Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Niliona BBC wameripoti kuhusu North Korea ku dis hiyi drama.

Ila all in all hawa jamaa wako professional sana na kazi zao, yaani ile drama imenichukua sana kimawazo mpka nikahisi hawa jamaa ni hatari sana. Ebu fikiria yale majengo ya North Korea kwenye drama walivyo yaandaa aisee ni hatari sana. Kuna vingi sana nimeona na nimejifunza sana kutokana na hiyo drama, nadhubutu kusema ile drama ndio bora kwangu.

Yule dada Son Ye Jin ni noma sana aisee, unajua huyu dada ameniliza sana.! Huyu dada ana hisia kali sana kwenye kuigiza, ile scene Hyun Bin na wenzake wanarudishwa kwao Korea Kaskazini aisee nilipenda sana yale maneno anamwambia mpenzi wake.
Son ye jin nilizoea kumuanglia kwenye personal taste nikjaa kumuona huku kwenye crash landing on u kabadlika kinoma

Sema hii crash landing ni nzuri mno huwezi amini kila siku naianglia hasa zile scene za north kuna yule maza wakuitwa wol suk ananifurahisha sana bila kumsahau pyo chi su[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Second Lead Syndrome inauma sana, Nampenda Yule kaka kweny Start Up Ila dah role anazocheza zinauma kama niache kutazama, Ila drama nzuri nayo
hii hali iliwahi kunikuta nyakati zile naangalia boys over flower drama.
nilitokezea kuvutiwa zaidi na kim hyun joong kuliko lee min ho.

kwa sasa naichukulia ni hali ya kawaida tu, ila mr dimples anastahili heshima zaidi ya hiii anayoipata.
wampe nafasi ya kuwa lead actor mara kwa mara kwenye project.
 
Penthouse nimeivuta ila bado sijaiangalia nahisi au nadhani nasubiria episode 16 zikamilike,

Malezi ya kikorea ni mabovu sana kila drama mtoto lazima amjibu mzazi vibaya mfano the heirs,18 again,sky castle, the world of the married. Yaani mzazi anajibishwa hadi sio poa ananuniwa,kitoto kikiamua hakiendi shule hakiendi na hakuna wa kumgusa. Kushinda PlayStation kitu cha kawaida,kuvuta sigara,makundi daah

Vipigo vya kibongo sometimes vinasaidia kurekebisha tabia

nipo na do do sol,start up huku nikichanganya na secret forest(hii bana story nzuri ila tu mie napenda kumuona huyu prosecutor mbishi mbishi hayumbishwi aiseee very handsome,sijui kutakua na kiss scene yake aaah😂😂😂😂😂eti hapo tu ndo napasubiria,mateso haya maana hata hakuna dalili😂😂😂😂)
mwezi December nimerudi kuangalia drama nilizokuwa na mipango nazo
  • nimemaliza kuiangalia start-up drama.
  • naangalia the penthouse drama

hawa watoto wa kitajiri na wale wakajamba nani walioko korea inaonekana wanalelewa kimasihara sana (kwa kuwa tupo korean nimeamua kuwatolea mfano wao tu), sijui ndio tuite utandawazi au utanda ukosefu wa tabia njema.

mtoto anampandishia sauti mzee wake, mzee hatimaye anaamua kuwa mnyonge kwa mtoto haijalishi awe sahihi kimtazamo dhidi ya mwanawe.

kwa sisi tuliolelewa na mama fatuma, mama asha, mama kipozeo, mama tukinao, mama maharibiko na mama wengineo wakiungana na baba mwijaku, baba mkandarasi, ukiwaletetea mbwembwe za kijinga zenye kuunganika na upumbavu mbona utakoma wewe.

mara zinatoka kauli:
" wewe khanithi (kwetu zenji ni tusi la kawaida tu), nimekulea miezi 9 tumboni ndio unaamua kuniletea sasa mambo ya kisengerema..... wewe mjaka mweusi hebu lete huo mkanda wa jeshi wa baba yako, huyu mpuuzi mwenzio anataka kunipanda matakoni(nimekusudia kichwani, typing error ila mtafuta nyinyi wasomaji)".

utapigwa hapo weee mpaka shekhe wa msikiti wa Ijumaa aje akuombee (na hotuba ya ijumaa ilivyo ndefu huyo shekhe hata akitoka msikitini mama watoto ameshakutoa makovu mwili mzima)
halafu kwa jeuri mama kibindinkoi anakwambia.

"sasa kesho utakwenda skuli, madrasa na sikupi hata shilingi 10 ya kutumia.
na utaisoma namba"
huu ndio uchumi wa buluuu
 
😂😂😂😂😂jamaa kauzu nimeimaliza season 1 ntaendelea na 2 ili tu nimuone
kuendelea kusubiria kiss scene ndani ya secret forest ni tukio gumu zaidi kuliko kuwasubiria wapinzani waitawale Tanzania pande zote mbili.
hivi haya maneno hukuwahi kuyasoma:
Hwang Si-Mok (Cho Seung-Woo) had brain surgery when he was a child, which caused him to lack emotion. Now, Hwang Si-Mok works as a prosecutor. He is rational, but cold and lonely.

muda wote huyo bwege anawaza haki
 
Pamoja na kwamba nina list ndefu lakini mwezi huu sio wangu Mara kichwa kinagonga balaa kikitulia nikitaka kuangalia usingizi huo. Aah nimeweka akiba za kutosha. Nipambane na afya kwanza nifanikiwe kuuona mwaka mpya
Asianwiki wameandika the penthouse ina episode 20.
niliwahi kusoma kichwa cha habari kwenye thread ya hiyo drama pale soompi inavyosemekana hiyo drama huenda ikarudi na season 2.

the penthouse usisubirie imalizike, nahofia itakupotezea masaa mengi kwa siku.
ni motooooooo
episode 13 nimeziangalia kwa siku 2, naitamani jumatatu ifike.
 
upcoming drama 2021: Mouse, 마우스
======

Jung Ba-Reum (Lee Seung-Gi) is a rookie police officer, working at a police substation. He is an honest person and tries to attain justice. He faces a psychopath murderer, who places the entire nation in fear. Jung Ba-Reum’s life is totally changed afterwards.
View attachment 1647979
Mkuu nataka kuangalia six flying dragon unaweza kunipa intro nini kimejili kwenye hii drama
Udambwi Udambwi wako unaweza kunipa ulevi
 
Hii drama nimetokea kuipenda mno. Japo kwa sababu zisizo na mashiko nilipomaliza tu kuiangalia nikaifuta ila ina kumbukumbu nzuri sana. Imenikumbusha mengi ya utoton huko,urafiki,kula kwa jirani(tena jirani mwenyewe anamtuma mwanae kamuite fulani mje mle ila ukigundulika home umekula kwa jirani fimbo zinahusika)
Kitu cha Awaken ni moto nacho

Nipo na penthouse
Awaken
Kairos
Na reply1988
 
★Guys habari zenu naomba Link nitakayo pata Tv series za Kichina tu hata zikiwemo za Korea ila Chinese series lazima ziwepo [emoji56][emoji119]★
 
Back
Top Bottom