Hatmaye Nimeimaliza "The Age of warriors", yenye episode 158. Hii series haikuwaelezea tawala za kijeshi kama ingeelzea zote basi tungekuwa Episode 300 na kuendelea.
Nadhani hakuna series nyingine yoyote iliyojawa na vipaji na masuperstar kuliko hii, toka nimeanza kuangalia Korean Drama, hii imevunja record ya kuwa na mastaa wengi na wenye vipaji vikubwa. Jambo la kufurahisha kwenye episode ya mwisho nipale baada ya msimulizi wa history anatupa summary ya kule tulipoanzia mpaka hapo mwisho, kisha anafanya Tathmini juu ya watawala wa kijeshi hao na Yi songgye( founder of Joeson) wanautofauti gani why walikuwa na uwezo wa kuwa Wafalme lakini waliiuacha ukoo wa Wang Madarakani kama puppet Kings wakati nguvu Mamlaka ilikuwa mikononi mwa Wanajeshi Hao, Lakini masomo tuliyopata kwenye historia ya watu hao. Kwahiyo niseme hii series ilipikwa kitaalam sana. Iliandaliwa na KBS.
List ya watawala wa Kijeshi(Goryeo )
1.Yi ui Bang (muda wa utawala miaka 5)
Aliuwawa na Jeong Jung Bu
2. Jeong Jung Bu (miaka 5), aliuwawa na Kyeong Dae Seung aliyekuwa na umri wa miaka 26.
3. Kyeong Dae Seung( miaka 4)
Alikufa kwa Maradhi baada ya kupewa sumu na mlinzi wake( Kim Ja kyuk) ambaye alikuwa Rafiki yake wa karibu. Baada ya kifo Chake Yi ui min ambaye alikuwa mlinzi wa Yi ui Bang ali - conquer Mji mkuu na kuchukua Madaraka.
4. Yi Ui Mini( miaka 13) aliuwawa na Choi cheong heon
5.Choi cheong heon(miaka 24) alirithisha madaraka kwa Mwanae( Choi woo)
Drama yetu( Age of warriors)iliishia kwa Choi Cheong heon.
6. Choi woo(miaka 30) alirithisha kwa mwanae Choi Hang
7. Choi hang( miaka 8) akarithi mwanae Choi Ui
8. Choi Ui(mwaka 1) akawauwawa na Kim Jun
9. Kim Jun( miaka 10) akauwawa na Im yeon ambaye alijiadaptisha kwa Kim Jun, na Kumuita Baba.
10. Im yeon(miaka 2) mtoto wake akarithi( Im yu mu
11. Im yu mu( mwaka 1) kisha akakonkwa na Mongol Dynasty ambayo muda wote ilikuwa na Vita dhidi ya Korea( Goryeo Dynasty)Tangu zama za Mwisho wa Utawala wa Choi Cheong heon. Hawa jamaa walipigana kwa miaka mingi hatmaye Goeyeo wakaenda chini ya Mongols and Yuen Dynasties.na ndio ulikuwa mwisho wa zama za utawala wa kijeshi. Miaka karibu 80 ilipopita ndipo General Choi Young na Yi Songgye walipoanza mapambano na Mongols na Yuan waliposhinda vita na kuikomboa Koryeo toka mikononi mwa wa wamongoli na wayuan.
NOTE; Yi Songgye mwanzilishi wa Joseon Dynasty alikuwa ni zao la familia ya Yi In, ambaye alikuwa ni mdogo wa General Yi ui Bang. Huu ukoo wa kina Yi ui bang ulikuwa wa Mageneral, maana Baba yao pia alikuwa General, hata Yi Songgye kabla ya kuwa mfalme alikuwa ni General wa Goryeo.