BLACK DOG
Kwa ambaye bado hujaanza kuifuatilia Project hii ama ndiyo umeanza hivi sasa, nakukaribisha sana!
Hii ni Project ambayo kidogo imetanguliza simanzi machoni petu sisi watazamaji hususani pale ambapo muhusika wetu mkuu aliponusurika kifo katika ajali mbaya ya basi katika kipindi cha maisha yake ya utotoni.
Mbaya zaidi, kitendo cha binti huyu mdogo,
Haneul kuokolewa katika ile ajali mbaya, kunasababisha kupotea kwa maisha ya mtu mwingine aliyejitolea kama sadaka kumuokoa Haneul. Si mwingine bali ni mwalimu Young Ha aliyekufa katika ajali hiyo baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika basi hilo lililoanguka.
Maisha yanazidi kuwa magumu hususani kwa familia ya mwalimu Young Ha aliyekufa katika ile ajali.
Hiyo ni baada ya wafiwa kutokabidhiwa kiasi chochote cha fedha kama fidia kutokana na kifo cha mwalimu huyo na hilo ni kwa sababu, kisheria, mwalimu huyo hakuwa muajiriwa rasmi katika shule hiyo, yaani alikuwa ni mwalimu wa muda mfupi (short-term).
Sheria hiyo inazua mgogoro mkubwa sana katikati ya shughuli za msiba kati ya wafiwa na bodi ya wasimamizi katika shule ambayo Bw. Young Ha alikuwa akifanyia kazi.
Nisimalize uhondo. Hiyo ni kwa ufupi tu kuhusiana na matukio machache ambayo kwa namna moja ama nyingine yameleta simanzi machoni petu kama watazamaji hususani mwanzoni kabisa mwa Drama yetu ya Black Dog.
Changamoto ni nyingi bila kusahau 'Visa' vya hapa na pale.
Karibu sana tuendelee kuifuatilia!