Ukitaka mtoto ale inabidi sometimes ujichetue akili uwe ka mtoto, umwimbieimbie akiwa anakushangaa unamwekea kijiko hivohivo utashangaa anamaliza pia jaribu kumbadilishia mlo kila siku usimpe uji kila siku asubuhi unaweza mpa mtori wa ndizi na viazi mixer nyama kama finyango kadhaa na supu yake then unablend, akilala akiamka mpe smooth ya parachichi, embe na ndizi unaweza tia yogurt, siku nyingine ndizi mzuzu ile ya kuiva unaisteam au unaichemsha kidogo ikiiva unaacha inapoa unaweka parachichi na maziwa/yogurt unablend , au viazi mbatata unachemsha vikipoa unablend na yai la kienyeji la kuchemsha .
Watoto wanapenda vyakula tofauti ladha moja huwa zinawachosha. Lakini pia unaweza ukawa unamshikisha vyakula vilaini au matunda kama tikiti anakula mwenyewe .