Innocent defendant adui na stering wanajulikana tangu mwanzo. Na tangu mwanzo adui ni bata tu kila akifanyacho anafanikiwa huku stering akiteseka weeee. Innocent ddefendant hadi episode za kati kati fumbo limeshafunguka. Na mwenye akili za haraka haraka baada ya mauaji ya mke wa defendant,muuaji alishajulikana vizuri tu
Vagabond haitabiriki,umdhaniae ni adui kumbe sio na umdhaniae ni mtu mwema kumbe adui. Vagabond hadi inaisha fumbo halijafunguka
Kutoroka gerezani kwa innocent defendant ni kwa uzembe wa askari gereza au tuseme maigizo yalizidi,defendant wakati anakimbizwa na polisi akawapoteza kidogo kisha akakutana na gari la wenzie wakapisha na polisi huku hawajazima taa ndani ya gari,askari wazembe tu wanaweza pitwa na tukio kama hilo.
Vagabond ina mbio za magari kutoka bandarin hadi karibu na mahakama. Wakati innocent ina mbio za miguu kutoka gerezani hadi uraiani.