Kwa wasiofuga na kulima ndio uona maisha ni magumu

Kwa wasiofuga na kulima ndio uona maisha ni magumu

Mtu kasomea udaktari unamlazimisha akalime wakati anaweza kufungua hata duka la dawa akapiga pesa vizuri tu.

Miwili wa binadamu unatufundisha kuwa Kuna specialization kwani kila kiungo kinafanya kazi yake kwa kushirikiana na vingine
Kila mmoja akikumbatia anachozalisha bila kukiuza kwa wengine, wapo watakao lala njaa na phd zao.​
 
Maisha ni magumu kwa asiyelima na kufuga, anayetegemea apate shilingi mia ndio iwe unga, kitunguu, nyanya n.k

Kama una lima na kufuga, tayari unakuwa na uhakika wa chakula pamoja na hela za ziada; na hii itakuletea utulivu wa nafsi na kujiamini bila kumtegemea mtu.

Kwa wale wasiolima na kutegemea mishahara tu, ndio wanao ona maisha ni magumu.

Majungu, fitna, na chuki za hapa na pale, zinatokana na kutokulima pamoja na kufuga.

Je ni kweli ama si kweli?​
Ukweli mtupu
 
Hajawahi kutokea hiyo ni nadharia tu

Na sisi tusiponunua chakula chako, utapata wapi hela ya pembejeo?

Mkeo akiumwa utaenda na ng'ombe wako hospitali ? (Barter trade)
'Barter trade' ikirudi, wote wa mjini watakufa kwa njaa kwa sababu hawazalishi zaidi ya kuishi kwa maandishi andishi.
 
Watanzania wanaoongoza kwa umaskini ni wakulima kisha wanafuata wafugaji.

Kwa wastani, mlinzi wa mgambo wa jiji ana asilimia kubwa ya kuwa na uchumi mkubwa kumzidi mkulima. Au twende Matombo tuwaone hao wakulima wasio hata na kiberiti wanagongea moto kwa jirani mwalimu wa shule ya msingi?
Lakini kila siku mabucha yamejaa nyama, zinatoka wapi?
 
Kila mmoja akikumbatia anachozalisha bila kukiuza kwa wengine, wapo watakao lala njaa na phd zao.​
Hao wenye PHD, wengine wanafanya research kila siku ili wewe uzalishe kwa ubora na kwa wingi, bila wao kuzalisha pembejeo, vifaa hata wewe huwezi kulima

Unalimaje bila afya, ulinzi

Bila madaktari, mapolisi, walimu, jeshi huenda hata hapa Jf usingekuwepo, maana ungekuwa hata kusoma hujui pia ungekuwa ushakufa kwa magonjwa
 
Wakulima hawana hela yoyote na wengi ni masikini

Wakulima wenye pesa ni hawa ambao wanalima kibiashara na kimkakati .

Ila 90% wapo wanalima for substance and not commercial.

Ikiwa Kama Mimi ni bora nifanye Kazi inayoweza nipatia 2M kwa mwezi Ila sio kulima Kama mkulima mdogo anayetegemea Mvua na hana uhakika wa kuvuna .


Kwakuwa bajeti ya chakula ni ndogo ukiwa na 100K unapata Michele wa kula .mwezi mzima familia ya watu watano

Hoja yako ni.nzuri Sana Ila imewalenga watu wa vijijini ambao wapo na Kazi zao nyingine au wale watu wa kati
 
Maisha ni magumu kwa asiyelima na kufuga, anayetegemea apate shilingi mia ndio iwe unga, kitunguu, nyanya n.k

Kama una lima na kufuga, tayari unakuwa na uhakika wa chakula pamoja na hela za ziada; na hii itakuletea utulivu wa nafsi na kujiamini bila kumtegemea mtu.

Kwa wale wasiolima na kutegemea mishahara tu, ndio wanao ona maisha ni magumu.

Majungu, fitna, na chuki za hapa na pale, zinatokana na kutokulima pamoja na kufuga.

Je ni kweli ama si kweli?​
Si lazima kufuga wanyama mahayawani au kulima mazao.Mimi sifanyi hayo yote ila nafuga familia tu.Na nina furaha.
 
Bila madaktari, mapolisi, walimu, jeshi huenda hata hapa Jf usingekuwepo, maana ungekuwa hata kusoma hujui pia ungekuwa ushakufa kwa magonjwa
Kuna mifumo mingine ilianzishwa kwa ajili ya kuwanyonya wazalishaji halali ambao ni wakulima na wafugaji; haiwezekani mtu aponde kokoto la tipa zima apewe elfu 30, huku mwingine ameajiriwa na kuhudhuria kikao cha nusu saa akapewa laki 5; hapo ni yupi mnyonyaji?

'Barter trade' ina umuhimu sana katika kupunguza hilo 'gap'​
 
nimegindua asilimia kubwa ya watu majini wameajiriwa.

yanileo asubuhi njia nyeupe sana nimefanya mambo kwa uhuru
Na hawawezi kuwa na mawazo ya kuwekeza kwenye kilimo/ufugaji; ndio maana mapori ni mengi yanazidi idadi ya watu.
Kila mmoja anapambana asifukuzwe kazi​
 
Wakulima hawana hela yoyote na wengi ni masikini

Wakulima wenye pesa ni hawa ambao wanalima kibiashara na kimkakati .

Ila 90% wapo wanalima for substance and not commercial.

Ikiwa Kama Mimi ni bora nifanye Kazi inayoweza nipatia 2M kwa mwezi Ila sio kulima Kama mkulima mdogo anayetegemea Mvua na hana uhakika wa kuvuna .


Kwakuwa bajeti ya chakula ni ndogo ukiwa na 100K unapata Michele wa kula .mwezi mzima familia ya watu watano

Hoja yako ni.nzuri Sana Ila imewalenga watu wa vijijini ambao wapo na Kazi zao nyingine au wale watu wa kati
'Barter trade' ikirudi, utaweza kuishi?
 
Back
Top Bottom