Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 16,096
- 49,651
Habari za Muda huu Wakuu!
Kadri Umri unavyosogea, na majukumu yanapoongezeka ndivyo tunavyozidi kutafuta namna mpya ya kuwekeza ili kupata Uhuru wa Kiuchumi (Financial Freedom) kuelekea kwenye Umri wa Uzee.
Kwa muda mrefu nimekuwa nawiwa kufanya uwekezaji kupitia kujenga na kumiliki Kituo cha Mafuta (Fuel station ).
Nia ninayo, ila wasiwasi wangu ni kwenye mtaji halisi unaohitajika kufanikisha uwekezaji huu.
Binafsi nina milioni 50 ambazo nadhani naweza kuzitumia kwenye shughuli za awali ikiwemo Ujenzi n.k
Nina kiwanja nimenunua mahali ekari 5, na ni barabarani (Barabara ya Dsm - Mbeya).
Kwa kuwa mtaji wenyewe hautoshi, nafikiria kukopa Benki na kuweka dhamana Lodge yangu ya vyumba 8 niliyonayo.
Kuhusu vile vibali vya Nemc na Ewura, nina connection kule ya jamaa tunaofahamiana, kwahiyo nahisi nitatumia gharama kidogo kufacilitate mchakato.
Kutokana na ufinyu wa mtaji, nafikiria kujenga pump station 3 mbili za Petrol na Moja ya Dizeli. Pia ili kuongeza Wigo wa biashara, napanga kufunga compressor kwaajili ya upepo pia kujenga kibanda kwaajili ya kuosha magari (car wash).
Nitaanza na matenki ya kutunza mafuta ya ukubwa wa lita 10,000 kwa petrol na lita 5,000 dizeli.
Kwa kuwa ndiyo naanza biashara nitatumia magari ya kukodi kuniletea mafuta.
Ili kupata kujua gharama halisi za uendeshaji nitatenga shilingi milioni 15 kwaajili ya mishahara (ya miezi 8) ya pump attendants 5, mlinzi na Cashier ambaye nafikiria atafanya na kazi ya uwakala hapo hapo.
Karibuni kwa michango yenu ya mawazo ili kuboresha biashara hii, na pengine kunishauri kuachana na wazo hili la biashara kabla sijatumbukiza hela zangu.
Natanguliza shukrani za dhati 🙏🙏