Leo nilipata nafasi ta kuwa mgeni kwa rafiki yangu mmoja, nikiwa pale kuna K-drama niliiona na nikaipenda sana ila nimesindwa kuipata licha ya kuwajua waigizaji kwa sura zao, maana imetafasiriwa na Madj kwahiyo wameibadili jina.
Plot.
Kuna jamaa alikuwa general kwenye ufalme fulani lakini baada ya kurudi kutoka vitani aliuliwa kwa amri ya mfalme kwa kuchomwa panga kifuani, baada ya hapo alifufufuka na kuwa mtu ambaye hafi. Inasemekana kuna binti atakezaliwa ndiye atakaekuwa na uwezo wa kulichomoa hilo panga ili jamaa arudi kwenye gali yake ya ubinadamu.
Naombeni jina la drama kama hamtojali wakuu,...[emoji120]