wale wanaotaka kumn'goa madarakani, kama namuona proffessor wetu assad No Dae-Ho atakavyokinukisha.

duniani imekuwa ni rahisi sana kwa masikini kuwatajirisha matajiri kuliko matajiri kuwatajirisha masikini, kama kuna baadhi ya nchi kiwango cha matajiri ni kikubw kuliko kiwango cha umasikini lakini bado masikini wameendelea kuwepo vipi kwa huku kwetu?​
bado elimu ya utumiaji wa huduma za kibenki ni ndogo sana kwa wananchi, wengi wao wanaotumia benki ni wale waajiriwa au wafanya biashara wakubwa na kwa kiasi kikubwa hutumia huduma za kibenki kwa dhumuni la kutoa mishahara yao ya kila mwezi, ukiangalia drama hii kwa umakini utagundua hata wale wauza mboga mboga sokoni wana saving account.

Kuna raia mpaka leo wameshindwa kuwa na imani na huduma za kuhifadhi na kuhamisha fedha kwa njia za mitandao ya simu.
Afrika tupo nyuma sana​

Aigoooooo
Mimi nimeipenda pale inapoanza yule mzee anapolalamika juu ya lile ‘dude’ lililokuwa linamtesa hahaaaaa
Mimi nilidhani jambazi hatari au nini kumbe pig? Nilichekaaaaaaa

Nimependa caring ya Uncle Noh, ule msigano mule ndio raha yenyewe ya drama ilipo, ila ni wazi Auditor Noh na Mr. President wataishinda ile vita... sema watastruggle sana, wale wajinga nao wana backup ya wahuni wenzao.

Dogo kanichekesha alivyojiongeza kwa akawa detective, sio kwa kumfuata kule yule tapeli mpaka home. Mwanzoni nilitamani Uncle Noh amchukue waende wote Seoul ila sasa naona bora abaki tu awe anampa info za kule ‘home town’.

Wenzetu wako mbele sana kwakweli, ona watu wanavyojiongeza na maproject, wazee bado wanajishughulisha tena kwenye kilimo cha kisasa na hata wafanyabiashara wadogowadogo wana uelewa mkubwa na masuala ya kibenki.

Jambo pekee walilonidisappoint ni yale mambo yao ya kutaka kujirusha kwenye majengo marefu, na always huwa wanaokolewa, woiiiiiiiiii.
Wakorea wanapenda hizo scene sana, mijini wanajirusha kwenye maghorofa vijijini wanajirusha kwenye kingo ndefu za mito, bora kwenye historical huwa wanajirusha kweli.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hii Drama Niliicheki Kitambo Kidogo Ila Bado Naikumbuka Vyema. Kuna Vifo Vingi Ambavyo Viligusa Mioyo. Kuna Kifo Kimoja Hapo Kimesahaulika Cha General Mzee, General Komu.

Kifo Cha Huyu Mzee Kilinisikitisha Sana Ukizingatia Ndiye Alikuwa Generali Mbobevu Wa Vita Na Ndiye Aliyewalea Akina Damdeok Wakiwa Wadogo Ikiwemo Kuwafundisha Mbinu Nyingi Tu Za Kijeshi Na Mapigano.

Mchango Wake Hauwezi Kusaulika Katika Maisha Ya Damdeok Kwa Ujumla Na Hata Alipokufa, Alikufa Kifo Cha kishujaa Sana Wakati Anaitetea Ngome Isiyoingilika (Impregnable Fortress) Yodongseong. Alikuwa Loyal Sana Kwa Taifa La Goguryeo Na Alipigana Vita Nyingi Sana Kiasi Cha Kuathiri Afya Yake.

Bora umetukumbusha General Komu. Alikuwa general wa ukweli sana na mzalendo wa ukweli, aliplay part kubwa sana na bora alikufa mapema maana angemfunika hata Damdeok kama mzee Geumwa alivyoleta shida kwenye Jumong.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kweli kabisa tumemsahau Camander Komu mzalendo wa kweli katika Taifa lake mtu ambaye alikuwa anaijali Gogryeo kuliko hata familia yake, Nakumbuka alipokuwa anakwenda kupigana na Murong Choi huku akiwa na hali mbaya Kiafya,Nadhani Chanzo cha kifo Murong Choi ilikuwa ni kupigana na Camander Komu ama mmiliki wa Ngome ya Yodoseong.

Hapana, kifo cha Murong Chui kilitokana na jeraha alilolipata wakati anapigana na Damdeok.
Nafikiri ulitaka kusema kifo cha General Komu kilichangiwa na kupigana na Emperor Chui, japo afya yake ilikuwa imezorota tayari.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyo Empress Ki Ni Drama Ya Aina Yake. Ni Drama Yenye Sad Ending Na Kama Wewe Si Mpenzi Wa Sad Endings Basi Hutoifurahia.

Hii Drama Ilikuwa Controversial China Sababu Ya Baadhi Ya Mambo Ambayo Hayakuwa Na Uhalisia Ndani Yake. Inasemekana Empress Ki Alikuwa Katili Sana Na Alikuwa Na Maovu Kibao Ila Kwenye Hii Drama Amekuwa Portrayed Kama Mtu Mwema, Jasiri Na Mvumilivu Kitu Ambacho Wanahistoria Wanakataa.
dah hii drama ya empress ki niliishia episode 11.
mkuu kwani ni china au korea?

kwa mujibu wa stori ila sina uhakika ni kwamba jamii ya wakorea wengi wao hawavutiwi na historia ya empress ki kutokana na mambo aliyoyafanya wakati alipokuwa na cheo kwenye serikali ya YUAN (mongolia).

Mongolia waliivamia goryeo kwenye vita iliodumu kwa miaka 30 na kufanikiwa kuyachukua maeneo mengi ya kaskazini na kuyafanya himaya yao kwa takribani miaka 80.

kitendo cha kuwapa madaraka jamaa zake kwenye serikali ya yuan kilileta athari kubwa sana kwa serikali ya goryeo kwa sababu ilifika wakati kabila lao ndio lilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi kwenye serikali ya goryeo kwa kutumia nguvu ya yuan dynasty.

kaka yake aliwahi kufanya jaribio la kutaka kumuondoa madarakani mfalme lakini jaribio hilo lilishindikana na mfalme kuamua kulipa kisasi kwa kuangamiza koo ya GI.

empress ki akaamua kutuma wanajeshi wa mongolia ili wamuondoe madarakani mfalme gong min ambaye kwenye utawala wake alifanya jitihada kubwa sana ili kuinusuru goryeo isiendelee kutawaliwa na mongolia ila kabla ya jeshi halijafika korea wanajeshi watiifu waliwazuia mongolia kwenye border ya goryeo.

empress ki alitumia nguvu yake ili kuifanya familia yake iwe na nguvu ya utawala kwenye nchi ya goryeo kwa kutumia nguvu za utawala wa mongolia.

nakumbuka aminas aliwahi kuandika hadithi yake humu ndani.
 
Attachments

  • 1554061627262.png
    1554061627262.png
    74.5 KB · Views: 30
View attachment 1059726
hahahahahaaaa nimecheka sehemu hii wazee walipoona dalili za kugeuziwa kibao wacha wakinukishe.

Hahaaaaa vizee vinachamba hatari, sio kwa kumsema kule dada wa watu kwamba anajidai kisa katoka mjini kumbe ana stress za kukosa mkopo!

Sasa itaendelea lini? Kila saa nachungulia! Ndio maana sipendi haya mambo ya ongoing.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hahaaaaa vizee vinachamba hatari, sio kwa kumsema kule dada wa watu kwamba anajidai kisa katoka mjini kumbe ana stress za kukosa mkopo!

Sasa itaendelea lini? Kila saa nachungulia! Ndio maana sipendi haya mambo ya ongoing.

Sent from my iPhone using JamiiForums
jumatano na alhamisi.
hahahahaaaaaaa utanitoa roho yangu kwa kucheka.
 
jumatano na alhamisi.
hahahahaaaaaaa utanitoa roho yangu kwa kucheka.

Hahaaaaa jana nimechekaaaaaa. Ila mke wake na Uncle Noh sio kabisa, ndio nini kudivorce na mwenzie kisa baba yake kajinyonga kwa kukosa mkopo?

Tunapoelekea nahisi kutakuwa na mapigano makali sana ya kutumia silaha, ndio lengo la kumuonesha Uncle Noh kama sniper hatari aliyeshinda medali.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
jumatano na alhamisi.
hahahahaaaaaaa utanitoa roho yangu kwa kucheka.
Kwahiyo siku hizi Historical Drama hazipandi sana?!, Miye bado Naisaka historia vizuri halafu nijue kama narudi mjini au laa!, Ingawa Jumong ndiye aliyenikaribisha Korea miaka ile 2007/2008 nikiwa primary baadae nikaishuhudia 2009 Capital 2010 nikaishuhudia ikiwa imetiwa maneno ya kiswahili, nikaja Queen Seon deok, The Great King, ndiyo tukahamia mjini kwa mara ya kwanza. Hii ni list ya drama za mjini nilizowahi kuzitazama:
Iris, A man Called God, Lobbyist ,Crime Squad , Bodyguard ,Time btn Dog n wolf ,
the President ,Fugitive Plan B,Gold Cross,K2, Ghost Agent ,Swallow of the Sun, City Hunter,Good Doctor, The Promise,
TEMPTATIONS OF ANGEL, morin School. Nadhani hizo kama kuna ambazo nimesahau hazifiki 7 ila kwenye historical hapa kuna mvua.
Japo nilikuwa nakoshwa na JamesBong wa kwenye plan B jamaa ana vituko huyo?!
 
zamani zilikuwa zinanishinda lakini tokea niingie ulimwengu wa going on nimeshakuwa muathirika zaidi ya piere na pombe, makonda na madaraka,

DRAMASIKUNO: OF EPISODEMAUDHUI
haechi drama
jumatatu + jumanne​
48/2 = 24 episode​
historical
item drama jumatatu + jumanne
32/2 = 16 episode​
super natural
waikiki season 2 jumatatu + jumanne 16 episodecomedy
doctor prisoner jumatano + alhamisi 16 episodemedical
the banker drama jumatano + alhamisi 36/2 = 18 episodefinance
the fiery priest drama ijumaa + jumamosi 40/2 = 20 episodeaction, comedy, religion
kill it drama jumamosi + jumapili 16 episodeaction, criminal
confession drama jumamosi + jumapili 16 episodelaw, criminal
chicago typewriter drama completed 16 episode

kuna baadhi ya drama zitatumbuliwa muda si mrefu, kuna baadhi ya drama zitaingia kwenye list.
Sawa nitajisajiri huko wacha ni mtazame kwanza Jang yeong sil halafu baadaye nije.
 
drama zinazoangazia three kingdom kwa kiasi kikubwa nimeshaziangalia na nyengine niliachana nazo kwa sababu hazikunivutia.
korea proejct nyingi wanazotengeneza miaka hii ya karibuni ni modern drama pamoja na drama za joseon dynasty.
  1. prince of the legend (jumong)
  2. kingdom of the wind
  3. kings dream / dreams of emperor
  4. emperor of the sea/ haeshin
  5. dae jo yeong
  6. emperor wang guhn : sijaimaliza ina episode 200
  7. sword and flower:
  8. shine or go crazy
  9. scarlet heart ryeo
  10. hwarang
  11. queen seondeok
  12. faith
  13. gwanggaeto
  14. gye baek
  15. king geunchogo
  16. the king in love
  17. god of war
  18. jung do jeon
  19. six flying dragons
  20. empress cheonchu: sijaimaliza
usiku mwema kwa wote, macho yangu yameshachoka.
anyeong chingus
Rrrryeyyy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaaaa jana nimechekaaaaaa. Ila mke wake na Uncle Noh sio kabisa, ndio nini kudivorce na mwenzie kisa baba yake kajinyonga kwa kukosa mkopo?

Tunapoelekea nahisi kutakuwa na mapigano makali sana ya kutumia silaha, ndio lengo la kumuonesha Uncle Noh kama sniper hatari aliyeshinda medali.
Sent from my iPhone using JamiiForums
upo sahihi, hayakuwa maamuzi sahihi kiupande fulani labda alichukua maamuzi kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya kumpoteza baba yake aliyeamua kukatisha uhai wake kutokana na depression. laiti kama wanadamu tungelikuwa na uwezo wa kutabiri kitakachojiri mbeleni kwa usahihi basi mke wake angelikuwa na haki ya kudai talaka kwa mume wake kwa kushindwa kwake kuzuia kifo cha mkwe wake.

taarifa ya habari ilielezea tukio lililoitikisa dunia kiuchumi baada ya taasisi kubwa ya kifedha ya lehman brother iliopo marekani kufilisika, sio tu marekani hata soko la hisa linalopatikana london pia lilikumbwa na athari bila ya kusahau nchi za Asia nazo zilikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi ikiwemo japan.

mtikisiko wa uchumi ulioikumbuka ulaya na marekani ndio ulipelekea taasisi nyingi za kifedha nchini korea zikiwemo benki za biashara kukumbwa na athari ndio maana mzee alishindwa kupata msaada kwa muda muafaka kutoka benki.

hivyo basi hata mimi sijaliona kosa la mzee noh kwa sababu yeye si aliyepelekea dunia kukumbwa na mtikisiko wa kiuchumi mnamo mwaka 2008.

ni matumaini yangu kabla ya kufariki dunia kwa mwanamama ambaye kwa sasa ni mgonjwa atarudisha tena moyo wake kwa bwana assad wa the banker drama.
sidhani kama ndani ya dunia hii tunayoishi wanafika angalau wanaume 100 ambao wako tayari kuwasaidia kifedha wanawake ambao walikwisha kuachana pindi wanapokutwa au kukumbwa na mitihani ikiwemo maradhi, auditor noh nafsi yake imejawa na ubinadamu uliovuka mipaka.
 
Damushin “Sound Of Winter”

Hii Nyimbo! Dooh!
Park Hyo Shin announcing that his 20th anniversary solo concert will take place this coming June

collaborations kati ya the king of ballad park hyo shin na composer jung jae il inakufanya usahau machungu yote ya kukosa top 4.
achana na mafundi wengine wa piano kama vile yiruma huyu jung jae il ni balaa na wameanza kufanya kazi kwa pamoja kuanzia wild flower nyakati hizo wanatoka jeshini, mwanzoni inasemekana jamaaa alimkatalia park hyo shin kufanya kazi pamoja kwa sababu alihofia park atafeli.

naweza kufuta nyimbo za waimbaji wote ila si gwiji park hyo shin, nimeshakuwa mgonjwa wa sauti yake..
 
Back
Top Bottom