Kwa watoa sadaka tu: Sadaka ya vitu Ina nguvu kubwa kuliko cash au sadaka za miamala

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Tendo la Kutoa sadaka limefungamanishwa katika Kila selihai ya mwanadamu bila kujali anamuamini au haamini Mungu.

Watu wote hutoa sadaka. Tofauti ni mahali wanapotoa na Nia nyuma ya utoaji huo.

Ukifuatilia historian ya utoaji sadaka sadaka inayozolewa moja kwa moja kama vitu au huduma inanguvu kubwa kuliko cash.

Cash inaongeza mzunguko, unampa mpokeaji jukumu la kuibadili hiyo cash kuwa huduma au kitu. Hapo katikati kwenye mchakato inaweza kifujwa, kibadilishiwa matumizi au kucheleweshwa kufikia lengo. Hii inamnyima mnufaikaji kifurahi kusudi la sadaka hiyo kwa wakati. Baraka za sadaka humwagwa baada ya kusudi kufikia kwa mlengwa.

Katika sadaka zako, jitahidi utoe vitu. Au huduma. Kama ni Cash basi iwe ni wakati ambapo hakuna namna kabisa.

Barikiwa

Mtumishi
Matunduizi
 
Mchungaji wetu alichangisha sadaka ya ujenzi wa kanisa ni sawa,
Akaja kutangaza kabisa halitoshi anataka ajenge la ghorofa🤔 watu wakajichanga sasa hivi linajengwa

Hapo kati akasema sadaka ya ujenzi inaendelea sababu anataka kujenga shule ya msingi ya kanisa🤔
Nikiangalia waumini wenzangu maisha yetu ni ya kuungaunga.
Nikamuuliza katibu wa kanisa, shule ikijengwa watoto wa waumini waliochanga pesa zao watasoma bure? Nikajibiwa hapana lazima wachangie.

Sadaka yenye baraka ni ile ya kuwapa wenye uhitaji na sio kuwalimbikizia mali wachungaji.

Mimi wachungaji hawatokula tena hela zangu kizembe.
 
Sitakaa toa sadaka kanisani au msikitini kamwe.

Sadaka yangu nitatoa katika watu wenye uhitaji wa moja kwa moja..
-- Kuna watu wako mahospitalini walipata magonjwa wameshindwa lipa bili ili watoke na wao ndo baba au mama wanaotegemewa na familia zao(Mtu kama huyu ukaenda uka mlipia bili alafu akatoka akaenda pambania familia yake ) baraka ukazo pata hapa ni mara mia ya ulotoa kwa nabiii.

--Kuna watu kwa kumuungalia tuu unaona anazo shida hata kula ni tatizo japo hajakuomba ila mtu kama huyu ukamtengenezea njia maisha yake yakawa na ahueni ni baraka tosha.
-Niliwahi mkuta mama mmoja yuko njiani amekaa kando ya barabara na mtoto wake kalala pembeni yeye anauza karanga za mia mia zilikuwa kama 20 hivi. Sura inaonesha tuu shida alizokuwa nazo kabisa(ki mahesabu hata akiuza karanga zote faida ni ipi hapo na mtaji ni upi uapo ili aendelee ishi?)

Watu kama hawa ndo unatafuta kibiashara chochote unamletea ambacho kitaendelea mpa zaidi ya kile.(kama masanduku ya kuhifadhi baridi na vinywaji humo ndan na maji ) awe anauza.

Nachokereka makanisani hasa yakinabiii hawana utu kabisaa narudia hawana utu kabisa hakuna hata siku nabii au mchungaji anasemea tutembelee wenye uhitaji.. Kwa upande wa Waislam hilo nawapa hongera wamejitahidi.
 
tukuletee nini nabii/mtume matunduizi?
Nitake radhi Mimi sio unabii wala mtume.
Ukiniita Matunduizi inatosha.
Wanaoleta ni walioongozwa kuleta sio wanaoomba kuleta. Ukiongozwa kuleta utaambiwa na cha kuleta.
 
Mchungaji wetu alichangisha sadaka ya ujenzi wa kanisa ni sawa,
Akaja kutangaza kabisa halitoshi anataka ajenge la ghorofa🤔 watu wakajichanga sasa hivi linajengwa

Hapo kati akasema sadaka ya ujenzi inaendelea sababu anataka kujenga shule ya msingi ya kanisa🤔
Nikiangalia waumini wenzangu maisha yetu ni ya kuungaunga.
Nikamuuliza katibu wa kanisa, shule ikijengwa watoto wa waumini waliochanga pesa zao watasoma bure? Nikajibiwa hapana lazima wachangie.

Sadaka yenye baraka ni ile ya kuwapa wenye uhitaji na sio kuwalimbikizia mali wachungaji.

Mimi wachungaji hawatokula tena hela zangu kizembe.
Sadaka ni Pato halali la mchungaji.

Mtoa sadaka ni Yule anayeamini, alivyonavyo sio vyake ni Mungu tu amepitishia vitu kwake ili viwe Baraka kwa familia, wahitaji na kazi zake. Mtu ambaye anadhani sadaka anatoa kwenye pesa zake anazomiliki sadaka hizo hazima Baraka wala matokeo
 
Waweza elezea utofauti wa madhabu na kanisa?
Madhabahu: a place of contact with devine. Mahala/Muundombinu au mazingira ambapo panamuunganisha mtoaji na Mungu wake au Muungu kwa wanadamu.
Kanisa ni mkusanyiko wa watu wa Imani moja wenye mafundisho wanayokubaliana. Sio jengo japo watu Hao wanaweza kukutqna mjrngoni.
Madhabahu sio Lazima iwe kanisani.

Unaweza kusahihisha au kuongeza
 
Mchungaji wetu alichangisha sadaka ya ujenzi wa kanisa ni sawa,
Akaja kutangaza kabisa halitoshi anataka ajenge la ghorofa🤔 watu wakajichanga sasa hivi linajengwa

Hapo kati akasema sadaka ya ujenzi inaendelea sababu anataka kujenga shule ya msingi ya kanisa🤔
Nikiangalia waumini wenzangu maisha yetu ni ya kuungaunga.
Nikamuuliza katibu wa kanisa, shule ikijengwa watoto wa waumini waliochanga pesa zao watasoma bure? Nikajibiwa hapana lazima wachangie.

Sadaka yenye baraka ni ile ya kuwapa wenye uhitaji na sio kuwalimbikizia mali wachungaji.

Mimi wachungaji hawatokula tena hela zangu kizembe.
Watasoma bure kwamba mtakuwa mnaingia ninyi wenyewe madarasani kuwafundisha watoto wenu mkuu?

Maana shule itahitaji walimu,itahitaji vifaa darasa etc.
 
Kuna kitu kilinisikitisha sana siku moja Mchungaji alisema pale madhabahuni kuwa hapa kanisani sio pa kupata msaada unapokuwa na shida ya pesa.... Hii kitu Inaendelea kunipatia tafakari ngumu sana mpaka leo hii...
 
Kwahiyo tunamjengea mchungaji na familia yake shule?🤔 akifa unabaki urithi wa watoto wake?

Kama ni hicyo kwanini asiende kuchukua mkopo bank? Akiwa anapata faida atarudisha
Wachungaji wengi wanawanyonya waumini
 
Sitakaa toa sadaka kanisani au msikitini kamwe.

Sadaka yangu nitatoa katika watu wenye uhitaji wa moja kwa moja..
-- Kuna watu wako mahospitalini walipata magonjwa wameshindwa lipa bili ili watoke na wao ndo baba au mama wanaotegemewa na familia zao(Mtu kama huyu ukaenda uka mlipia bili alafu akatoka akaenda pambania familia yake ) baraka ukazo pata hapa ni mara mia ya ulotoa kwa nabiii.

--Kuna watu kwa kumuungalia tuu unaona anazo shida hata kula ni tatizo japo hajakuomba ila mtu kama huyu ukamtengenezea njia maisha yake yakawa na ahueni ni baraka tosha.
-Niliwahi mkuta mama mmoja yuko njiani amekaa kando ya barabara na mtoto wake kalala pembeni yeye anauza karanga za mia mia zilikuwa kama 20 hivi. Sura inaonesha tuu shida alizokuwa nazo kabisa(ki mahesabu hata akiuza karanga zote faida ni ipi hapo na mtaji ni upi uapo ili aendelee ishi?)

Watu kama hawa ndo unatafuta kibiashara chochote unamletea ambacho kitaendelea mpa zaidi ya kile.(kama masanduku ya kuhifadhi baridi na vinywaji humo ndan na maji ) awe anauza.

Nachokereka makanisani hasa yakinabiii hawana utu kabisaa narudia hawana utu kabisa hakuna hata siku nabii au mchungaji anasemea tutembelee wenye uhitaji.. Kwa upande wa Waislam hilo nawapa hongera wamejitahidi.
Utakuwa sahihi bado. Ila Kila kanisa linalokitambua lina uwazi wa kifedha. Na limechanganua Kila senti destination yake ni wapi. Hocho unachokitaka kinaweza kufanyia pika kupitia makanisani.

Wako watumishi ambao wamejitoa 100% kumtumikia Mungu bila kujishughulisha na shughuli nyingine za vipato. Na wajibu wao wanaufanya kwa nguvu zote. Hawa nao ni amri ya Mungu kuwategemea kwa sadaka na zaka zako.
 
Kuna kitu kilinisikitisha sana siku moja Mchungaji alisema pale madhabahuni kuwa hapa kanisani sio pa kupata msaada unapokuwa na shida ya pesa.... Hii kitu Inaendelea kunipatia tafakari ngumu sana mpaka leo hii...
Makanisa mengi watu ni wachoyo. Ndio maana zamani hekaluni watu walikaa nje wakisubiri msaada. Siku hizi pia hofu za mapato kushuka attention yote inalazimishwa kupelekwa kwa mchungaji.
Makanisa ya awali waikuwa wanasaidiana Sana.
 
hamna, sisi tusioamini hatutoi sadaka,

sadaka si unatoa kumridhisha mungu? sisi hatuna lengo la kumridhisha mungu
 
Back
Top Bottom