Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

  • Mtoto anapolialia
  • Mtoto anapopata gesi tumboni
  • Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
  • Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
  • Umeme
  • Maji
  • Moto
  • Mwanga wa Tv
  • Simu, mawimbi yake
  • Vyombo na vitu mbalimbali
  • Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
Za siku nyingi anko, naomba kuuliza dawa nzuri ya kikohozi kwa mtoto anae kalibia kufunga mwaka mana anakohoa mpaka anatapika. Dawa nilizotumia MUCOLYN, ZEN COFFEE, PRINATRIM, hata kama kuna mtu anajua dawa za kienyeji anijuze.
 
Umejaribu kumtibu minyoo kwanza?
 
Za siku nyingi anko, naomba kuuliza dawa nzuri ya kikohozi kwa mtoto anae kalibia kufunga mwaka mana anakohoa mpaka anatapika. Dawa nilizotumia MUCOLYN, ZEN COFFEE, PRINATRIM, hata kama kuna mtu anajua dawa za kienyeji anijuze.
Umemcheki minyoo? Ngoja kuna moja ya kienyeji nikuchekie
 
Za siku nyingi anko, naomba kuuliza dawa nzuri ya kikohozi kwa mtoto anae kalibia kufunga mwaka mana anakohoa mpaka anatapika. Dawa nilizotumia MUCOLYN, ZEN COFFEE, PRINATRIM, hata kama kuna mtu anajua dawa za kienyeji anijuze.
Nzuri Mungu ni mwema Umemcheki minyoo? Ngoja kuna moja ya kienyeji nikuchekie
 
Wazazi na walezi wengi hujisahau kuwapa watoto maji ya kunywa....ukiona mtoto analialia jaribu yafuatayo
-mgeuzegeuze huku ukimminyaminya kila sehemu inawezekana kuna mahali kaumia au amaumwa
-mpe maji
-pengine joto limezidi inabidi umpunguzie nguo au umuweke kwenye hewa
-njaa
-uchovu
-usingizi
Homa nk
Si mara zote mtoto akiwa na mabadiliko yoyote ukimbilie hospitali, ni vema kujiridhisha kwanza kama kuna uhitaji wa kwenda hospital
Mtoto wa miezi 2 anapaswa kupewa maji ya kunywa?
 
Mtoto wangu wa mwezi mmoja nanusu amepata mafua, yanamsumbua wakati wa usiku, halali kabisa kila muda anastuka anashika pua analia, unaona kabisa yanamtesa.. Tumeenda hospital wamempa dawa ya Amoxilyn Syrup.. Hamna njia nyingine ya kumsaidia ? Please help yoyote aliewahi kupitia hii situation..
 
Kitunguu saumu na maji ya vuguvugu yenye chumvi muogeshee
 
Mtoto wangu wa mwezi mmoja nanusu amepata mafua, yanamsumbua wakati wa usiku, halali kabisa kila muda anastuka anashika pua analia, unaona kabisa yanamtesa.. Tumeenda hospital wamempa dawa ya Amoxilyn Syrup.. Hamna njia nyingine ya kumsaidia ? Please help yoyote aliewahi kupitia hii situation..

Kama uko sehem ambapo NAKIETE wapo, nenda wanadawa ya mafua nzuri kweli unampakia anapolala
Wanauza kimoja 2,000
Pia hakikisha usafi muda wote sehem anapolala kusiwe na hali ya vumbi vumbi
 
Za siku nyingi anko, naomba kuuliza dawa nzuri ya kikohozi kwa mtoto anae kalibia kufunga mwaka mana anakohoa mpaka anatapika. Dawa nilizotumia MUCOLYN, ZEN COFFEE, PRINATRIM, hata kama kuna mtu anajua dawa za kienyeji anijuze.

Kamuangalie pia kimeo (wakati mwingine husababisha mtt kukohoa sana na kutokula)
 
Back
Top Bottom