Kwa watumishi wa Mungu Joel na Munalove

Kwa watumishi wa Mungu Joel na Munalove

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Wanajamvi katika sakata la kifo cha mtoto Patrick na mkanganyiko juu ya msiba uwe wapi na nani baba halisi wa mtoto kuna huyu mtumishi wa Mungu anaitwa Joel Lwaga. Joel Lwaga mimi namfahamu kama mtumishi wa Mungu aliyeushikilia wokovu na mwimbaji wa nyimbo za injili. Wimbo wake maarufu wa "Sitabaki kama nilivyo" ambao pia ruby aliufanyia cover hauishi kunibariki masikioni mwangu.

Katika hili swala la Muna Joel ametajwa kama bwana wa Muna wa sasa, ukiachilia mbali haijathibitishwa hizi tuhuma kwa Mtumishi wa Mungu siyo nzuri kwani zinalitukanisha jina la Bwana wa Majeshi tunayemuamini.

Pili, Joel alikuwa karibu na Muna mpaka Nairobi alikokuwa anamuuguza mtoto, hata tukichukulia kwamba ni urafiki tu wa watumishi kusaidiana (maana inasemekana Muna naye "eti" ameokoka), kwanini Joel Lwaga hakukaa na Muna kumshauri vyema kuhusu huu mkanganyiko wa baba wa mtoto na sakata zima la msiba?
Kuna maana gani kwa watumishi wa Mungu kuwa pamoja na kushirikiana huku hamshauriani katika maswala nyeti kama haya mpaka yanaleta taharuki kwenye jamii?

Tatu, Joel jana airport amepita kwa kujificha sana huku amejifunika usoni na poll over ni nini hiki? Anahofu ya nini? Ana hatia gani? Biblia inasema waovu ndiyo wenye hofu, hukimbia hata wasipokimbizwa.
Muna na Joel mliyoyafanya yamefanya watu wahoji ukristo wenu na utumishi wenu kwa Mungu. Mtumishi wa Mungu ukifikia hapo ni rahisi hata kulifanya jina la Mungu litukanwe na Roho Mtakatifu akufuriwe(God forbid).
Joel na Muna mjitafakari uhusiano wenu na Mungu na jinsi mnavyolitukanisha jina la Bwana wa Majeshi mnayemtumikia.
muna-389x330.jpg
24294151_2012365865705855_2662816686390277034_n-300x300.jpg
 
Kwani mtumishi wa Mungu hatakiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi? Ikiwa aliingia kwa kujifunika au kutokujifunika hayo ni maamuzi yake binafsi hayahusiani na utumishi wake! Kumsaidia Mona alipokuwa Kenya huo ni ubinaadamu tu ambao huenda umechagizwa na ukaribu wao. Kuhusu kumshauri au kutomshauri wewe na mimi hakuna tujualo huenda alimshauri ila Mona hakutaka kuupokea ushauri huo, huenda hakumshauri na huenda kila kilichofanywa na Mona kimefuata ushauri wa huyo mtumishi. Usiwe mtu wa kulaumu laumu tu kila wakati!!!!
 
Hahaaaaaaahaaa Uko kujificha veeepe km ni jambo la kawaida? Kwanini asiwe huru Tu.
 
Mara nyingi huwa tunasikia watu wakubwa kabisa duniani wanaingia TZ kimya kimya na wanaondoka kimya kimya, hii inamaanisha Kama binaadamu kuna wakati wanahitaji faragha. Kila wakati kuzungukwa na makamera inachosha. Halafu kaja kwenye mazishi ya mtoto na sio kuuza sura! Tatizo tumezoea wasanii wetu ambao wengi ni wa hovyo hovyo huwa wanauza sura hadi kwenye misiba
 
humu hamna shughuli za kufanya? Magufuli itabidi afanye kama museven kuweka kodi kwenye mitandao ya kijamii.
 
Mara nyingi huwa tunasikia watu wakubwa kabisa duniani wanaingia TZ kimya kimya na wanaondoka kimya kimya, hii inamaanisha Kama binaadamu kuna wakati wanahitaji faragha. Kila wakati kuzungukwa na makamera inachosha. Halafu kaja kwenye mazishi ya mtoto na sio kuuza sura! Tatizo tumezoea wasanii wetu ambao wengi ni wa hovyo hovyo huwa wanauza sura hadi kwenye misiba
Hata Joel ni msanii wetu, amekosea sana anautia Dosari utumishi wa Mungu
 
Kwani mtumishi wa Mungu hatakiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi? Ikiwa aliingia kwa kujifunika au kutokujifunika hayo ni maamuzi yake binafsi hayahusiani na utumishi wake! Kumsaidia Mona alipokuwa Kenya huo ni ubinaadamu tu ambao huenda umechagizwa na ukaribu wao. Kuhusu kumshauri au kutomshauri wewe na mimi hakuna tujualo huenda alimshauri ila Mona hakutaka kuupokea ushauri huo, huenda hakumshauri na huenda kila kilichofanywa na Mona kimefuata ushauri wa huyo mtumishi. Usiwe mtu wa kulaumu laumu tu kila wakati!!!!
Mtumishi wa Mungu kuna utaratibu wake wa kujihusisha na mapenzi, hatutegemei Mtumishi wa Mungu kubehave namna hiyo.
 
Mtumishi wa Mungu anatakiwa kujihusisha vipi katika mahusiano ya kimapenzi? Au shida ni kuwa tu na muna?
 
Kwani mtumishi wa Mungu hatakiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi? Ikiwa aliingia kwa kujifunika au kutokujifunika hayo ni maamuzi yake binafsi hayahusiani na utumishi wake! Kumsaidia Mona alipokuwa Kenya huo ni ubinaadamu tu ambao huenda umechagizwa na ukaribu wao. Kuhusu kumshauri au kutomshauri wewe na mimi hakuna tujualo huenda alimshauri ila Mona hakutaka kuupokea ushauri huo, huenda hakumshauri na huenda kila kilichofanywa na Mona kimefuata ushauri wa huyo mtumishi. Usiwe mtu wa kulaumu laumu tu kila wakati!!!!
Brother uko serious kweli kwamba amri ya usizini inefutwa kwenye amri 10 za Mungu?

Kweli hizi ni nyakati za mwisho, hata ukifirwa utatetea ni haki yako kufirwa.
 
Back
Top Bottom