Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wale wenye watoto wanaosoma
-ni lazima na ni muhimu kumpa namba zenu wazazi au kuziandika kwenye begi lake ni muhimu na zimesaidia wengi
-kumuonya tabia ya kuombaomba na kuwa makini na watu asiowajua. ..watoto wengi wanaopotea hupotea kwa staili hizi
Hawa watoto wanaosoma ni vema kuzifuatilia nyendo zao kwa karibu tabia zao marafiki walionao na vitu walivyo navyo kwenye mikoba na vyumbani mwao
mimi sio kuandika tu bali nilimkaririsha namba za mimi na mama yake na bibi yake na hii ilisaidia siku moja alienda na shangazi yake kutembea sabasaba wakapotezana akapelekwa akamuomba mama mmoja ampigie simu mama yake then mama yake akampigia shangazi yake ili aende kwenye hilo banda amchukue
 
Nimejifunza kitu hapa
 
Mada zako mshana jr nyingi ni nzuri na zenye mafunzo mazuri ila nadhani humu wengi ni vijana ambao hawajaanza kulea na mara nyingi mada kama hizi wachangiaji wanakuwa si wengi sana lakini weka mada ihusianayo na ngono uone!
Kijana wa leo mzazi wa kesho wapite wajifunze.
 
mimi sio kuandika tu bali nilimkaririsha namba za mimi na mama yake na bibi yake na hii ilisaidia siku moja alienda na shangazi yake kutembea sabasaba wakapotezana akapelekwa akamuomba mama mmoja ampigie simu mama yake then mama yake akampigia shangazi yake ili aende kwenye hilo banda amchukue
Mkuu ulimkaririsha akiwa na umri gani? nimeipenda hii.
 
Hebu tujikumbushe na hili la watoto kukojoa kitandani usiku
Ukiachana na tatizo la sphincters kulegea na kuruhusu mkojo kupita bila kizuizi ambalo hili ni tatizo la kitabibu, unaweza kumfanya mwanao asikojoe kitandani kwa wale watoto ambao tayari wako kwenye umri wa kujitambua
Unachofanya ni rahisi sana japo kina karaha zake
Unamzoeza kumuasha usiku kila ifikapo muda fulani kwa mfano saa nane usiku na kumpeleka kujisaidia
Ni zoezi lenye ugumu wake hasa kwa wafanyakazi lakini unachofanya unategesha alarm ili nawe usipitiwe, ukiweza kulifanya hili kwa wiki mbili mfululizo baada ya hapo hutahangaika kumuamsha
 
Lingine la muhimu sana ni kuacha tabia ya kumlazimisha mtoto kutumia mkono fulani hasa kwenye kuandika nk
Kuna watoto kiasili wamezaliwa kutumia mkono wa kushoto huna haja ya kwenda kinyume na asili
 
Hili lilinisumbua kidogo kwa mwanangu wa kwaza kwani hadi kula alikua anatumia kushoto na kulia nikaweza kumlazimisha awe anakula na kwa mkono wa kulia,ila kwenye kuandika anatumia mikono yote miwili na sikumzuia.
 
Hapo ulifanya vema sana hasa ukizingatia mila na desturi zetu kwenye kula na kusalimiana
 
Afadhali nimeiona hii thread wakati muhafaka maana juzi hapa siku mbili zimepita tukiwa tunaangalia tamthilia moja mida ya jioni Mdogo wangu wa kike yupo around 17 yrs alikuja kunitembelea jioni akiwa ameambatana my uncle kasichana kama 13 au 12 yrs hivi

Nikawa nawapa mafundisho Mara ikaingia maada ya Amri kuu za mungu, wakati nazitaja ilipofika amri ya 6 nayo nikaitaja lakini bila kusita kale kabinti kakadakia na kuniuliza "hivi uncle Kuzini maana yake nini? maana nasikia sana watu wakilisema neno hili" duh wote tulistuka na nilipigwa na butwaa na kuona noma ,kwakweli nilizuga tu na kumwambia ni kufanya mapenzi na uchafu ambao haumfurahishi Mungu ,akaangalia chini kwa kuona aibu

Je,mtoto kama huyo ni majibu ya aina gani ambayo anapaswa kupewa katika kipindi kama icho na je nilikosea kumjibu hivyo
 
Makuzi ni muhimu na yana impact kubwa sana kwa mtoto...hapo majibu yako yatategemea mtoto amelelewa katika malezi gani
-ya mtaani?
-ya kidini?
-ya kuhoji bila kutafakari?
Kwa jibu ulilomjibu bado ulikuwa kwenye njia sahihi
 
Kwa hisani ya mama kubwa naomba niliseme hili
Nina imani kabisa wengi wetu hatujui madhara ya kumlaza mtoto na mto , lakini kumbe haishauriwi kabisa kwakuwa mtoto anaweza kujigeuzageuza na kufunikwa na mto ambao unaweza kumziba pumzi na kumletea madhara makubwa hata kifo
 
Kuna hivi vitu sijajua vina ithibati kiasi gani
-maziwa ya mama kuwa na mafuta mengi
-maziwa ya mama kuwa mepesi/mzito
-mtoto kupenda ziwa moja zaidi ya lingine

Mkuu @mshanajr naomba nikujibu kipengele cha mwisho. Sababu na mtoto kupenda ziwa moja zaidi ya jingine...

Mama anaponyonyesha inatakiwa anyonyeshe maziwa yote mawili. kwa muda sawa kama ni dakika 15 -20 asije nyonyesha ziwa moja kwa wingi kuliko jingine ,hilo asilo nyonyesha litakuwa dogo na hilo jingine litakuwa kubwa kiasi cha kwamba akiva nguo itaonyesha utofauti , mtoto hatolitaka kunyonya tena sababu maziwa yake yatakuwa yamechacha kutokana na kutonyonywa mara kwa mara,kila akimnyonyesha atahisi machungu na kukataa. Hii ndio sababu inayopelekea mtoto kukataa ziwa moja.
 
Asante sana charminglady na hongera kwa kujifungua salama Glory be to God
 
Shukrani sana mkuu, tuko pamoja. Tutaendelea kujuzana mengi katika hii mada maana niko "Live".
c224b1ac88859cb0ddd99455ebfaf518.jpg

Barikiwa mno pamoja na kichanga bila kumsahau baba
 
Back
Top Bottom