Kwa Watanzania walio na malengo ya kuishi kutafuta kazi au kusoma nchini Ubelgiji au Uswisi someni hapa

Kwa Watanzania walio na malengo ya kuishi kutafuta kazi au kusoma nchini Ubelgiji au Uswisi someni hapa

Uzi mzuri lakini wabongo kuchangamkia fursa kimataifa huwa ni wagumu mno wengi hawajiamini hili andiko labda litawafaidisha wakenya tu kupata connection na huyo mwenzao uliesema anamiliki Club ya Rumba
 
Uzi mzuri lakini wabongo kuchangamkia fursa kimataifa huwa ni wagumu mno wengi hawajiamini hili andiko labda litawafaidisha wakenya tu kupata connection na huyo mwenzao uliesema anamiliki Club ya Rumba
😀😀😀
 
Mkuu Parabora ingependeza ungeshea nasi vile vilivyomo au vinavyopatikana ndani ya hizo night club nadhani kutakuwa na vitu vya ziada tofauti na night club zetu,,
 
Kipindi hiki ambacho niko kwenye zuio la kutoka nje liliowekwa na mamlaka ya jiji nililomo nimeamua kuwa nashare hapa baadhi ya mambo ya nchi nilizowahi kukaa ili ziwe na manufaa kwa wenye malengo ya kutafuta maisha nje ya Africa mashariki.

Juzi nilileta andiko linahusu nchi ya Uswisi baadhi ya wachangiaji walicomplain kwamba nimezungumzia starehe zaidi ni kweli ilikuwa hivo na kwa bahati mbaya sikufikiria Kama lengo kuu la wasomaji litakuwa fursa za ajira tuwiane radhi kwa hilo

Kama heading isemavyo leo nazizungumzia hizi nchi mbili za Ubelgiji na Uswisi kwa kuzilinganisha na mazingira ya muhamiaji mweusi anaeanza kutafuta maisha ughaibuni kwa mara ya kwanza, nilikaa Ubelgiji kwa miaka 4 nikiwa nasoma chuo cha Ghent University ambacho kipo katika mji wenye masoko na supermarket nyingi wa Ghent kabla ya kwenda Japan kufanya kazi na Baadae kuhamishiwa Uswisi miaka 3 iliyopita kama ilivyokuwa kwenye andiko la Uswisi juzi hizi nchi zote ziko chini ya umoja wa Ulaya (EU) na zina mambo mengi ya kisera na kidiplomasia yanayofanana na zimetangishwa na umbali usiozidi 650km kwa barabara na unaweza kuzisafiria kwa kutumia gari binafsi, basi la abiria, treni au hata ndege

Lugha zinazotumika Ubelgiji ni kifaransa, kijerumani na kidutch kulingana na wenyeji wa eneo husika mji wa Ghent ambao nilikuwa nasoma wenyeji lugha yao ni ki-dutch japokuwa karibia wabelgiji wote wanajua lugha ya kiingereza kwa ufasaha pamoja na kwamba watu wa Switzerland ni wakarimu lakini wabelgiji ni wakarimu sana sana hawa wako tayari kujitolea kukupa msaada wowote pale itakapohitajika ni watu wenye upendo na heshima kwa kila mtu na usalama wa nchi sio wa kutisha sana ni nchi tulivu

Maisha katika majiji ya Ubelgiji ni nafuu sana ukilinganisha na maisha katika majiji ya Switzerland ambako ni ghali zaidi ni vigumu kula msosi mbaya nchini Ubelgiji, gharama za makazi, vyakula, vinywaji, usafiri na huduma za afya ziko chini sana MFANO nyumba unayoweza kupata kwa Euro 1000 jijini Geneva na Euro1300 jijini Zurich unaweza kuipata kwa Euro 300 mpaka Euro 420 jijini Brussels (Ubelgiji) na bia za zinazotengenezwa ndani zenye ujazo wa lita moja ambazo Geneva wanauza Euro16 na Zurich Euro18 Brussels zinauzwa Euro8 vivyo hivyo na kwa huduma nyingine ni nafuu zaidi japokuwa gharama za Kodi zinazotozwa na mamlaka ya Uswisi ziko chini kulinganisha na kodi zinazotozwa nchini Ubelgiji,
Kwa watafutaji wanaoanza maisha na wenye uhakika wa kipato ama ajira za mishahara ya kati Ubelgiji ni nchi nzuri ya kuanzia maisha kuliko Switzerland.

Ubelgiji wahamiaji wengi hukimbilia kuishi Brussels na kupata ajira Ubelgiji kwa mhamiaji wa kiafrica fresh graduate degree/diploma na hauna special skills nyingine yoyote ni vigumu mno na inaweza kuchukua mda sana hizi nchi zote Swiz na Ubelgiji wanatumia sheria za EU kwenye ajira ili kujaribu kutafuta raia wa Ulaya ambae ana sifa za kufanya kazi husika kabla ya kumuangalia wa nje na hili kwa Belgium wanalitekeleza kisawasawa tofauti na Uswiz ambako Kuna room ya kupata kazi kama una ujuzi na weledi wa kutosha na usiotia mashaka kwa kujitosheleza, kwa Ubelgiji raia wa EU wanapata kazi kirahisi sana kuliko raia wa nchi zingine

Kwa wasio na ujuzi Ubelgiji sio sehemu nzuri ya kujilipua kwa madhumuni ya kutafuta kazi au maisha ni vigumu sana kupata kulingana na maelezo niliyotoa hapo juu na sera zao za EU wahispania wengi wameshazichangamkia japo kuna black walio pata na hii inategemea na uenyeji wako, uswisi uwezekano wa kupata hata kazi za kuhudumia kambi za wazee, walemavu,mashambani kukata nyasi au viwandani Kwa wahamiaji kama vibarua kwa malipo yasiyopungua CHF 30 kwa saa upo japo nako sio rahisi lakini sio Kama Belgium

Kwenye suala la malipo Uswisi wanalipa unono sana zaidi ya mara5 kwa kiasi ambacho analipwa mtaalam anaefanya kazi nchini Ubelgiji kwa kada hiyohiyo na bado utalipwa housing na transport, support ya bill ya umeme na maji pamoja na malipo ya Emergency na makato ya Kodi ni madogo kulinganisha na Belgium na hata kwa vibarua ni hivohivo na hapa unaweza kuona Ubelgiji maisha ni magumu lakini yanavumilika kutokana na gharama za huduma muhimu kuwa chini kuliko uswisi ambapo unalipwa vizuri na ughali wa maisha uko juu na hili linafanya wengi wanaofanya kazi Uswisi kupanga Apartment na kukaa katika nchi jirani Kama Ufaransa, Ujerumani,Italia na Austria Uswisi inakuwa ni sehemu ya kufanya kazi tu shopping na kila kitu vinafanyika nchi jirani na kwa miundombinu iliyopo usafiri na suala la kuwahi kazini sio tatizo japo wanaishi na kufanya kazi nchi tofauti

LAKINI likija suala la nchi gani nzuri ya kuishi kati ya hizi mbili jibu ni SWITZERLAND.

Kwa wenye uhitaji wa kutafuta elimu katika nchi hizi, nikuhakikishie tu zote zina mifumo mizuri ya kielimu kuanzia kindergarten mpaka elimu ya chuo yenye hadhi ya kimataifa na raia wengi wa hizi nchi hupeleka watoto wao shule na vyuo vya serikali kulingana na ubora uliopo na gharama kuwa ndogo shule za private mara nyingi hutumiwa na wageni kusomeshea watoto wao kwa nchi ya Ubelgiji kuna baadhi ya vyuo vya kanisa katolic vina ubora mno sawa au zaidi ya vya umma, kwa waafrica na wageni wengine gharama ni za kawaida kabisa kwa school fees kuanzia Euro4000 na kuendeleza na vingine vipo pungufu ya bei hiyo, binafsi nashauri kama kuna mtu atahitaji kusoma katika nchi hizi basi chaguo liwe Uswisi hasa kwa fani za sayansi na teknolojia hawa jamaa ni wanasayansi haswa japokuwa kwamba maisha ni ghali sana kwenye kujikimu na pia hili haliondoi kwamba vyuo vya Ubelgiji ni bora duniani

KWA WALE WAPENDA STAREHE KAMA MIMI
Itabidi mnisamehe tu wanabodi siwezi kumaliza bila kugusia hiki kipengele cha kujirusha wengine ndio ulevi wetu maana hatunywi wala hatuvuti chochote.
Kipindi naanza chuo Ghent University mkuu wa shughuli za Event katika serikali ya wanafunzi alikuwa bwana mmoja Denis John Obiel raia wa Nigeria alikuwa anasomea uchumi na pia alikuwa msimamizi wa Ghent Students Club huyu jamaa baadae aliniteua kuwa msaidizi wake baada ya kutengeneza nae urafiki kwa vile wote tulijikuta ni watu wa Night-life na starehe na tukawa marafiki wa damu tuliingia karibu Club zote za karibu na chuo na jiji zima la Ghent zilizokuwa zinavuma Kama Abacho Club, Club1847, Hot Club Gent, Niche Club, Club central, Club69 na tukitaka kujichanganya kwa pamoja tunaenda Black & white night Club

Na kwa vile Brussels haikuwa mbali kutoka Ghent hatukusita kutia timu kwenye Club zao ambazo ni za ubora zaidi kama vile Sunset Club, Fuse, zodiac, C12 club na Birdy Brussels Club

na tulipoona hatutosheki tulichukua tax kwa Euro10 mpaka mji wa leuven mwendo wa dk 20 kutoka jiji la Brussels huko kulikuwa na Club inayomilikiwa na mkenya bwana Jangis Ong'ong'o ilijulikama kama Rumba Club na tulikuwa tunaingia bure na Kama ilivyo kwa wapenda starehe hatukuridhika tukawa tunaenda Club zingine za huohuo mji Kama Faculty club na The social Club kwa kulipia wakati kwa mzee Ong'ong'o ipo ya bure na ni ya hadhi ya juu kwa wapenda Night-life ukifika huko zitafute hizo Club hutojuta kwa uzuri wake na kukutana na watoto wa kike wa Kibelgiji wabichi kabisa wasiokuwa na mapozi.

MENGINE TUTAJADILIANA KWENYE COMMENT

Parabora
Geneva -Switzerland

Chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hatari
Mkuu hebu nipe connection ya scholarship za Masters huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Parabora mi nakualika Scotland na nakuahidi Ukija huku,stress free na nyumba ya kufikia na chakula chako chote during your stay,

Ila Mzee Mimi nakujirusha katika maisha yangu yote nimewahi mara moja Tu night club Scotland tena ilikuwa ni Kwa sababu maalum ndo mana nilienda,jamaa walikuwa wanafanya fund Raising ya charity ambayo nipo involved,

Ukifika huku ntakupa kila Aina support na list ya club zote na kama Una driving licence ya EU,na Gari pia ntakupa uzungukie night club zote mpka uchoke,

Hapa IPO Night club moja ya wakenya kama ulivyozungumzia hapo juu ukanimbusha unaitwa KALABASH,ndo huwa naskia vijana wengi wa ngozi zetu hizi wanajitumbukiza huko,Mimi sijawahi Tia mguu labda kupita Kwa nje Tu.

Wabongo walio wengi huwa wanapenda kwenda nje kujiripua kikimbizi na kutobolea njia hiyo na sio wengi sana ambao wanapenda kutumia route ya kusoma,nadhani hili linachagizwa zaidi na gharama ndefu za kuandaa masomo nje ya Nchi,

Karibu Sana Mkuu
Mzee wa Scotland Adabwash washe, Daby na totoz zako akina Khantwe na Jael kujeni huku mfanye utaratibu wa kukwea mwewe
cc Depal ,Victoire , Dinazarde,Witmak255, daud 1990,bullar, amu, Extrovert,HARUFU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Parabora mi nakualika Scotland na nakuahidi Ukija huku,stress free na nyumba ya kufikia na chakula chako chote during your stay,

Ila Mzee Mimi nakujirusha katika maisha yangu yote nimewahi mara moja Tu night club Scotland tena ilikuwa ni Kwa sababu maalum ndo mana nilienda,jamaa walikuwa wanafanya fund Raising ya charity ambayo nipo involved,

Ukifika huku ntakupa kila Aina support na list ya club zote na kama Una driving licence ya EU,na Gari pia ntakupa uzungukie night club zote mpka uchoke,

Hapa IPO Night club moja ya wakenya kama ulivyozungumzia hapo juu ukanimbusha unaitwa KALABASH,ndo huwa naskia vijana wengi wa ngozi zetu hizi wanajitumbukiza huko,Mimi sijawahi Tia mguu labda kupita Kwa nje Tu.

Wabongo walio wengi huwa wanapenda kwenda nje kujiripua kikimbizi na kutobolea njia hiyo na sio wengi sana ambao wanapenda kutumia route ya kusoma,nadhani hili linachagizwa zaidi na gharama ndefu za kuandaa masomo nje ya Nchi,

Karibu Sana Mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu Adabwash kwanza nashukuru sana Jf kutukutanisha wewe tayari ni ndugu na rafiki wa karibu nakuahidi nitakuwa huko kabla ya mwaka huu kuisha
 
Lockdown inafaida zake,Mabandiko kama haya tusingeyapata kama si Kwa faida ya covid 19,

Mi Mzee nimekaa ndani mpaka Najiskia kupiga makele, na nikiona video watu wapaost ukifungua mlango ndo kirusi kinakungoje ndo kabisaaaa nazidi kuchanganyikiwa.
Mzee wa Scotland Adabwash washe, Daby na totoz zako akina Khantwe na Jael kujeni huku mfanye utaratibu wa kukwea mwewe
cc Depal ,Victoire , Dinazarde,Witmak255, daud 1990,bullar, amu, Extrovert,HARUFU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown inafaida zake,Mabandiko kama haya tusingeyapata kama si Kwa faida ya covid 19,

Mi Mzee nimekaa ndani mpaka Najiskia kupiga makele, na nikiona video watu wapaost ukifungua mlango ndo kirusi kinakungoje ndo kabisaaaa nazidi kuchanganyikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
😃😃😃😃😃Kaka we acha tu Mimi mgongo unauma kwa kulala
 
Back
Top Bottom