Wanajamvi katika sakata la kifo cha mtoto Patrick na mkanganyiko juu ya msiba uwe wapi na nani baba halisi wa mtoto kuna huyu mtumishi wa Mungu anaitwa Joel Lwaga. Joel Lwaga mimi namfahamu kama mtumishi wa Mungu aliyeushikilia wokovu na mwimbaji wa nyimbo za injili. Wimbo wake maarufu wa "Sitabaki kama nilivyo" ambao pia ruby aliufanyia cover hauishi kunibariki masikioni mwangu.
Katika hili swala la Muna Joel ametajwa kama bwana wa Muna wa sasa, ukiachilia mbali haijathibitishwa hizi tuhuma kwa Mtumishi wa Mungu siyo nzuri kwani zinalitukanisha jina la Bwana wa Majeshi tunayemuamini.
Pili, Joel alikuwa karibu na Muna mpaka Nairobi alikokuwa anamuuguza mtoto, hata tukichukulia kwamba ni urafiki tu wa watumishi kusaidiana (maana inasemekana Muna naye "eti" ameokoka), kwanini Joel Lwaga hakukaa na Muna kumshauri vyema kuhusu huu mkanganyiko wa baba wa mtoto na sakata zima la msiba?
Kuna maana gani kwa watumishi wa Mungu kuwa pamoja na kushirikiana huku hamshauriani katika maswala nyeti kama haya mpaka yanaleta taharuki kwenye jamii?
Tatu, Joel jana airport amepita kwa kujificha sana huku amejifunika usoni na poll over ni nini hiki? Anahofu ya nini? Ana hatia gani? Biblia inasema waovu ndiyo wenye hofu, hukimbia hata wasipokimbizwa.
Muna na Joel mliyoyafanya yamefanya watu wahoji ukristo wenu na utumishi wenu kwa Mungu. Mtumishi wa Mungu ukifikia hapo ni rahisi hata kulifanya jina la Mungu litukanwe na Roho Mtakatifu akufuriwe(God forbid).
Joel na Muna mjitafakari uhusiano wenu na Mungu na jinsi mnavyolitukanisha jina la Bwana wa Majeshi mnayemtumikia.
View attachment 804179View attachment 804180