Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Jamani wakulu,naona mnajadili sana kuhusu afya ya kimwili sana kwa watoto wetu,hivi mnaonaje mkagusia kidogo hili suala mtambuka la ugaynism kwa watoto wetu wa kiume hasa hasa huko mashuleni,tuwalindaje madogo manake kwa kweli hali ni mbaya,ripoti ya mwakyembe imenishtua sana mtima wanje
 
Jamani wakulu,naona mnajadili sana kuhusu afya ya kimwili sana kwa watoto wetu,hivi mnaonaje mkagusia kidogo hili suala mtambuka la ugaynism kwa watoto wetu wa kiume hasa hasa huko mashuleni,tuwalindaje madogo manake kwa kweli hali ni mbaya,ripoti ya mwakyembe imenishtua sana mtima wanje
Asante sana naomba nitarejea
 
Sawa sawa mkuu
Kuna haya machache nayo ni ya kuzingatia mno
. Wasaidizi nyumbani, lazima ujenge tabia ya kutotabirika muda wa kurejea home na uwe mchunguzi wa vitu vidogo vidogo hasa mwendo wa mtoto, tabia zake, mikao yake nk
. Ukaribu na wasaidizi wa nyumbani na watoto pia ni muhimu kuufuatilia kwa karibu
. Ndugu wanaoshinda nyumbani hasa wa kiume jitahidi kuweka mipaka na watoto, hasa kwenye ishu ya kulala pamoja hilo likatae kwa asilimia 100
. Mashuleni
Jiridhishe na historia ya shule hasa kwenye upande wa kashfa mbalimbali
. Muda wao kuingia na kutoka
. Muda wa mapumziko
. Marafiki zake shuleni, mtaani na nyumbani
. Ukaribu wake na walimu wake
. Ukaribu na walimu wake wa dini
. Vitu anavyopendelea je ni sahihi kwa jinsia yake? Nknk
 
Jamani wakulu,naona mnajadili sana kuhusu afya ya kimwili sana kwa watoto wetu,hivi mnaonaje mkagusia kidogo hili suala mtambuka la ugaynism kwa watoto wetu wa kiume hasa hasa huko mashuleni,tuwalindaje madogo manake kwa kweli hali ni mbaya,ripoti ya mwakyembe imenishtua sana mtima wanje
hivi ndivyo mzee wangu alivyonihusia........
[03/04, 19:52] :

La msingi msikubali watoto waje na vitu eti wamepewa shuleni vikataeni wasivitumie kama ukivitilia wasiwasi. Hizi shule kwa sasa ni za LGBTQ!
[03/04, 19:53]

Watoto wanafundishwa ushoga! Kaeni na watoto jueni tabia zao ukiona kuna mabadiliko huyaelewi chukua hatua!
 
hivi ndivyo mzee wangu alivyonihusia........
[03/04, 19:52] :

La msingi msikubali watoto waje na vitu eti wamepewa shuleni vikataeni wasivitumie kama ukivitilia wasiwasi. Hizi shule kwa sasa ni za LGBTQ!
[03/04, 19:53]

Watoto wanafundishwa ushoga! Kaeni na watoto jueni tabia zao ukiona kuna mabadiliko huyaelewi chukua hatua!
Vitu kama vitu gani mkuu?
 
Kuna haya machache nayo ni ya kuzingatia mno
. Wasaidizi nyumbani, lazima ujenge tabia ya kutotabirika muda wa kurejea home na uwe mchunguzi wa vitu vidogo vidogo hasa mwendo wa mtoto, tabia zake, mikao yake nk
. Ukaribu na wasaidizi wa nyumbani na watoto pia ni muhimu kuufuatilia kwa karibu
. Ndugu wanaoshinda nyumbani hasa wa kiume jitahidi kuweka mipaka na watoto, hasa kwenye ishu ya kulala pamoja hilo likatae kwa asilimia 100
. Mashuleni
Jiridhishe na historia ya shule hasa kwenye upande wa kashfa mbalimbali
. Muda wao kuingia na kutoka
. Muda wa mapumziko
. Marafiki zake shuleni, mtaani na nyumbani
. Ukaribu wake na walimu wake
. Ukaribu na walimu wake wa dini
. Vitu anavyopendelea je ni sahihi kwa jinsia yake? Nknk
Naweza nikaongezea
1. Kwenye marafiki shuleni jaribu kumdadisi mwanao tabia za marafiki zake, nani mwenye tabia mbaya, nani huwa anazungumza maneno mabaya, nani huwa anacheza vibaya na wenzake haswa kwenye kushikana, hiii utaipata kama ukiwa na ukaribu sana na mtoto na uwe na desturi ya kuuliza mara kwa mara ili waone kawaida.

2. Fundisha mtoto c kila kitu wanachokiona lazima wakifanye. Haswa kama ulishawaonya kuwa vitu hivi ni vibaya na hivi sitaki kuona mnafanya hata kwa utani. Kwa kusema hivyo utapiga marufuku kucheza michezo ya kukata viuno, singeli, mambo ya uigizaji kuwa mwanamke na uchekeshaji wa kujidhalilisha uaname wake. Piga marufuku na ikiwezekana chimba mkwara mbele ya mama na dada yake. Maana huwa wanawajaza ujinga embu igiza kama mwanamke au katika kama nani...

3. Waambie kabisa kuwa. Muogope Mungu, Mungu anaona unachokifanya hata wewe humuoninkiwa anakuona. Kwa hiyo chochote kibaya ambacho Mungu hapendi ukifanya anakuona ukiwa unawaza kukifanya. Bora nikichape fimbo mimi kuliko Mungu.

Kulea ni kazi kama kazi nyingine

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
hivi ndivyo mzee wangu alivyonihusia........
[03/04, 19:52] :

La msingi msikubali watoto waje na vitu eti wamepewa shuleni vikataeni wasivitumie kama ukivitilia wasiwasi. Hizi shule kwa sasa ni za LGBTQ!
[03/04, 19:53]

Watoto wanafundishwa ushoga! Kaeni na watoto jueni tabia zao ukiona kuna mabadiliko huyaelewi chukua hatua!
Sure
 
Kuhusu gesi especially kwa mtoto mchanga ile ni matokeo ya kupata bloating kama vile mtu mzima anavyopata gesi.

Shida sasa mtoto mchanga kwa umri wake hatakiwi kulishwa kitu nje ya maziwa ya mama yake. So mimi huwa namfanyia massage (kumbinya taratibu) tumbo lake downwards yaani kutoka juu kushuka chini taratibu sana na bila kumuumiza hata yeye utaona anakuwa anajinganyonga tumbo mithiri ya chatu ili tu kuonyesha ushirikiano na ghafla utashangaa kaachia shuzi la maana ambalo muda mwingine linaweza kusindikizwa na uharo. Ukifanya hivi mara kadhaa mtoto hawezi kuwa bloated muda wote.

Shida nadhani inakuwa kwenye maziwa ya mama zao kulingana na ulaji wao wa siku hizi so maziwa yanakuwa na contents zinazosababisha watoto wanakuwa bloated.
 
Kitu kingine ningependa kuchangia ni tabia ya wazazi especially akina mama mtoto akipatwa na kwikwi wao wanamuweka kanyuzi kwenye paji la uso au kwenye komwe.

Kimsingi hiyo ni fikra potofu kwasababu hakuna uhusiano wa kuzuia kwikwi na kumuwekea kinyuzi kwenye paji la uso.

Mtoto anapatwa na kwikwi ikiwa ni matokeo ya kunyonya na kumeza au kuvuta hewa pale anapokuwa ananyonyeshwa na haya ni matokeo ya kunyonyesha mtoto bila kumuweka mkao maalumu wa kunyonyesha. Hewa anayovuta na kuimeza huenda kwenye kifuko cha chakula yaani tumbo na kukaa pale hadi atakapomaliza kunyonya na kwikwi huanza ili ile hewa itolewe ni reaction ya kibailojia sio uchawi wala swala la kiimani.

Suluhu ya hii hali ni kuzingatia kanuni za unyonyeshaji mtoto kwanza kwa kumuweka mkao mzuri wa kunyonya yaani mama utaweka mkono wako eneo la kona ya kipepsi pale mtoto anapoegemea na kumnyanyua kwa level ambayo atakuwa hajalala sana wala kuinuka sana. Huu mkao wanafundisha sana huko clinic.

Unaponyonyesha hakikisha chuchu inakuwa mdomoni halafu ile sehemu nyeusi inafunika vema mdomo wa mtoto ili kusiwe na uwazi wa kuvuta hewa nje ili mtoto apumue kwa kutumia pua.

Ukishajirishisha kuwa mtoto ameshanyonya na kutosheka then muda huo huo (sio baadae wala sio dakika chache baadae au masaa kadhaa baadae) muweke mtoto begani na huku ukimpigapiga kwa utaratibu yaani kupetipeti pale mgongoni eneo la usawa wa kifuko cha chakula au chini kidogo ya shingo hadi usikie amebeuwa hapo sasa ndipo umshushe na kuendelea na shughuli zingine. Hii kazi si lazima afanye mama mtoto tu, anaweza fanya baba, dada, bibi , babu au mtu yoyote ambaye anaweza kusaidia. So kama upo na mume wako mnyonyeshe mtoto halafu dakika hiyo hiyo mpatie baba yake kama wewe unashughuli nyingine unafanya kama kupika na haiwezi kusubiri then yeye atamuweka begani na kumpeti hadi abeuwe.

Kufanya hivi kunamsaidia mtoto kwanza kuepukana na kwikwi kwasababu huwa inamchosha mbavu zake ile kustukastuka. Sasa kama mzazi atakuwa mzembe katika kubeulisha ndipo ataona mfululizo wa kwikwi muda wote na hii ni mbaya sana kwa mtoto sababu inamnyima furaha na kuathiri ukuaji wake,mtoto mwenye furaha huwa anakua na amani.

Pili kunaondoa shida ya mtoto kucheua cheua maziwa na kuchafua nguo zake pamoja na wageni wanapombeba au wewe mzazi unapokuwa nae sehemu anacheua na kuluchafua unaanza kuhangaika kumfuta futa. Pia inaondoa risk ya mtoto kupaliwa na matapishi kipindi hali ya kicheuwa na kwikwi vikikutana kwa wakati m'moja halafu mtoto amelala inaweza sababisha hizi vitu zikamtokea puani ambayo si nzuri maana ina mshtua na kumvurugia mood haraka sana.


Wanawake mjitahidi sana kunyonyesha mkiwa mkao wa kukaa na achaneni na tabia ya kunyonyesha mtoto huku umelala naye hiyo si tabia nzuri. Hata kama ni usiku amka muweke mkao wa kunyonya anza kunyonyesha achacheni na tabia za mazoea kuwa aaaah mbona fulani mtoto wake ananyonyeshwa huku kalala au mbona jana na juzi nilimnyonyesha nikiwa nimelala na hakukutokea shida, sio sawa. Kuti la mazoea ndio humuangusha mgema.

Acha kunyonyesha mtoto ukiwa umelala sio tabia nzuri na inaleta shida za kwikwi na kucheua na hata kuchangia bloating sababu ya gesi kwenda ndani ya utumbo kitokea kwenye kifuko cha chakula. Mbona wewe huwezi kunywa chai, maji, soda, beer au juice huku ukiwa umelala chali , why sasa mtoto unamfanyia hivyo au kwasababu ni kichanga hawezi jitetea na kujisemea kero zake. ACHA HIYO TABIA YA KUNYONYESHA MTOTO HUKU UMELALA NA MTOTO KALALA.
 
mshana jr hiyo ya kumvisha mtoto nguo nyingi sijaelewa, wengne wanasema hiyo ndo inafaa
Sasa wewe upo kwenye chumba ambacho joto lake na wewe unasweat halafu unasema mtoto anasikia baridi inatoka wapo hiyo baridi?

Ukiona tu ndani ya nyumba kuna hali ya joto hadi na wewe mzazi unasikia joto jua na mtoto anasikia hivyo hivyo so andaa nguo nyepesi na ziwe rangi nyeupe maana rangi nyeupe haina tabia ya kutengeneza joto mwilini.

Sio unamvalisha mtoto manguo rundo kama vile yupo Urusi wakati yupo Dar tena kwenye hili joto.
 
Wazazi wengi siku hizi hatuna muda na watoto wetu... Watoto wamekuwa ni wa wadada wa kazi na walimu, makuzi ya mtoto kiakili na kimaadili yanahitaji uwepo na ukaribu wa mtoto kuliko mtu mwingine yeyote yule.

Pamoja na harakati za kimaisha lakini ni vema ni muhimu na kuna wakati kutenga muda wa kukaa na familia yako ili kile ukitafutacho kiwe na manufaa na baraka mbeleni.

Dada wa kazi ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4
Mwalimu ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4 pia
Mzazi ana majukumu yake ambayo ni 1/2

Kwahiyo kama mzazi usibweteke nusu nzima ya malezi ya mtoto inakuhusu wewe.
Balaa linaanzia kuanza kushika ujauzito bila kupanga nini kitakwenda vipi huko mbeleni.

Kunakitu kinaitwa uzazi wa mpango sijui kwann vijana na mabinti wanahisi hili jambo haliwahusu. Sababu ukitazama kwa kina uzazi wa mpango unazo program na maelekezo ya namna life ya uzazi inatakiwa kupangwa from the beginning kabla hata mwanamke hajabeba ujauzito.

Mipango ya mtaishi wapi, nani atakaa na mtoto na mama wa mtoto wakati wa uzazi yaani ile miaka 2 ya kwanza sababu hiki ni kipindi ambacho mwanamke anatakiwa kutoa 100% ya attention yake kwa mtoto muda wote ili akue vizuri na kiwa imara.

BAJETI YA MALEZI YA MAMA NA MTOTO WAKE.

Miezi 6 ya kwanza mtoto hali kitu chochote nje ya maziwa ya mama, so mama anatakiwa kula vizuri ili aweze kuproduce maziwa mazuri kwaajiri ya mtoto. Anatakiwa kupumzika kwa maana kutokuwa na shughuli nje ya mtoto kama kwenda kazini na kadhalika.

Maziwa au lishe ya mtoto atakapo anza kula vyakula nje ya mama yake. Kuna yale maziwa ya kopo kama haujajipanga utaona kama mtoto na mama yake wamekula njama kukufilisi maana mfano mtoto wa kiume anakata kopo moja ndani ya wiki tu maana hawa wanakunywa sana maziwa kuliko wa kike.

Je, kama kama bibie atashika ujauzito na wewe bado upo na mishe mishe atakaa wapi, utapanga nyumba au ataenda kukaa kwa mama mkwe au mama yako? Na je utakuwa unawawezesha kwa namna gani kwa maana ya kuwapelekea mahitaji sio tu mkeo na mtoto ila hata familia husika ambapo mkeo yupo ili ulezi wa mkeo na mtoto uwe na manufaa kwa wote.

Kama itawezekana baada ya mwaka anaweza kufanyiwa mpango wa kwenda gym ili kurejesha uimara wa mwili sababu ya kukaa muda mwingi ndani ili kurudisha mwili na mvuto wake.

Haya yanawezekana kama mtakaa na kupanga mapema. Hivi niwaulize unapokaa na girlfriend wako, mchumba wako au mume wako huwa mnajadili nini nje ya haya maana haya ndio maisha yenu so kama hamjadili nje ya haya it means huwa hamna la maana mnapanga juu ya umoja wenu na kuishi pamoja.
 
Ni kweli mshana jr, itakuwa nzuri maana wazazi wengi wa Kileo kila kitu wanajifunza ukubwani, naamini tutasaidiana kujua malezi ya wanetu...
Na hii ni hatari sana. Hiki kizazi cha wanawake na wanaume wa sasa sijui watakuja wafundisha nini watoto wao aisee mimi nahofia sana .
 
Kati ya mambo yanayonikosesha raha ni jinsi hawa madriver wa hizi school bus walivyokosa umakini waendeshapo watoto wetu.

Nilshuhudia ajali ya bus la shule iliopelekea kupoteza uhai wa watoto watatu hapo hapo...niliumia mno na siwezi sahau tukio lile.

Toka siku hiyo huwa najitahidi sana asubuh kuhakikisha na wadrop watoto wangu shuleni kwao mwenyewe nimeshindwa tu kuwachukua jioni.

Kweli kuna changa moto sana kumlea mtoto hadi akue
Tatizo wanakabidhi madereva wa bodaboda na bajaji kuendesha magari ya shule jambo ambalo ni negligence na irresponsibility.
 
Na hii ni hatari sana. Hiki kizazi cha wanawake na wanaume wa sasa sijui watakuja wafundisha nini watoto wao aisee mimi nahofia sana .
Zemanda asante kwa michango mizuri iliyosheheni elimu na maarifa mengi [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Back
Top Bottom