Kwa watumishi wa Mungu Joel na Munalove

Kwa watumishi wa Mungu Joel na Munalove

Kumbukumbu zangu zinaniambia baada ya kujutenga na Wema na baada ya mwanawe kuumwa mguu, Muna alifanikiwa sana kujitenga na drama za mjini na pia alisema ameokoka je ikiwa ni kweli aliweka nadhiri ya kubadirika bado hakustahili kupendwa na Joel?

Utumishi ina maana kutokuwa na hisia za mapenzi kwa mwakondoo wako hata pale ambapo kanuni za kimaadili zinaruhusu?

Sasa kama hatakiwi kuwa na Muna kisa tu historia ya Muna kimaadili haipendezi, wokovu au kuokoa kuna maana gani? Yaani japo Muna aliokoka bado alitakiwa kuendelea kuhukumiwa kwa historia yake? (Hapa sijagusia hili linaloendelea sasa maana linaleta maswali kuhusu wokovu wake maana huenda alikuwa kwenye drama ila Joel angejuaje kuhusu yajayo)
Muna bado ni mke wa mtu na talaka walokole hawazitambui unasemaje yuko right? Right Mtumishi wa Mungu kutembea na mke wa mtu?
 
Muna bado ni mke wa mtu na talaka walokole hawazitambui unasemaje yuko right? Right Mtumishi wa Mungu kutembea na mke wa mtu?
Madame Flora baada ya kufarakana na Mbasha si aliolewa tena? Au pale walokole walisahau kuwa huwa hawatambui talaka?
 
Kujificha ilikua lazima ajifiche sababu maneno tayari yalikua yameenea kua Muna yupo Nairobi na bwana mwingine anaita Joel unahisi angefanyaje hata kama hawana uhusiano tayari imeshaenea kwenye vichwa vya watu kua ni mtu wake.
 
Thread zote za Umbea wa muna zimeanzishwa na wanaume[emoji3][emoji3][emoji16][emoji16]
Hahahhaha wameumia sana lakini wao wakikataa mimba ni sawa au wakiwaletea wake zao watoto ni sawa.... Muna kawanyoosha.
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia baada ya kujutenga na Wema na baada ya mwanawe kuumwa mguu, Muna alifanikiwa sana kujitenga na drama za mjini na pia alisema ameokoka je ikiwa ni kweli aliweka nadhiri ya kubadirika bado hakustahili kupendwa na Joel?

Utumishi ina maana kutokuwa na hisia za mapenzi kwa mwakondoo wako hata pale ambapo kanuni za kimaadili zinaruhusu?

Sasa kama hatakiwi kuwa na Muna kisa tu historia ya Muna kimaadili haipendezi, wokovu au kuokoa kuna maana gani? Yaani japo Muna aliokoka bado alitakiwa kuendelea kuhukumiwa kwa historia yake? (Hapa sijagusia hili linaloendelea sasa maana linaleta maswali kuhusu wokovu wake maana huenda alikuwa kwenye drama ila Joel angejuaje kuhusu yajayo)
Wewe ni wa kupimwa akili, unazijuwa amri 10 za Mungu?

Na unajuwa kwamba Muna ni mke halali wa Peter?

Huo wokovu wao ni wokovu upi sasa? Mimi siyo Mungu ila hawa ni kuni za motoni za kutuchemshia siye ambao tutakuwa kwenye sufuria.
 
Madame Flora baada ya kufarakana na Mbasha si aliolewa tena? Au pale walokole walisahau kuwa huwa hawatambui talaka?
Hakuna mlokole hapo, hao ni wasanii wa nyimbo za injili hata muislamu anaweza kuwepo kwenye band ya nyimbo za injili kama ni mpiga dram mzuri au gitaa, wengi mpo gizani hamuelewi lolote.

Kanisa la kweli la mitume ni kanisa katoliki tu, hizi NGO zingine zilianzishwa na watu kupingana na ukatoliki.
 
Yaani hawa wanaoimba gospel kwa mahadhi ya bongofleva ndo maana sitaki kuwasikiliza. Wananyoa viduku, wanavaa visuti njiwa vilivyobana na wanaweka video vixens kwny video. Waimbanji wa gospel waliishia kina Mwansasu, malebo na Mwaitege. Wa siku hizi ni wase*** tu. Ndo maana nikitaka kusikiliza kwaya nawasikiliza AICT shinyanga, Cecilia Arusha na SDA kurasini.
 
Wewe ni wa kupimwa akili, unazijuwa amri 10 za Mungu?

Na unajuwa kwamba Muna ni mke halali wa Peter?

Huo wokovu wao ni wokovu upi sasa? Mimi siyo Mungu ila hawa ni kuni za motoni za kutuchemshia siye ambao tutakuwa kwenye sufuria.
kwaiyo wewe mkatoliki utakuwa kwenye sufuria ukichemswa sasa tofauti itakuwa wapi?
 
Ni kifungu gani katika sheria za utumishi wa Mungu alichokivunja Joel?
We nae unapenda ligi, ukiamua kumtumikia Mungu kuna namna unatakiwa kuishi ili kutuonyesha wengine huo utukufu wa Mungu, sio kuishi kihuni kama wahuni wa mtaani. Kasome Biblia vizuri.
 
Pole sana kwa kuamini kuwa waimbaji wa nyimbo za gospel ni watu wachaMungu......refer to Rose,Mbasha F,Bahati Bukuku,Gozbat......hao ni vielelezo halisi vya kuni za motoni.
Mkuu,mbona Bahati Bukuku naona kama ni mtu mshika injili?
BTW;music wa injili ni kazi kama zilivyo kazi nyingine!
 
Mtumishi wa Mungu anatakiwa kujihusisha vipi katika mahusiano ya kimapenzi? Au shida ni kuwa tu na muna?
Mtumishi wa Mungu na Mkristo yeyote ni dhambi kubwa kuzini (kutembea nje ya ndoa) Joel kama anatoka kimapenzi na Muna anatenda dhambi kubwa zaidi ya uzinzi maana Muna bado ni mke wa mtu so ana kosa la kuzini na anakosa la kutoheshimu ndoa. (Ndoa na iheshimiwe na watu wote)
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia baada ya kujutenga na Wema na baada ya mwanawe kuumwa mguu, Muna alifanikiwa sana kujitenga na drama za mjini na pia alisema ameokoka je ikiwa ni kweli aliweka nadhiri ya kubadirika bado hakustahili kupendwa na Joel?

Utumishi ina maana kutokuwa na hisia za mapenzi kwa mwakondoo wako hata pale ambapo kanuni za kimaadili zinaruhusu?

Sasa kama hatakiwi kuwa na Muna kisa tu historia ya Muna kimaadili haipendezi, wokovu au kuokoa kuna maana gani? Yaani japo Muna aliokoka bado alitakiwa kuendelea kuhukumiwa kwa historia yake? (Hapa sijagusia hili linaloendelea sasa maana linaleta maswali kuhusu wokovu wake maana huenda alikuwa kwenye drama ila Joel angejuaje kuhusu yajayo)
Ndoa yake ya kwanza ilivunjika lini? Nikumbushe pia siku waliyofunga ndoa na Joel! Unaentertain uzinzi!!!? Hao ni wazinifu na wana kosa lingine kubwa kabisa la kutoheshimu ndoa. (Ndoa na iheshimiwe na watu wote)
 
Kwani mtumishi wa Mungu hatakiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi? Ikiwa aliingia kwa kujifunika au kutokujifunika hayo ni maamuzi yake binafsi hayahusiani na utumishi wake! Kumsaidia Mona alipokuwa Kenya huo ni ubinaadamu tu ambao huenda umechagizwa na ukaribu wao. Kuhusu kumshauri au kutomshauri wewe na mimi hakuna tujualo huenda alimshauri ila Mona hakutaka kuupokea ushauri huo, huenda hakumshauri na huenda kila kilichofanywa na Mona kimefuata ushauri wa huyo mtumishi. Usiwe mtu wa kulaumu laumu tu kila wakati!!!!
We naye unaongea nini?yaani mtumishi wa mungu naye awe na mahusiano ya ngono na mke wa mtu?/msichana tu bado unaona hakuna shida??baba mtoto ametoa pesa za nauli ya ndege ili mtoto apelekwe nairobi hospital muna na joeli wametumia usafiri wa barabara masaa 14 na mtoto akiwa mgonjwa bado huoni shida?!!peter anasema huyo joel mala nyingi alikuwa ana andaa matamasha kwa kutumia pesa za muna,na kibaya zaidi huyo muna alikuwa anakwenda kwa mzazi mwenzake kuomba pesa kama mkopo ili baada ya tamasha arudishe,na halikuwa harudishi!!unaposema kuwa huenda kila alichofanya muna amepewa ushauri na joeli !!basi itakuwa ndio amemuingiza chaka kwa ushauri huo daaa!!na inasemekana hata account ya instagram ya muna huyo joeri ndio alikuwa anaitumia kuandika mambo ya ajabu wakati wa msiba,na ndiyo yalizidi kuchafua hali ya hewa .huyo joer ni MARIO
 
Back
Top Bottom