Tokea nianze kuangalia na kufuatilia sanaa ya wakorea hususani upande wa tamthilia kwa miaka 11.
nashawishika kukiri ya kwamba sijapata kushuhudia uhusika wa muigizaji msaidizi ulioshiba na kujitosheleza kuzidi uhusika wa
MI SHIL ndani ya queen seondeok drama.
Nimefika episodes ya 20 ya hii drama.
Nimeandika komenti hii nikiwa:-
sijalewa,
Zeco hawajakata umeme kwamba nimeandika gizani,
Sijavuta bangi,
Sijanywa sumu,
Sijavaa fulana ya chama dola,
Sijatekwa,
sijalala kwa hamida.
sijanywa mirinda nyeusi,
Sijaandaa kamba ya katani kwa kujinyongea,
Kudos kwa muandishi, kudos kwa director, kudos kwa makeup artist aliyehusika na upambaji wa mwanadada Go Hyung Jung, bila ya kusahau heshima iendelee kumfikia mtaalamu wa mavazi.
Huyu dada ameigiza ikiwa amerelax, mpaka nimefikia kujiuliza huyu mjinga anaigiza au ni uhalisia?
Ni haki yake kushinda tuzo ya grand prize, amemfundisha jinsi ya kuigiza mwanadada lee yo won
View attachment 2433669