Law school nimejikuta naenda nayo hivyo hivyo mpaka episode 16 jamani jamani inachosha sio tu kwa vifungu vya laws bali haina story nzuri yenye kauhalisia,walitakiwa wa focus maisha ya chuo na mafunzo ya sheria kama medical dramas ila hawa wameenda mbali kupelekana mahakamani mara wanafunzi wa first year wanatunishiana misuli na kigogo mwenye nguvu zake bungeni. Inaenda mbele inarudi nyuma.Nilitegemea watakaa darasani ,wataonyesha struggle za wanachuo wa laws,mitihani,practices za hapa na pale chuoni kisha wakienda fields kama interns
HAINA HATA KISS SCENE YA KUBABAISHIA
Weekend inanikuta na drama ya so i married an anti fan(story ya kuzugia ili mradi tu na wao wamefyatua ka drama)nimependa scene ya japan daah watu wanaishi. Bonge la daraja linalovuka sijui bahari ile hadi hotelini
Nina kiporo cha gye baek(nimekosa historical nimenasa hapa kwa muda,ukichanganya ya mjini na historical inanoga)
Sell your haunted house(ipo poa japo nimevuta mpaka ep 2 ila ntaenda nayo mpaka mwisho)
Bila kusahau family drama i have a lover(shukran kwa sifa ilizopewa na dae,naenda nayo mdogo mdogo)
Happy weekend!!