chukua assignment nyengine itakayokusaidia kufikisha angalau alama 16 za kufanyia mtihani wa mwisho.
AGE OF WARRIORS DRAMA
kwa taarifa zilizothibitishwa na
daemusin bin makinikiyya bin koroshow bin vipigo kwa shangazi zenu ni kwamba ndani ya drama hii hamuna muigizaji mwenye sura ya mvuto haijalishi ni mwanamke.
🙂 🙂 😛 😛 .
hii drama episode 11 za mwanzoni ni mwendo wa kuchinjana kwa mapanga, shoka, iron ball n.k,
View attachment 1111637
kwa nini ikaitwa age of warriors?
kutoka mwaka 1170 hadi mwaka 1270 taifa la goryeo lilijikuta likiendeshwa kwa nguvu za kijeshi (goryeo millitary regime).
walikuwepo watemi watatu wakiongozwa na
yi ui bang ambao ndio waliongoza mapinduzi ya kumuondoa mfalme aliyechaguliwa kwa nguvu za wananchi anayeitwa Uijong na hatimaye wakamweka madarakani mdogo wake aliyeitwa Myeongjong.
kwa takribani miaka 100 goryeo ilijikuta ikiendeshwa kwa njia hiyo, mfalme anakuwepo kama kawaida lakini nguvu ya kimaamuzi inabaki kwa mwanajeshi aliye na nguvu pamoja na ukoo wake.
kwa ufupi ilikuwa ni mwendo wa kupinduana mwanzo mwisho, si unajua nyakati hizo kila mwenye nguvu alikuwa na jeshi lake.
ujinga huu uliisha baada ya goryeo kukaliwa kimabavu na MONGOLIA.
yi ui bang na wenzake waliongoza mapinduzi na kumweka madarakani mfalme myeongjong
baadae siku za mbeleni mnamo mwaka 1174 jeong jung bu ambaye pia alishiriki mapinduzi ya mwanzo pamoja na yi ui bang alimuondoa madarakani mwenzake na kutoa amri ya kunyongwa kwa general yi ui bang (hakuna rafiki wa kudumu kwenye madaraka),
mwaka 1179 general gyeong dae seung ikawa ni zamu yake kutamba, huyu alimuondoa madarakani jeong jung bu huku akitoa amri ya kunyongwa kwa familia nzima ya general jeong bung ju (karma is bitch).huyu jamaa yeye akataka kurudisha serikali itakayoongozwa kwa sauti za wananchi lakini ikashindikana
mnamo mwaka 1183 nguvu za utawala zikahamia kwa yi ui min baada ya kifo cha gyeong.
mfumo wa utawala ukaendelea hivyo hivyo kwa miaka mingi sana mpaka kuuliwa kwa Kim Jun (ukiangalia god of war drama imejaribu kuzungumzia maisha yake kutoka kuwa mtumwa hadi kuwa kiongozi mwenye nguvu wa goryeo).
kifo chake kilipelekea madaraka yarithiwe na kiongozi mwengine lakini hakudumu sana kwa sababu goryeo ilijikuta ikiwa chini ya himaya ya mongolia kwa miaka takribani 80.
ukifuatilia hali ilivyokuwa utagundua ya kwamba goryeo karne ya mwishoni ilikuwa inapumulia mashine kwa sababu royal family (wang clan) walikosa nguvu na ushawishi mbele ya koo nyengine zenye nguvu
View attachment 1111639
bado namtafuta hand some boy mtoto mwenye sura nyepesi kama makonda.
drama ime contained episode 158
This drama is set in a tumultuous time in Korean history, where warriors led by Jung Joong Bu, Lee Ui Bang, Lee Go and Chae Won rose in rebellion against King Ui Jong of Goryeo and his government, dominated by scholars and ministers, with the aim of ... at Dramanice
www2.ondramanice.tv