kirikou1
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 4,815
- 6,517
Comment safi sana hiiAisee usijaribu utajiri wa ndumba una masharti magumu balaa.
Fikiria una utajiri wa Bilioni mbili lakini huruhusiwi kulala kitandani au huruhusiwi kupanda gari.
Una utajiri mkubwa lakini hutakiwi kuvaa viatu vya kufunika au unataka wa kuvaa malapa.
Kuna tajiri mmoja alikua na sharti la kutovaa viatu, ikatokea akapata emergency ya kwenda Dar es Salaam haraka ikabidi apande ndege. Alipofika kwenye ndege wakamzuia coz amevaa malapa wakamwambia avae angalau sandals.
Akavaa sandals akasafiri, kufika Dar es Salaam anapewa taarifa magari yake yamepata ajali na mali zimeungua moto.
Bado alikua ametoa kafara ndugu Zake wengi lakini mwisho wa siku akapoteza mali zake na ndugu Zake pia aliowatoa kafara.
Katika maisha chagua vitu viwili pesa au amani(furaha). Kama kipaumbele chako ni pesa sio amani unaweza kutafuta utajiri kwa waganga utaupata lakini utakua na maisha yasiyo ya furaha.
Kama Amani kwako ni muhimu fanya kazi kwa jasho lako usitegemee waganga.
Usisahau kujihusisha na waganga ni kutengeneza maagano ambayo kuyavunja ni ngumu.
Baki na imani yako.
Hakika amani na furaha ndio kila kitu hapa duniani. Fikiria umeua ndugu na familia mwisho wa siku na utajiri umepotea.