Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Baada ya mapumziko ya miezi miwili nahitaji kurudi tena kwenye huu ulimwengu wa Kdrama.

Zamani nilikuwa siwezi kutimiza hata wiki mbili ila kwa sasa nateleza kama kambare, si ajabu mwezi septemba ukamaliza na bado sijarudi ulingoni

Changamoto kuu niliyoiona ni kupanda kwa gharama za mtandao wa internet, kwa drama inayobeba episode 16 ukitumia tovuti ya kimoi, kisssasian au nkiri utahitaji wastani wa GB 2 hadi 3.

Jaalia una viporo vyako vitatu wataka kuvipasha moto, kule wanakotokea wazazi wangu wanaita mwiku badala ya uporo

Kwa pesa za kitanzania hiyo ni shilingi 6000 kwa kila drama.
Ngoja hawa watu wa hii taasisi wanipe password ya WI-FI yao

Tozonovic kuelekea tozoninho
 
VIPORO VYANGU
  • Doctor lawyer drama - nilifika episode 10​
  • She would never know drama - nimeshasahau, huenda ni 10 au 12​
  • Alchemy of souls drama - episode 6 au 7 ndipo nilipofikia, nakumbuka nilimaliza pale yule bwana anayetafuta naksu alipoingia katika mwili wa lead actor.​
Mudeok ananifurahisha sana na lahaja yake (dialect) ya chun cheong do.
Wakorea kusini wana lahaja takribani 6.
Wanaotumia lahaja ya chun cheong do mara nyingi matamshi yao ya maneno humalizia na Yo au Yu.

geureom yooo
jamkkanman yoooo
jangnanhae yoooo

Raha ukutane na watu wa busan na lafudhi yao ya Gyeong sang do,
halafu umkute jamaa ndio wale wakopeshaji wanaowaita loan shark kwenye drama au wahuni wanaovaa mashati ya rangi yenye maua ya dada mwajuma.

Mannaa, kamsahaemniddaa.
Wamekazana mpaka wanapozungumza
Teh teh teh
-----------

Huku kwetu tunaona aibu kutumia lahaja zetu, ukiangalia filamu au tamthilia zetu tunajikita zaidi na kiswahili cha mjini.

Naenjoy sana nikiwasikiliza wapemba wenzangu au wamakunduchi wanapochowea.

Nakona sinakuona siku hizi pwani au kuundu lako jahazi.

mbona siku hizi sikuoni pwani au unaunda au kutengeza jahazi lako

Unabaki unaduwaaa
Huyu bwege hapa amenisifia au amenitukana.
 
Umesema lahaja umenikumbusha hiyo ya busan uloitaja si ndo alikua nayo kim so hyun kwenye dream high

Basi wakati natizama masked singer kuna mwimbaj mmoja wa troti wanasema ndo BTS wa trot music akiongea hivyo alafu alivyo handsome hadi sijaamini, Yan hafananii[emoji16]

Vilahaja vingine havivutii kusema kweli kama kina nchumali [emoji1787] nisameheni
 
Baada ya mapumziko ya miezi miwili nahitaji kurudi tena kwenye huu ulimwengu wa Kdrama.

Zamani nilikuwa siwezi kutimiza hata wiki mbili ila kwa sasa nateleza kama kambare, si ajabu mwezi septemba ukamaliza na bado sijarudi ulingoni

Changamoto kuu niliyoiona ni kupanda kwa gharama za mtandao wa internet, kwa drama inayobeba episode 16 ukitumia tovuti ya kimoi, kisssasian au nkiri utahitaji wastani wa GB 2 hadi 3.

Jaalia una viporo vyako vitatu wataka kuvipasha moto, kule wanakotokea wazazi wangu wanaita mwiku badala ya uporo

Kwa pesa za kitanzania hiyo ni shilingi 6000 kwa kila drama.
Ngoja hawa watu wa hii taasisi wanipe password ya WI-FI yao

Tozonovic kuelekea tozoninho

Hali ikiwa tete Dae utajifunza kwa moyo namna ya kutumia kitonga kama ulivyotufundisha ku download wakorea
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti kiupinde upinde. Haina bwana pale alitaka kumkata ngebe tu yule mjinga aliyekuwa anamchimba
Hehehehehe... homosexuality scenes annoy me kiukweli ndo maana napenda kdrama sababu ni nadra sana, Holywood zenyewe huwa nachagua sana kama zipo basi 1% kama suits as in wanakua wanaongea tu na hakuna ishu za romance
 
Umesema lahaja umenikumbusha hiyo ya busan uloitaja si ndo alikua nayo kim so hyun kwenye dream high
Hii sijaiangalia

Basi wakati natizama masked singer kuna mwimbaj mmoja wa troti wanasema ndo BTS wa trot music akiongea hivyo alafu alivyo handsome hadi sijaamini, Yan hafananii
Ukiishi naye Seoul atabadilika, ungelifanya mpango ukamuomba namba yake ya simu.

Ungelimwambia mimi ni fans wako japokuwa sipendi lafudhi yako
Teh teh teh
 
Hehehehehe... homosexuality scenes annoy me kiukweli ndo maana napenda kdrama sababu ni nadra sana, Holywood zenyewe huwa nachagua sana kama zipo basi 1% kama suits as in wanakua wanaongea tu na hakuna ishu za romance
Wakorea wanazo BL dramas za kumwaga, na zinafuatiliwa kwa kiwango kikubwa sana na mashabiki wa nje.

BL = boy's love
 
Wafatilie tu... I thank God until now na hata zamani sijawahi kutana na upinde upinde kwa nilizoangalia... (za kijijini huwa ni 1st priority kwangu za mjini nimeangalia chache na zote nimezipenda with 0 upinde)
 
SBS "One Dollar Lawyer drama" Teaser​

talnam
Namgoong min anagonga papo kwa papo.
Akitoka hapo ana project nyengine ya historical anaifanyia review na pia kuna doctor prisoner season 2

Bila ya shaka huyu bwana atakuwa na mihela mingi mno, anawezaje kulipia hela ya pango, chakula, mavazi na mengineyo kwa malipo ya dola 1 tu anayopokea kutoka kwa wateja wake.

Jaalia kibatala ndio unamlipa buku 1 kwa msaada wa kisheria atakaokupa.
Sijui mmenielewa

Itakuwa ni September 23
Inshaallah (akipenda Mungu na majaaliwa yake)
 
Am looking forward to it ingawa drama yake nimetoka kuifuta jana baada ya kufika episode ya saba nikashindwa kuendelea. Nina mpango wa kuicheki The veil na hii
 
Back
Top Bottom