Transistor
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,061
- 1,637
- Thread starter
- #41
Kijana akiwa site!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli;Itabidi ushauri namna gani tutakabiliana na Hilo;kwasababu hatari hiyo ipo kwenye sector nyingi za utafutaji.MMMhhh Risk ya kuzunguka na kibasikeli chako umebeba na mashine na pesa kusaka wateja ni kubwa sana!
Kijana salehe [emoji23] [emoji23] anayoa sikuhizi daah.Hapa ni ofisi ya kijiji cha vikumburu wilaya ya kisalawe.Kijana Salehe akikabidhiwa mtambo na mashine yake mbele ya Afisa mtendaji wa kijiji hicho.
Tayari ambao wako ndani ni watatu ukijumuisha na mimi mwenyewe.
Hivyo tuna 150,000/- Ahadi bado 650,000/-Tupate mashine moja na vifaa vyake.
Ambapo tutakuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa kijana 1.
Tuendelee kusapoti wazo wadau au kama kuna ushauri na maoni yanahitajika.
MCHANGANUO WA UWEKEZAJINilishakwambia tokea kitambo kuwa wewe ni Millionaire haujajua tu.
Pia si lazima iwe 50,000/- hicho kinaweza kuwa ni kiasi cha kuanzia. Mnaweza ruhusu watu wenye uwezo hata wa kutoa 200,000/- ilimradi mgawango wa faida uzingatie uwiano wa kiasi cha uwekezaji.
Nilishakwambia tokea kitambo kuwa wewe ni Millionaire haujajua tu.
[emoji3][emoji3][emoji3].
ukweli mchungu kwamba hapa ndio nimejua maana hasa ya 'hisa' 😀MCHANGANUO WA UWEKEZAJI
Mtaji ni Tsh 800,000/- kwa project 1
Kiasi cha chini cha uwekezaji mtaji ni 50000 kwa project 1
IDADI YA HISA
Mtaji mkuu 800,000 ÷ kiwango cha chini cha uchangiaji 50,000 = jumla ya hisa 16
Mwekezaji anaweza kununua zaidi ya hisa 1
Kwa mtaji wa 800,000;kadilio la kati la faida kwa mwezi ni 120,000
Faida ÷ idadi ya hisa
120000 ÷ 16 = 7500
Gawio la kati la faida kwa kila hisa ni = 7,500 kadilio la juu 8,000 kadilio la chini 5,000
Kwa maelezo zaidi rejea katika mchanganuo wa mradi.
Maswali zaidi uliza
Habari wakuu,twende katika hoja.
Napendekezo la kushirikisha wadau wenye mitaji kuanzia 50,000/- na kuendelea tuungane katika uwekezaji katika mradi wa nishati inayo tembea (mobile energy).
Project ambazo nitaziwakilisha hapa tayari binafsi nimesha zijaribu na kuona kuna fursa lakini pia marrjesho ya uhakika ya kiuchumi.
1.MRADI WA MTAMBO WA KUENDESHA MASHINE YA KUNYOLEA (MOBILE BARBER) INAYO TUMIA MFUMO WA SOLAR (mradi huu umesha jaribiwa na unaweza kuhakikiwa).
Mitambo inayotunza umeme ambayo itatumika katika kuendesha mashine za kunyolea maeneo ya vijijini.
Mtambo huu unakuwa unaweza kubebeka katika baiskeli,ambapo kijana wa kunyoa anakabidhiwa vifaa vifuatavyo
i.Mtambo wenyewe
ii.Baiskeli
iii. Vifaa vya kunyolea (mashine,kioo,dawa n.k)
UTENDAJI WA KIBIASHARA.
Kijana anakua akitembea na baiskeli katika kaya mbalimbali kutoa huduma ya kunyoa,ambapo anakuwa na uwezo wa kutembelea vijiji vya jirani ili kutoa huduma hiyo.
Pia atakuwa akitumia mikusanyiko ya minada,mashule na vilabu vya pombe kutoa huduma hiyo.
UPATIKANAJI WA KIJANA WA KUNYOA.
Kwa majaribio nilio fanya katika vijiji hua kuna vijana ambao wananyoa kwa kutumia vitana na wembe,mara nyingi hao ndiyo huwa wanafahamiana na wateja wengi wa kunyoa wa maeneo hayo na pia hao huwa rahisi kufundishika kutumia mashine ya umeme kunyoa.
Baada ya kumpata kijana huyo mnakubaliana katika malipo na mnaenda kukabidhiana na kuandikishiana katika ofisi ya kijiji ambayo huyo kijana ni mkazi.
Baada ya hapo unamkabidhi baiskeli na mtambo na vifaa vyake.
GHARAMA ZA MTAMBO MMOJA.
i. Mtambo na mashine yake ya kunyolea jumla ni 620,000/-
ii. Baiskeli 150000
iii.Vifaa vingine 30000
JUMLA Tsh 800,000/-
MAPATO NA MFUMO WA KUYAKUSANYA.
Mtambo huu umewekwa kifaa ambacho kinapima matumizi ya mtambo kwa masaa.
Jinsi mashine inavyofanya kazi ndivyo kipimo kinavyo soma,Kwa mashine moja ya kunyolea kipimo kitasoma point 1 baada ya mashine ya kunyolea kufanya kazi kwa masaa masaa 10,na point 2 baada ya masaa 20 na itaendelea hivyo hivyo kulingana na masaa.
Siyo lazima mashine ifanye kazi kwa masaa 10 mfululizo hapana hata kama inawashwa na kuzimwa mfano.
Mteja wa 1:kanyolewa dakika 45
2:Kanyolewa dakika 30
3:Kanyolewa lisaa 1
JUMLA itakua masaa 2 na dakika 15,hivyo itakua bado masaa 7 na dakika 45 kutimia masaa 10.
Baada ya kutimiza masaa 10 ya kazi kipimo kitaandika point .
Hivyo makubaliano ya malipo yatakuwa kulingana na pointi ikiwa na maana unaweza kukadilia kila lisaa 1 la kazi iwe unalipwa 1000/= kwa masaa 10 ya kazi utalipwa 10,000/=
Mita ya malipo itasoma muda pale tu wakati mashine ya kunyolea imewashwa. Na itasimama mashine ya kunyolea ikizimwa.
Hivyo kutokana na mfumo huu ni rahisi kufatilia malipo na kuepuka udanganyifu.
Unaweza ukawa unakusanya malipo yako baada ya kila pointi kadhaa ukijua kabisa kila pointi 1 ni sawa 10000 n.k
MAJARIBIO YA MASHINE NA WAZO LA MRADI.
Baada ya kuunda mashine hii niliitangaza hapa kwa kuiuza ila wadau wengi walionekana kuto zingatia sana sababu ni kitu kipya na baadhi wakawa waoga kujaribu.
Hivyo nikachukua jukumu la kuipeleka mashine field na kuangalia utendaji wa kazi na marejesho.
Kuna kijiji kipo wilaya ya kisarawe mkoa wa Pwani ambapo Mashine imepelekwa kule ambapo nikapata msimamizi na kinyozi.
Wastani wa mapato kwa wiki ni Tsh 50000
- Ambapo siku za minada ananyoa hadi 17,000/- kwa bei ya mkubwa 1000 mtoto 500. Ambapo kwa kule minada ni siku 2
Na siku za kawaida ananyoa kati ya 7000 hasi 10000 kati ya vijiji viwili hadi vitatu anavyo tembelea.
Tulivyo kubaliana kinyozi anachukua asilimia 40 ya mapato
Na mwenye mashine anachukua asilimia 60 ya mapato.
Hivyo kinyozi anachukua 2800 kwa siku sawa na 20000 kwa wiki sawa na 85000 kwa mwezi.
Mwenye mashine atachukua 4200 kwa siku sawa na 30000 kwa wiki sawa na 128000 kwa mwezi.
Uchangamfu na speed ya kinyozi,mazingira ya mabonde na milima,na idadi ya watu,idadi ya kaya,uwepo wa shule vinaweza kuathiri makadilio haya chanya au hasi.
Hivyo nashauri wadau ambao wanalengo la kuthubutu tujiunge tutengeneze kikundi,cha mradi huu.
Wadau tukutane tujuane tujue tunaweza kuwekeza kiasi gani,tutembelee kule ambako mashine ya majaribio imewekwa kwa uhakika na kujifunza zaidi.
Ikionekana tija ya jambo hili tunaweza unda uongozi wa kikundi tukafungua akaunti ya kikundi na watu wakaamua kuwekeza katika mradi huu.
UPDATE
WHATSUP LINK
......................
![]()
.................
Mtambo wa kuendesha mashine ya kunyolea bila uwepo wa umeme wa TANESCO ni mkombozi kwa wajasiriamali wa saluni za kunyoa
Kutokana na changamoto za umeme kukatika katika au baadhi ya maeneo kutokuwa na umeme Nimebuni mashine hii ambayo itamwezesha kinyozi kuendelea na shughuri yake ya kunyoa bila kujali umememe upo au haupo. Mashine hii inatumia nguvu ya jua ambayo inahifadhi umeme katika bank ya umeme...www.jamiiforums.com
View attachment 1210881
Kwa maelezo ya miradi hii pakua pdf hii