Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

images (1).jpeg

Hatimaye nimeimaliza " MONEY GAME " hii drama kwangu imekuwa kama shule, nimejifunza sana jinsi mambo yanavyofanyika huko na wakubwa hasa wataalam wa uchumi. kama umesoma uchumi nadhani hii Drama inakufaa sana..
Mbali na hayo, Hii drama wahusika wake ni wabobezi kweli kweli. yaani inafika sehemu akili inasahau kama ungalia drama, maaana wanavaa sana uhusika, huwezi kuamini kama wanaigiza. Jamaa wanajua mambo ya uchumi kuliko hata wataalam wetu huku wa uchumi.

yote kwa yote, hii Drama buana!!, Yaani inawanywaji wa pombe ( Soju, n.k) kuliko zote nilizowahi kuziona, yani hao watumishi wa umma baada ya kazi jioni lazima wajipongeze kwa pombe, asubuhi kabla ya kazi wanapiga supu safi. kifupi humu ndani mambo ya misosi na vinywaji sio haba.
kama nakuona Dae kwa mbaali.
 
wakorea wameanza ufala

secret forest (stranger) :
production team responded that there is a possibility the drama will produce season 3, they will set a schedule to discuss it.
=====
kwa next year sidhani kama itawezekana.

  1. cho seung woo kwa sasa yuko bize na shooting, project yake mpya ameshirikiana park shin hye na itaanza kuonekana mwaka ujao. Baada ya hapo maybe anaweza kurudi upande wa musical acting
  2. bae dona project ijayo itaonekana netflix akiwa sambamba na gong yoo (sina uhakika kama wameshaanza shooting)....mara paap kingdom season 4

tvN watumalizie kwanza arthdal chronicles
Kwa kweli hatujasahau kuhusu arthdal...kuna mtu nilimpa anavyosumbua Sasa mi nafanya kuomba hela ya bundle nione kama tayar Kumbe nashusha midude mingine
 
View attachment 1592221

Hatimaye nimeimaliza " MONEY GAME " hii drama kwangu imekuwa kama shule, nimejifunza sana jinsi mambo yanavyofanyika huko na wakubwa hasa wataalam wa uchumi. kama umesoma uchumi nadhani hii Drama inakufaa sana..
Mbali na hayo, Hii drama wahusika wake ni wabobezi kweli kweli. yaani inafika sehemu akili inasahau kama ungalia drama, maaana wanavaa sana uhusika, huwezi kuamini kama wanaigiza. Jamaa wanajua mambo ya uchumi kuliko hata wataalam wetu huku wa uchumi.

yote kwa yote, hii Drama buana!!, Yaani inawanywaji wa pombe ( Soju, n.k) kuliko zote nilizowahi kuziona, yani hao watumishi wa umma baada ya kazi jioni lazima wajipongeze kwa pombe, asubuhi kabla ya kazi wanapiga supu safi. kifupi humu ndani mambo ya misosi na vinywaji sio haba.
kama nakuona Dae kwa mbaali.
Kwa kweli money game mi pia nilienjoy sana, japo sio mtu wa uchumi lakin nlipata darasa mambo yanavyoenda
 
Hong gil dong,
Warrior Baek dong su,
Princess Iron ( Empress Chunchu),
King Gwanggaeto the Great Conqueror,
God of war,
Bridal Mask,
Inspiring Generation.
anza na hizo kwanza
Hiyo hong gil dong ni hatari naipatia site gan nidownload
 
Namba 4 😂😂😂😂😂. Pia Healer nzuri sana
genre ya THRILLER&ROMANCE kwa muda mmoja
labda kwa ninazozikumbuka haraka haraka
  1. IRIS 1 = kim hyun jun (lee byung hun) ni special agent kutoka shirika la NSS anayefanikiwa kufichua uharamia unaotendwa na kundi lenye nguvu kisiasa, kijamii, kibiashara linaloitwa IRIS
  2. IRIS 2 = mwendelezo wake baada ya kifo cha special agent kim hyun jun (aliuliwa na wauaji kutoka kundi la IRIS). nafasi ya lee byung hun ikazibwa na jang hyuk
  3. athena goddess of war: sijui niseme ni muendelezo au upande wa pili wa IRIS, ila nayo ni nzuri sana, nayo bajeti yake ilikuwa ni kubwa sana na pia lead actor ana ushawishi sana kwa sanaa ya korea hususani upande wa movies anaitwa jung sung woong (ana miaka 47 na wala hana stress ya ndoa, kwa nini dae nifunge ndoa)
  4. city hunter = stering ni mrembo kuliko mwanamke wake (halafu anavaa suruali mlegezo, sijui kama anaweza kubeba matofali yule fala)
  5. vagabond = ni nzuri sana
  6. W- Two Worlds = nzuri sana
  7. yongpal
  8. Memories of Alambara = ulimwengu wa game
  9. healer = sijawahi kuiangalia (no comment)
  10. come and hug me = sijawahi kuiangalia (no comment)
 
The Gentlemen of Wolgyesu Tailor Shop drama:

lee man sool na falsafa yake:
kwenye hii drama vazi la suit limetumika kama ni alama ya utambulisho wa heshima, nidhamu, haiba yenye kuambatana na Ihsani pamoja na msimamo imara wa mwanaume kwenye kuitafuta furaha ya maisha yake ya kila siku.
mzee lee man sool ametufikishia falsafa hii ya kuitafuta furaha ya nafsi kwa njia ya ushoni (si lazima tumuige mzee lee man sool njia yake bali kina mtu anapaswa abuni au aitafute njia yake itakayompatia furaha ya nafsi pasina kuvunja misingi ya kimaadili hususani ya ubindamu)

msuguano wa kifikra (digital vs analog):
Dong-Jin aliamini tailorshop ni biashara isiopaswa kuendelezwa tena na familia baada ya kudumu kwa takribani miaka 100 (aliamini ya kwamba imeshapitwa na wakati (nani atakayeshona suti kwa fundi makoleo haliyakuwa maduka ya kununulia suti yamejaa tele).....uzuri hii drama iliendelea kutuonyesha the nostalgic and wistful charms ya biashara hii ya ushoni ilioudumu kwa takribani miaka 100. Ndipo hapo tunapopaswa kujiuliza swali
kwenye ulimwengu huu wa digital (modernity), is tradition still relevant?

The bespoke suit (suit za kutengeneza kwa mkono) ni alama kuu ya analog iliotumika humu ndani inayounganisha dhamira kuu ya kuitafuta furaha ya nafsi kupitia njia ya utamaduni zaidi kuliko njia ya kisasa (binadamu anatengeneza suit na suit inamtengeneza mwanadamu mwenye heshima, mwenye kuheshimu muda, mtiifu na mwenye huruma kwa wenzake bila ya kuangalia ni kwa kiwango gani cha mali kinachopatikana kupitia kazi ya mikono na jasho lake). The bespoke suit ni alama kuu ya analog (kumbe bado kuna umuhimu wa kuvithamini vya zamani)

Lee man sool na ukumbusho bora kwa mwanawe (lee dong jin):
ukiangalia mtiririko mzima wa maisha ya Dong jin tulioonyeshwa kwa takribani episode 54 za drama hii yamefupishwa kwenye nukuu hii ya baba yake.
kwa sasa nimeshakuwa mtu mzima (binadamu mwenye umri mkubwa), kwenye maisha yangu nimejifunza ya kwamba pindi utakapokaa mbali na tamaa za kiulimwengu ndipo hapo utakapofanikiwa kulifahamu dhumuni kuu la maisha yako. ninachohitaji kutoka kwako ni kukuona unathamini na kuridhika na hata kile kidogo ulichonacho, usisahau kwenye maisha chochote kinachopanda juu (iwe ni mali, furaha) basi kuna siku kitashuka chini (hakuna kitakachobaki juu miele)

ukubwa wa pua si wingi wa kamasi
meesa company (chaebol) na laurel tailor shop (wolgyesu tailor shop) wote ni wazalishaji wa suti ila wana tofautiana kwenye filosophy nzima ya uzalishaji na mauzo ya bidhaa hiyo na hapo ndipo unapozaliwa mgongano wa kimaslahi na kiutu ndani ya drama.
meesa corporation kwa upande wao suti ni kazi ya sanaa, laurel shop kwa upande wao suti ni kazi inayohitaji ubunifu( ubunifu ndio huzalisa form of art).

Hyo sang hakuwawekea heshima kubwa wolgyesu(aliamini biashara yao itabaki kwenye ule ule wa Mom-and-pop stores).
hata leo hii nje ya drama mabadiliko ya teknolojia na utandawazi yamepelekea anguko kubwa sana kwa biashara ndogo zinazoendeshwa kwa msingi wa familia jambo amabalo pia limeleta athari kuu ya utengano wa kimatabaka, msingi mkuu wa mgawanyiko huu wa matabaka umechangiwa zaidi na kule kutofautiana kwa falsafa za uendeshaji wa biashara kati ya corporation na Mom-and-pop stores kwa kuanzia uzalishazi, usambazaji hadi mauzo ya bidhaa.

in reality it may seem that washonaji nguo kwa njia ya mkono na wale wazalishaji wakuu kupitia mashirika makubwa kwa sasa wanategemea masoko tofauti hii ni kwa sababu mashirika au kampuni kubwa zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwaibia wateja washonaji wadogo kwa miaka ya karibuni (leo hii ni wachache sana wanaokimbilia kwa mafundi kwa lengo la kutengeneza nguo ukilinganisha na wale wanaokwenda kwenye malls tofauti kununua moja kwa moja)

mwenye nguvu hapishwi bila ya kuandaa mikakati, sera na mbinu za kupambana naye
nimevutiwa na idea aliyokuja nayo dong jin ya kuwaunganisha washonaji wadogo (kwa kuanzisha ushirika) hususani kwa waliokuwa bado hawajamezwa na nguvu mpya ya uwekezaji(lengo ni kuwawezesha kuendelea na biashara zao bila ya khofu ya kupoteza wateja, kuendelea kuwepo kwa wateja wa uhakika ndio muendelezo wa familia zako kupata mahitaji yao ya msingi)

ko family craziness.
teh teh teh nimejikuta naikumbuka sauti ya marehemu kim young ae (ametumia uhusika wa choi gok ji humu ndani)pindi anapomwita mrs koo. episode mbili za mwisho pia zilifocus zaidi upande wa familia ya ko katika harakati zao kuyatafuta maridhiano, kilichonifurahisha zaidi ni kushuhudia kila muhusika getting redeemed kwa njia ilio sahihi na ya amani zaidi hatimaye baada ya vimbwanga vilivyodumu kwa takrabani episode 50 hatimaye familia ikawa ni kitu kimoja.
1602060537442.png
==========================

laurel tailor shop drama = marks 7.4/10
marry me now drama bado imebaki kuwa ni family drama bora kiupande wangu.
kinachofuata ni kuimaliza father is strange drama
 
genre ya THRILLER&ROMANCE kwa muda mmoja
labda kwa ninazozikumbuka haraka haraka
  1. IRIS 1 = kim hyun jun (lee byung hun) ni special agent kutoka shirika la NSS anayefanikiwa kufichua uharamia unaotendwa na kundi lenye nguvu kisiasa, kijamii, kibiashara linaloitwa IRIS
  2. IRIS 2 = mwendelezo wake baada ya kifo cha special agent kim hyun jun (aliuliwa na wauaji kutoka kundi la IRIS). nafasi ya lee byung hun ikazibwa na jang hyuk
  3. athena goddess of war: sijui niseme ni muendelezo au upande wa pili wa IRIS, ila nayo ni nzuri sana, nayo bajeti yake ilikuwa ni kubwa sana na pia lead actor ana ushawishi sana kwa sanaa ya korea hususani upande wa movies anaitwa jung sung woong (ana miaka 47 na wala hana stress ya ndoa, kwa nini dae nifunge ndoa)
  4. city hunter = stering ni mrembo kuliko mwanamke wake (halafu anavaa suruali mlegezo, sijui kama anaweza kubeba matofali yule fala)
  5. vagabond = ni nzuri sana
  6. W- Two Worlds = nzuri sana
  7. yongpal
  8. Memories of Alambara = ulimwengu wa game
  9. healer = sijawahi kuiangalia (no comment)
  10. come and hug me = sijawahi kuiangalia (no comment)
[emoji16][emoji16][emoji16] hivi we Dae una nini lakini kila siku unamuattack babe wangu, hem kaa kwa kutulia mxiiiuuu...wivu tu
 
Back
Top Bottom