Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Jamani naombeni mnisaidie ni app gani nzuri ninayoweza kuwa natazama korean drama,maana nshahangaika bila majibu,hasa hasa naitaka drama ya emperor of the sea na iljimae

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..[emoji382]
 
Niko Episode ya 17 Hii "SHIN DON" sio mchezo, naona Empress KI anayomuenda Gongmin na Goryeo.
ila Huyu Mfalme Gongmin bado alikuwa mdhaifu kwelikweli.
Nadhani hizi zama za Gongmin ndio za Ambazo Waliishi kina Sambong, Choi Young & Yi Songgye.
Yote kwa Yote Wa-Goryeo walikuwa mashujaa sana kuliko wa-Joseon, huwa nawaza kwa jinsi wa-choseon walivyodhaifu wasingeweza kupata uhuru kutoka kwa Wa-Mongolia.
 
mapenzi yalizidi kumtia msongo wa mawazo na tatizo la akili baada ya kifo cha malikia noguk (binti kutoka mongolia).....licha ya kwamba bidada alikuwa ni mwana wa mfalme kutoka mongolia (yuan dynasty) lakini aliipa heshima na kuichukulia goryeo pamoja na vizazi viliyomo ndani ya nchi hiyo kuwa na haki sawa na yuan dynasty ,

queen noguk alimsaidia kwa kiasi kikubwa sana kwenye kampeni yake ya kuirudisha goryeo kwenye njia ilio sahihi (kwa kuwaondoa pro mongolia wakiongozwa na ukoo wa empress ki).

ukaribu wake kimahusiano na malikia noguk ulipelekea jamaa akatae kuongeza mke wa pili licha ya kushauriwa mara kwa mara na familia yake (walitaka afunge ndoa na mwanamke wa goryeo), sababu kubwa ilikuwa ni kushindwa kwake kupata mrithi wa madaraka kwa sababu ya kushindwa kuzaa kwa malikia noguk (huyu malikia baada ya kuhangaika kupata mtoto hatimaye baadae alikufa kwa tatizo hilo la uzazi, ilikuwa ni maumivu makubwa sana kwa gongmin).
----------------------------------------------------
ukirudisha kumbukumbu zako mpaka kufikia drama ya jeong do jeon, six flying dragons, greet seer unakutana tena na mwendelezo wa hadithi ya mfalme gongmin..

teh teh teh
jamaa alioa concubines lakini hakuwa na muda wa kutimiza wajibu wake (code nyepesi), hatimaye siku moja mfalme gongmin alijikuta akiuwawa na mlinzi fulani ambaye inasemekana alikuwa anatembea na mke wake.
-----------------------------------------------

maisha yote mshindi wa vita ndiye mwenye haki ya kuandika historia atakavyo,
kuna simulizi fulani inadai ya kwamba mtoto aliyezaa na concubine hakuwa wake bali alikuwa ni mtoto wa huyo monk shin don.

nukuu hiyo ni kwa mujibu wa drama ya jeong do jeon.

===============



kifo cha gongmin ilikuwa ndio mwanzo wa kuanguka kwa goryeo....

vita ya siasa ilianzia hapo pale yupo lee imin na timu yake, pale yupo general choi yeong, pale yupo kichwa kigumu sambong........na kule kuna simba mwenda kimya general yi song gye....... kuleee kuna mwanadamu aliyekunywa maji ya bendera ya goryeo bwana jeong mong jo a.k.a poun.............................................. na mwisho kuleeeeeee kuna mwendawazimu yi bang won na akili zake nyingi zilizofungamana na ukatili.

nitaitafuta tena hii project siku za mbeleni, nilifika episode 12
Huyo Queen Noguk alikuwa Smart mpaka raha, alikuwa mjasiri sana na Mshauri na mtu wa kumpa mfalme matumaini na kumtia moyo.
Miye mwenyewe nimempenda bure kwa ujasiri wake, Nadhani kama angeishi miaka mingi nadhani tusingeiona JOSEON( YI dynasty).

Hivi kwani Hamna Drama ya kumuhusu Mfalme JANG SU wa Gogryeo?
 
hata lile vugu vugu la kutengeneza project za three kingdom especially goguryeo limezimika kwa takribani muongo mmoja (decade), labda ni kwa sababu zile kelele za kila upande (korea na china) kujisifia umiliki wa historia ya goguryeo zimezimika kama mshumaa wa keki ya birthday.

miaka ile madirector wa korea walikuja na moto mkubwa sana (nadhani walikuwa wanawakomoa wachina)
jumong + dae jo yeong + yeon gae somun + the legend = zote hizi ndani ya mwaka mmoja


Writer Lee Hwan-kyung of "Yeongaesomun" openly stated that one of the reasons the drama was made was to counter China's claim over the history of Goguyreo.
Hahaha Wachina wasituchanganye, yaani King Gwanggaeto(Dam Doek) awe mchina!!, King Dongmyeong( Jumong)!!, Daemusin( Muyul)!! wasituzingue hao.
Basi hiyo Gogryeo haikuwa ya mchezo, mpaka wanagombania umiliki wa historia yake.

Lakini King Jang Su alikuwa ni mfalme mzuri, ni moja kati ya wafalme bora kabisa wa Gogryeo.
Ndiye mfalme aliyetawala miaka mingi zaidi, Karibu miaka 78 kwenye kiti cha enzi, aliyafaidi matunda ya baba yake King Gwanggaeto the Great.
yeye ndiye aliyeifupisha jina Gogryeo to Goryeo, na alihamisha makao makuu kitoka Gungnae-seong to Pyeongyang-seong.
 
father is strange nimeanza kuiangalia na nimefika episode 9 (nimeipakua mpaka episode 15).

FAMILY DRAMA
nimeangalia marry me now completed (hii bado haijapata mpinzani)
what happened to my family = nimefika episode 13
my golden life = niliangalia episode 1

hizi project unaweza kudhani zimeandikwa au kusimamiwa na mwanadamu mmoja, siyafahamu maisha ya wakorea ila kupitia drama hizo hapo juu nimejifunza au kugundua ya kwamba waandishi wote wanajaribu kuonyesha ya kwamba familia zenye kipato cha kawaida wanakuwa na maisha ya furaha, masikilizano, upendo na utiifu kuliko familia za mboga saba (chaebol family).
acha nipambane nayo
================================

hawa wahuni wawili vituko vyao vinalingana na familia ya kuleee ndani ya marry me now, hahahahaaaaaa
mama alifikiri chakula amepikiwa yeye, aigooo kumbe ni chakula cha paka
teh teh teh
huyu mzee ni kiboko ya uchafu
View attachment 1458311
View attachment 1458314

Hio marry me now itabidi niitafute naona inasifiwa sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
father is strange nimeanza kuiangalia na nimefika episode 9 (nimeipakua mpaka episode 15).

FAMILY DRAMA
nimeangalia marry me now completed (hii bado haijapata mpinzani)
what happened to my family = nimefika episode 13
my golden life = niliangalia episode 1

hizi project unaweza kudhani zimeandikwa au kusimamiwa na mwanadamu mmoja, siyafahamu maisha ya wakorea ila kupitia drama hizo hapo juu nimejifunza au kugundua ya kwamba waandishi wote wanajaribu kuonyesha ya kwamba familia zenye kipato cha kawaida wanakuwa na maisha ya furaha, masikilizano, upendo na utiifu kuliko familia za mboga saba (chaebol family).
acha nipambane nayo
================================

hawa wahuni wawili vituko vyao vinalingana na familia ya kuleee ndani ya marry me now, hahahahaaaaaa
mama alifikiri chakula amepikiwa yeye, aigooo kumbe ni chakula cha paka
teh teh teh
huyu mzee ni kiboko ya uchafu
View attachment 1458311
View attachment 1458314
Hakika Daemusin lkn pia wanatufundisha carrier za watu wa kawaida na nmna wanavyointeract
Pia suala la uhalisia na hisia tofauti na kwetu watu wanajibadili sauti, hakuna hisia wala harara ktk matendo ukiacha zilizotengenezwa na wageni kama Siri ya Mtungi,, Fatuma nk
Pia wanatufundisha tamaduni zao ni za namna gani nasi tunaweza ishi hivyo lkn tunaogopa au kudhauriana
Kulala watu wengi nyumba moja kwenye My Father is Strange pia inadhihirisha sio big deal ni uchoyo wetu tu kukaribisha watu
S korea seems people live simple but kama nchi wako mbali kimaendeleo

Suala la posho linaendelea pia yaani ukipitisha umri
wa kukaa nyumban lazma uchangie kama kodi kila mwezi na kama huna kazi wanakudistab mpaka upate

Golden sijaiangalia lkn naitafuta nikimaliza whisper na innocent Defendant

Vipi kuhusu king of amnbition
 
tawala za wachina walifanywa kitu mbaya sana na hao wahuni wa goguryeo kwa nyakati tofauti.....

nyakati fulani za utawala wa sui dynasty (kabla ya kuja tang dynasty) waliivamia goguryeo wakiwa na jeshi linalokadiriwa kufikia millioni 1......

ulikuwepo mzimu mmoja unaitwa general eulji mundeok.
mwanaume alimtumia shairi lifuatalo general wa nchi ya sui

Your divine plans have plumbed the heavens; Your subtle reckoning has spanned the earth;
You win every battle, your military merit is great; Why then not be content and stop the war?

kilichotokezea wachina tambi walifanyiwa ambush ya kinyama na huyo mwendawazimu
Duh! kweli hao Gogryeo walikuwa Wanaume.
ilikuwa miaka 700 ya kiume.
 
Back
Top Bottom